Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,966
- 11,218
Mabalozi wote wana muongozo wa kufanya kazi kutoka wizarani awakurupuki tu na kujiamulia. Ndio maana kama swala lipo juu yao na la msingi limeibuliwa watakwambia tutawarudishia wizarani au taasisi husika walifanyie kazi.Hizi ni fikra zako ukweli ni kwamba jumuia ya dallas imejitambulisha toka 2009. Imesajiliwa rasmi, viongozi wametoa mawasiliano yao balozini. Isitoshe wametuma list ya watu zaidi ya 120 wanataka passport tena wiki jana tu. Wamefanya kila kitu hivyo hakuna kisingizio. USA kuna jumuia za Watanzania nyingi sana ni nchi kubwa hivyo ukitoa mifano toa mifano kamili na uwe na facts.
Clearly kwa maelezo yako Dallas kuna jumuiya ya watanzania, but then zipo ngapi? na viongozi wanaojulika ni wangapi.
Kuorodhesha jumuiya ubalozini ata mimi naweza kutoka mji wowote na ubalozi isijue kiongozi wa jumuiya zote ni yupi kama kuna jumuiya kadhaa kwenye mji mmoja.
So wao wana contact wote na kuwapa rank sawa kama kuna jumuiya nyingi sometimes wanatoa mwaliko kwa watanzania wote ili kuondoa migongano ya favouritism.
Hoja za US haziko mbali na nchi nyingine yeyote.
Swala la passport US ina states ngapi na cities ngapi zinazokaa watanzania? Unataka ubalozi ufanye kazi ya kuzunguka nchi nzima na watu wanaomba passport kwa muda wanaojisikia wao hiyo manpower wanayo? halafu who’s to cover those costs.
Ni hivi from what I gather viongozi wa jumuiya yenu awajaongea na ubalozi kupewa ufafanuzi kuhusu maswala ya passport na kama wamefanya ivyo they haven’t shared that info with the group.
Ubalozi ahusiki na maswala ya passport ilo ni jukumu la uhamiaji pekee Tanzania. Wao ni kama stop centre tu ya finger print na kutuma info.
Mikakati yote ya wao watakavyofanya kazi ugenini ni maelekezo kutoka uhamiaji upande wa Tanzania. Ata siku ukipewa appointment ukienda ubalozini system ikiwa down wanaelewa nauli yako, usumbufu wa kulala ikibidi na mengineo; lakini sytem ipo controlled Tanzania sio wao.
Hayo malalamiko wanapokea sana na washawarudishia wahusika, ila wenyewe Tanzania are not bothered and there is nothing the embassy can do.
Badala ya kudhania ubalozi unajifanyia mambo tu muwe mnapiga simu mpewe maelezo ya kina na wahusika kwenye hoja zenu sio kutoa lawama za jumla jumla.