Ubalozi wa Tanzania US ni vituko tupu

Mabalozi wote wana muongozo wa kufanya kazi kutoka wizarani awakurupuki tu na kujiamulia. Ndio maana kama swala lipo juu yao na la msingi limeibuliwa watakwambia tutawarudishia wizarani au taasisi husika walifanyie kazi.

Clearly kwa maelezo yako Dallas kuna jumuiya ya watanzania, but then zipo ngapi? na viongozi wanaojulika ni wangapi.

Kuorodhesha jumuiya ubalozini ata mimi naweza kutoka mji wowote na ubalozi isijue kiongozi wa jumuiya zote ni yupi kama kuna jumuiya kadhaa kwenye mji mmoja.

So wao wana contact wote na kuwapa rank sawa kama kuna jumuiya nyingi sometimes wanatoa mwaliko kwa watanzania wote ili kuondoa migongano ya favouritism.

Hoja za US haziko mbali na nchi nyingine yeyote.

Swala la passport US ina states ngapi na cities ngapi zinazokaa watanzania? Unataka ubalozi ufanye kazi ya kuzunguka nchi nzima na watu wanaomba passport kwa muda wanaojisikia wao hiyo manpower wanayo? halafu who’s to cover those costs.

Ni hivi from what I gather viongozi wa jumuiya yenu awajaongea na ubalozi kupewa ufafanuzi kuhusu maswala ya passport na kama wamefanya ivyo they haven’t shared that info with the group.

Ubalozi ahusiki na maswala ya passport ilo ni jukumu la uhamiaji pekee Tanzania. Wao ni kama stop centre tu ya finger print na kutuma info.

Mikakati yote ya wao watakavyofanya kazi ugenini ni maelekezo kutoka uhamiaji upande wa Tanzania. Ata siku ukipewa appointment ukienda ubalozini system ikiwa down wanaelewa nauli yako, usumbufu wa kulala ikibidi na mengineo; lakini sytem ipo controlled Tanzania sio wao.

Hayo malalamiko wanapokea sana na washawarudishia wahusika, ila wenyewe Tanzania are not bothered and there is nothing the embassy can do.

Badala ya kudhania ubalozi unajifanyia mambo tu muwe mnapiga simu mpewe maelezo ya kina na wahusika kwenye hoja zenu sio kutoa lawama za jumla jumla.
 
Mama kajaza vilaza wa kizanzibari kila mahali, awamu ya tano ilikuwa ya wasukuma na kanda ya ziwa, awamu hii ni ya wazanzibari na waislam
 
Mama kajaza vilaza wa kizanzibari kila mahali, awamu ya tano ilikuwa ya wasukuma na kanda ya ziwa, awamu hii ni ya wazanzibari na waislam
Tena aliyesaini barua Anaitwa ....S.Hassan
Kwa haraka haraka anaweza kuwa mwanafamilia Namba 1 ya Tzie.
 
Tuyaache haya ya ubalozini ni mbali sana.
Tuje hapa nyumbani, ni mara ngapi unaenda ofisi ya umma unapewa jibo boss yahupo, au file halionekani? Kumbukeni enzi zile za wastaafu kufuatilia majadalada ili wapewe mafao yao.

Kuna nyakati ulikuwa unafika ofisini unakuta wahusika/mhusika kaenda kunywa chai. Kwa ujumla mfumo wa utumishi wa umma unahitaji kuwa revamped.

Wapo watumishi wa umma wanafanya kazi na kazi zao zinaonekana, ila kuna ofisi zingine, labda waje malaika toka mbinguni wasaidie mambo yaende.

Poleni mlio nje ya Tanzania, na tuendelee na Tanzania yetu; ipo siku tutafika, ila isiwe tunafika tumechoka sana au tumechelewa sana.
 
Nepotism. Unampeleka mtoto wa dada na shangazi ubalozini what do you expect. kingine ni budget yao ndogo sana. Ofisi zetu nyingi za ubalozi unakuta zimechoka ile mbaya mpaka unaona aibu. I dont know what is wrong with us. Ninafikiri kuna makosa yalifanyika hapo mwanzoni kwa kutokuwa na foundation nzuri kama taifa. Hii nchi inhitaji mapinduzi ya kiakili, kiuchumi na kisiasa na nachelea sijui tutapata wapi hao watu maana wote vichwa vyetu vinafanana tu kwa sasa. Ukiangalia viongozi tulio nao kwa sasa sijui wanatupeleka wapi. Mama alitaka kuonyesha njia lakini ninaona mshumaaa ukimsimikia kwa haraka sana. Lakini Bado tutaendelea kumwomba Mungu uenda akatupa viongozi wenye hekima ya uongozi waweze kututoa hapa tulipo.
 
Nimewahi kupeleka kesi moja hivi ya kudhurumiwa na kampuni moja ya nchi hiyo hiyo ambapo Mimi nilipeleka kesi hiyo ili nipate msaada zaidi!!!

Ndipo nilipoelewa Ni kwa Nini umasikini wa kitumwa Ni vigumu kuondokana nao

Mpaka leo hakujawahi kupatikana jibu na ukiwapigia kufahamu Ni wapi suala Hilo limefika, smu zenyewe huita tuu bila kupokelewa

U$ 17,000+ zimepotea hivihivi, sjui wamekulaga wao
.?
 
Hao kitaalamu wanaitwa "chawa pro"
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Yaani wakikuona tuuu wabajidistance.Hii ni hatari kubwa Sana asee tena ugeniniii
 
Siyo USA tu. Ni dunia nzima. Sisi ambao tumeishi nchi mbalimbali ughaibuni tunalijua hilo. Wala huwa sina mpango nao. Nikiwa nje wala huwa sitaki kufahamiana nao. Hawana msaada wowote. Wapo kwa ajili ya kujihudumia wenyewe na familia zao tu.
Duuuub 😰😰😰😰 hatari tupu
 
Siyo USA tu; balozi nyingi sana za Tanzania duniani ni za hovyo tu. Niliwahi kutembelea ofisi fulani ya ubbalozi wetu nikakutana na mtu aliyetaka nitambue kuwa yeye ni "mtu mkubwa" niongee naye kwa heshima! Kewa heshima yangu na kwa uungwana nikamwambia kuwa nilipita kusalimia tu kwa vile niliona bendera ya Tanzania huku ughaibuni, ila bado niko kazinii: kwa heri nitatafuta siku nyingine kutembelea wakati siko kazini!
 
Nilishaujua huo ubalozi.....Kuna dogo aliwahi kwenda kujisalimisha ubalozi wa UK in the name of Common Wealth na akasaidiwa.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…