Ubalozi Wetu DC...Pasipoti Yangu...

Ubalozi Wetu DC...Pasipoti Yangu...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Kwa kweli nimetiwa moyo na weledi, haraka, na utendaji ulioweza kufuatiĺia Hati ya kusafiria ya mdogo wangu Mange aka Damdogo. Licha ya kuchelewa kurenew lakini mambo ya ndani wameweza kushughulikia Hati yake kwa haraka.

Na mimi nilishakamilisha kila kitu ili kupatiwa Hati yangu ya kusafiria ili nije kuungana na Watanzania wenzangu kujenga nchi yetu.

Nilikamilisha taratibu zote tangu Novemba 2019. Miaka miwili kamili imepita bila kupatiwa Hati hiyo.

Natanguliza shukrani kama watalishughulikia na hili...kwa weledi uleule kama kwa damdogo.

Ntashukuru
 
Kumbe tatizo lako lilikuwa ni passport, shida yako ilikuwa nini mpaka wakuzuie muda wote huo kuipata? au uanaharakati wako wa miaka ile but si ulikuwa unatumia fake id?! au sababu ni urasimu tu wakawaida.
 
Shida wewe hujasimama waziwazi kuponda upinzani nakumuunga mkono Samia au kumponda hayati magufuri wazi wazi nakumuunga mkono Samia hivyo hatuwezi kukupa hiyo hati.Kama ungekuwa umwungana na kigogo kuoambana na hayati magufuri ..tungekupa.Tunaomba ufuate njia alizotumia mage
 
Hebu mu DM dada wa Taifa arushe malalamiko yako kwenye page yake utashughulikiwa haraka sana..

Yule Dada anaushawishi mkubwa sana kwenye serikali ya Chifu Hangaya.
 
Kwanini umeamua kurudi bongo mkuu? mie ningekuwa state hata kwa bunduki nisingerudi Afrika.
 
Karibu sana Mzee Mwanakijiji, Welcome home, It always feels good to be home again.
 
Karibu home Mkuu hapa ganda linakaa tuu kabatini mpaka siku ya safari mambo ya bank ni kitambulisho cha NIDA nyumbani ni nyumbani...
 
Kwanini umeamua kurudi bongo mkuu? mie ningekuwa state hata kwa bunduki nisingerudi Afrika.
Mimi nilikua na mawazo kama yako ila baada ya kukaa kiwanja kwa muda mrefu nimeanza kumiss maisha ya Nyumbani.
Asikwambie mtu Nyumbani ni nyumbani hata kama ni kichakani.
 
Kigogo yeye atarudi lini nyumbani Kwani wanasema KUMENOGA!; Ingawa hakuna maji na umeme wa mgao!!!
 
Mimi nilikua na mawazo kama yako ila baada ya kukaa kiwanja kwa muda mrefu nimeanza kumiss maisha ya Nyumbani.
Asikwambie mtu Nyumbani ni nyumbani hata kama ni kichakani.
Na kubeba mabox ni kerooo sana
 
Back
Top Bottom