Kwanza pole kwa maumivu dhidi ya kipenzi Chako.Watu wengi, especially wafuasi wa CHADEMA, wameonesha kupofushwa na chuki zao dhidi ya viongozi fulani kiasi cha kupoteza objectivity katika kupima nguvu ya hoja zinazotolewa na hao viongozi. That’s a very serious problem. Ni kukosa intellectual maturity!
Kimsingi, hatuhitaji kumpenda mtoa hoja. Kama hoja yake ni ya msingi, tunachounga mkono ni hoja iliyotolewa, sio mtoa hoja. Hakuna ubishani kwamba ubaya au uzuri wa mtoa hoja hauna maana kwamba hoja zake nazo ni mbaya au nzuri. Ukishaanza kumfikiria mtoa hoja, jua unahitaji break; you’re no longer objective. Ukiendelea on that path, utakuwa unafanya zoezi la kufurahisha nafsi yako. Conclusion utakayokuja nayo itakuwa completely useless.
Ndiyo maana Lissu, pamoja na uhasimu mkubwa ambao umekuwepo kati yake na Ndugai, ameshindwa kuja na automatic dismissal ya hoja ya Ndugai. Hii approach ni sahihi na ni moja ya maeneo machache ambayo mimi na Lissu tunasimama upande mmoja!
Hoja ya kulaumu chadema haina mashiko unawezaje kuwatambua wafuasi wa cdm mbona wengi walioonekana wakimshambulia na kumshinikiza Ndugai ajiuzulu ni wanaccm tena viongozi. Unataka chadema iingilie mambo ya ccm?
Ama kuhusu uzuri wa hoja kwamba hauhitaji uzuri wa mtu nayo hii unapotosha kwa sababu;
Wafuasi wa chadema wanakubali kuwa hoja ya Ndugai ina mashiko (rejea Lissu na mjadala clubhouse) ila tu hawawezi kukubali kusapoti mbeba hoja asiye na uhalali yaani ambaye aliyeshiriki kuasisi matendo maovu dhidi ya watetea hoja kama hiyo. Leo uhalali huo unaupata wapi?
Leo mnajifanya kutaka kuungwa mkono hata kama mtu ananuka damu za watu, ni lini wewe ulioonesha kuwaunga mkono cdm katika hoja nyingi za kitaifa kama katiba, thibitisha hapa au kwa kuwa maji yamewafika shingoni.
Ndugai asulubiwe kwanza na uovu wake Kisha hoja yake itabebwa na watu wenye uhalali na itapata sapoti na Wana cdm ila si huyo Ndugai wako.