Ubaya au uzuri wa kiongozi hauzifanyi hoja zake nazo kuwa mbaya au nzuri

Kwanza pole kwa maumivu dhidi ya kipenzi Chako.

Hoja ya kulaumu chadema haina mashiko unawezaje kuwatambua wafuasi wa cdm mbona wengi walioonekana wakimshambulia na kumshinikiza Ndugai ajiuzulu ni wanaccm tena viongozi. Unataka chadema iingilie mambo ya ccm?

Ama kuhusu uzuri wa hoja kwamba hauhitaji uzuri wa mtu nayo hii unapotosha kwa sababu;

Wafuasi wa chadema wanakubali kuwa hoja ya Ndugai ina mashiko (rejea Lissu na mjadala clubhouse) ila tu hawawezi kukubali kusapoti mbeba hoja asiye na uhalali yaani ambaye aliyeshiriki kuasisi matendo maovu dhidi ya watetea hoja kama hiyo. Leo uhalali huo unaupata wapi?

Leo mnajifanya kutaka kuungwa mkono hata kama mtu ananuka damu za watu, ni lini wewe ulioonesha kuwaunga mkono cdm katika hoja nyingi za kitaifa kama katiba, thibitisha hapa au kwa kuwa maji yamewafika shingoni.

Ndugai asulubiwe kwanza na uovu wake Kisha hoja yake itabebwa na watu wenye uhalali na itapata sapoti na Wana cdm ila si huyo Ndugai wako.
 
Wengi kati ya wanaochangia hapa naona hata hawaelewi maana ya precedence, ushabiki wa vyama umewatawala sana vichwani mwao.

Baada ya Ndugai kujiuzulu kwa kosa la kutumia haki yake kisheria kutoa maoni yake akaishia kusutwa, huyo msutaji akiwamaliza huko atarudi upinzani kama alivyoanza na Mbowe.

Tena bahati nzuri wa chama chake anaishia kuwasuta tu halafu wengi humu mnashangilia, ila akimgeukia mpinzani anaetoa maoni yake kosa lake ni gerezani, sasa sijui kwa nini kwa Mbowe mlie ila kwa Ndugai mshangilie.

Hii athari ya kufungwa midomo sijui mtaiona lini, mnaishi kwa mazoea sana, badala ya kuwa na msimamo mmoja usioyumba kukemea hii tabia bila kujali sura ya anayefanyiwa, mnayumba yumba kama matawi ya miti matokeo yake advantage kwa dikteta.

Huku ndio kule kupiga hatua moja mbele halafu mbili kurudi nyuma kisha mnashangilia...

Leo mnashangilia Ndugai kufungwa mdomo, kesho tena akifungwa mdomo wa kwenu mtaanza tena kulia, hapo ndipo mtakapojibiwa mbona kwa Ndugai mlifurahia? mnabaki na kelele tu, sisi ni special zaidi ya Ndugai hatuna dhambi!.
 

Hoja gani ya Ndugai, yeye mwenyewe kaikana na kusema ni ya kutengenezwa huko mitandaoni, kibaya zaidi kaomba msamaha kwa hoja hiyo. We ni nani kuitetea? Kama kweli mna uchungu na hii nchi, hoja za kuokoteza za kina Ndugai ambao hawawezi hata kuzisimamia, tudai katiba mpya tena ile bora ya rasimu ya jaji Warioba. Hapo tutakuwa pamoja, sio kututaka kutetea hoja ya huyo muovu Ndugai, ambayo yeye binafsi anaikwepa.
 
naunga mkono hoja
p
 

Watu hawaelewi maana ya precidence neno au muktadha wa precidence? Hivi unadhani watu hawajui hii hoja ya Ndugai na tofauti ya kuisimamia? Wapinzani wanaweza kujitetea wenyewe bila kutaka kujishikamanisha na utetezi wa hoja ya Ndugai. Hiki kinachomliza au alichofanyiwa Ndugai sasa, ni kilio cha siku zote cha wapinzani, na huyo Ndugai alikuwa ni mzizi mkuu wa madhila ya wapinzani. Hakuna mwenye tatizo na hoja ya Ndugai, bali watu wanafurahi yanayomkuta Ndugai kama sehemu ya somo kwa wote wanaotenda uovu sasa.

Sasa ww unataka kujifanya mwerevu as if kuna anayemuunga mkono Samia na genge lake dhidi ya uonevu unaoendelea hapa nchini. Jambo la msingi ni madai ya katiba mpya na bora, na sio kutaka watu waunge mkono hoja za huyo muhuni, huku yeye mwenyewe akizikana. Hakuna uovu wowote watafanyiwa wapinzani utakuwa mpya, na kisha wapinzani wapige kelele waambiwe eti walifurahia ya Ndugai. Yeyote atakayesema hivyo ni haki yake, lakini hatuwezi kumtetea huyo muhuni aliyeshiriki kutesa wapinzani, eti kwa kutaka huruma ya hao wanaoshabikia madhila ya wapinzani kila siku. Uzuri sasa hivi hata hao waliokuwa wanafurahia madhila ya wapinzani, wanapitia hali hiyo.

Kama unadhani wewe ni mwerevu sana, mtetetee Ndugai na hilo genge lake, kisha wapinzani wakinyanyaswa ushangilie maana una hiyo precidence ya hii scenario ya Ndugai. Kiufupi hakuna mpinzani anayehitaji msaada wako wa utetezi, kwakuwa wewe unajifanya uko principaled kwenye hili tukio la Ndugai. Hatushirikiani na mtesi wetu yoyote hata angekuja na hoja gani, labda akadai katiba mpya tena kivyake.
 
Ume panic tu.

Umeandika kama vile unashindana kumbe hata hunielewi mantiki ya hoja yangu, ukiacha mihemko ndio utanielewa. Endelea na msimamo wako wa hoja ya Ndugai ipigwe teke kwasababu aliyeitoa ameomba msamaha, kama vile huo msamaha wake umeifuta hoja yake kwenye vichwa vya watanzania.

Lastly, usinipangie cha ku-support, najielewa navyocheza karata zangu, sina siasa za mihemko ya kitoto kama zako. Unajishtukia sijasema popote kuna yeyote anamuunga mkono Samia wacha kutetemeka dogo, ni upeo wako mdogo unaokufanya ujione umetumbukia kwenye huo mtego, and why not? aliwazalo mjinga...

Siku zote nitasimamia haki ya mtu anayeonewa bila kujali sura yake au itikadi yake, yeye kunitenda mimi ubaya sina sababu ya kulipa baya kwa baya, i'm not that fool; wewe endelea kutopea kwenye hilo tope la siasa za uvyama lililokufunika akili ukidhani kuna chama cha kifamilia.
 

Sina chochote cha kupanick maana hujaoongea chochote cha kutisha,labda kama unadhani umeongea kitu cha kutisha sana. Ulichoongea ni cha kawaida sana. Nasema hivi, tunajua alichoongea Ndugai na jinsi ya kusimamia bila kumpa yeye credit yoyote, maana yeye amekuwa kikwazo muda wote wa hoja za namna hiyo.

Sina chochote cha kukupangia usupport, bali ni pale unapopangia watu wasupport hoja ya Ndugai ili uonekane unasimamia misingi kwa namna utakayo ww. Huna mihemko kwa vigezo ulivyojiwekea ww, ana hilo neno mihemko unalitumia kama bendera fuata upepo, ili na ww uonekane unaweza kujilinda kwa kutumia neno hilo? Unasimamia haki ya mtu yoyote anayeonewa, wakati yeye mwenyewe kaomba msamaha kwa kuona amekosea? Toka umeanza kusimamia haki za wanaoonewa bila kujali vyama ama sura, ni nani kaacha kuonewa kwa hiyo misimamo yako?
 
Sijui unaandika vitu gani, halafu ukiambiwa una-panic unalia; hunielewi mantiki yangu wacha kulazimisha.

Mimi kukemea maovu nitaendelea tu bila kujali kama waovu bado wanayatenda, kwani hata nikikaa kimya hakutasaidia wao kuyaacha, mbona unauliza swali la kitoto sana? au kama kila siku tunalia wanaiba kura ndio tunyamaze? hii ndio solution yako!

Get on with your life dude, stop wasting my time.
 

Yaani we ni wa kuniliza mimi, ukiwa na jazba unanielewaje kwa mfano? Au unatamani unilize? Mantiki yako haieleweki, labda uipange upya.

Nasema hivi, hakuna anayesubiri msaada wako ili kujihisi anapata utetezi wowote. Watu wanaweza kujitetea bila kutaka kujionyesha wako neutral kama unavyotaka kujionyesha. Hapo mwisho, halafu inaonekana unajua kiingereza, tena kile cha London katikati!
 
Kama haki ya kuhoji maamuzi ya Rais hamuoni kama ina mashiko, kuna sababu gani ya kutaka Watanzania waunge mkono madai ya katiba mpya?

Hoja mbaya ni mbaya tu bila kujali imetolewa na nani. Vilevile, hoja nzuri ni nzuri bila kujali imetolewa na nani.

Sasa wewe hoja gani ameitoa spika aliyejiuzulu wakati unaona kabisa aliikana na kuomba msamaha kwamva watu wameungaunga vipande ndio ikatokea hayo mambo?

Ok, hata kama hausomi Biblia au unasoma ila kuna mstari unasema, mtawatambua kwa matendo yao, mti mwema kamwe hauwezi kuwa na matunda mabaya.

Au unakumbuka Baba wa taifa aliwahi kusema tunataka mtu ambaye akisema anaichukia rushwa, ukimuangalia usoni na anavyosema anaichukia rushwa, uione hiyo hali ya kuchukia rushwa, sio itoke mdomoni peke yake.

Spika hoja kumbe ilipelekwa kabisa kwenye kamati ya bajeti bungeni na ikapita, hakuhoji wala kupinga. Na kuna siku hadharani akapongeza jinsi huo mkopo ulivyonufaisha jimbo lake.

Huyohuyo mtu anakuja kusimama kukosoa huo mkopo hadharani, tena sio bungeni au kumwendea Mama amshauri, la hasha, hadharani mbele ya kadamnasi anashangaa huo mkopo, utamtilua maanani?

Haujakaa sawa wakati bado unatafakari kauli yake, unaona amejitokeza kuomba radhi na kuikataa kauli yake. Sasa hapo kuna kitu cha maana? Bora angesimamia kauli yake ingeonekana kweli tufanye kuna namna bungeni mhimili wake unakandamizwa kupitisha baadhi ya mambo na mhimili mwingine, sasa ile kuomba radhi na kukana kauli yake inamuingiza kwenye unafiki.
 
Aisee babaangu, hatutaki hoja ya Ndugai kama ile ya simba kudai uhuru wa nyumbu! ... IISEEE!
YAANI UHURU ADAI SIMBA NYUMBU TUSHANGILIE ILI UKIPATIKANA TULIWE!!!!?
SIWEZI KUWA BOGAS!
 

1. Kukataa au kukubali kuunga mkono hoja bila kujali hoja imetolewa na nani ni kielelezo cha ukomavu.
2. Kuunga mkono hoja kwasababu tu unampenda mtoa hoja ni kielelezo cha ushabiki.
3. Kukataa kuunga mkono hoja kwasababu tu humpendi mtoa hoja ni kielelezo cha chuki.
4. Kukataa kuunga mkono hoja kwasababu tu mtoa hoja amebadili gia angani ni kielelezo cha unyumbu. 2015 CHADEMA walipobadili gia angani kuhusu hoja ya vita dhidi ya ufisadi, nyumbu wote nao walikengeuka na kuwaacha wasiokuwa nyumbu wakiendelea kusimama na hiyo hoja mpaka kesho!
 
Chadema ni kama wameshakata tamaa ya kushika dola hivi sasa hata ile sifa ya kuwa chama kikuu cha upinzani ni kama hawana tena.
 
Kunya anye kuku akinywa Bata ?
nenda kamfute machozi
Hata hvyo waliomfanyia ubaya NI CCM wenzake sio chadema
Mbona haumsemi Samia kumpa makavu laivu ndugai?
UNAFIKI BWANAAA
 
Aliyesababisha ndugai kujinyonga mwenyewe NI chadema au Samia ?
Au kwa kuwa chadema ndo WABEBA LAWAMA WENU?
Mimi binafsi sipo chadema Wala chama chochote Ila NIMEFURAHI SANA NDUGAI KUONDOKA HAPO.
Ubaya ubaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…