Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Tumepokea vyema taarifa za kuachiliwa kwa viongozi wa vyama vya siasa, vijana, waandishi wa habari, na mawakili waliokamatwa walipokuwa wakitaka kutekeleza haki yao ya kikatiba ya uhuru wa kukusanyika kwa amani.
Pia soma: Mbeya: Polisi yawaachia Viongozi na Wanachama wa CHADEMA kwa dhamana, baadhi wakwama
Marekani inaunga mkono kwa nguvu zote haki za msingi zisizoweza kupokwa za uhuru wa kujieleza na kukusanyika kwa amani kwa wote kama ilivyowekwa katika katiba za nchi zetu zote mbili, na ambazo ni muhimu kwa nchi zote za Kidemokrasia.
Tunatoa wito kwa serikali, vyama vyote vya siasa, asasi za kiraia, na wananchi kudumisha na kuheshimu haki hizi, na kushirikiana ili kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unakuwa huru, wa haki, wa amani, jumuishi, na wenye uwazi unaoakisi matarajio na matakwa ya wananchi wa Tanzania.
Pia soma=> Kuelekea 2025 - Ubalozi wa Marekani: Tumeshtushwa na taarifa za kuaminika kwamba polisi walitumia nguvu kupita kiasi kuwadhibiti CHADEMA