Uber yasitisha huduma zake Tanzania, yazitaja nauli elekezi Latra kama sababu. Itarejea kanuni zikibadilishwa

Uber yasitisha huduma zake Tanzania, yazitaja nauli elekezi Latra kama sababu. Itarejea kanuni zikibadilishwa

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
Wakuu,

Usiku huu Uber wametuma ujumbe unaosomeka hivi:
👇🏾

Huduma ambayo ilianza kama wazo tu — la kutumia simu yako kupata usafiri ndani ya dakika chache— Mfumo wa Uber umeenea duniani kote na zaidi ya safari milioni 15 hufanyika kila siku kupitia kwenye mfumo huu. Imekuwa ni heshima kubwa kupata nafasi ya kusaidia watu kupata usafiri duniani wanapofanya shughuli zao na kutangamana na watu wengine.

Lakini, maandalizi ni sehemu muhimu katika kufikia malengo ya siku za usoni.
Siku zote, lengo letu ni kuwa mshirika muhimu katika miji mbalimbali kwa kutoa usafiri wenye ufanisi, kutengeneza fursa za kiuchumi zinazowapa madereva uhuru wa kujiingizia kipato kwa muda wanaotaka wao na kuchangia katika mapato ya serikali. Na tumelisimamia lengo hili tangu tulipofungua milango yetu katika jiji la Dar es Salaam mwaka 2016.

Sera za usimamizi zinapaswa kuwa chachu wala sio kikwazo cha ubunifu

Tumefanya uamuzi mgumu wa kusitisha huduma zetu nchini Tanzania kuanzia Alhamisi ya Tarehe 14 Aprili 2022. Nauli elekezi iliyowekwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesababisha changamoto kubwa kwa mifumo kama Uber kuendelea kutoa huduma kwa wateja wetu. Inakua ngumu kwetu kuendelea kutoa huduma. Hatuta weza kutoa huduma mpaka pale mazingira yatakapo kua rafiki kwa sisi kuendelea kutoa huduma.

Kipaumbele Chetu: kuwasaidia Madereva Watanzania
Uamuzi huu umekuja baada ya mamlaka kuweka kanuni ambazo ni changamoto kubwa kwa mifumo kama Uber kuendesha biashara yake. Tutafanya kazi kwa karibu na madereva kwenye mpito huu.

Tuweke Wazi: Tungependa sana kuendelea kutoa huduma zetu nchini Tanzania

Nchi ya Tanzania kupitia Dira ya Maendeleo ya 2025 imedhamiria kujenga uchumi imara, anuwai, himilivu na shindani ambao unaendana na mabadiliko ya masoko na kiteknolojia kikanda na kimataifa. Tulitegemea kwamba hii ingejumuisha kujenga mazingira wezeshi ili biashara ya ndani na kimataifa inawiri katika njia nzuri na yenye usawa, lakini kwa bahati mbaya, hali ni kinyume na matarajio.

Tutarudi kuzindua huduma zetu mara tu kutakapokuwa na kanuni mpya.

Ingawa tumefunga huduma za UberX, UberXL na UberX Saver nchini Tanzania, tuko tayari kushirikiana na mamlaka husika katika kuunda kanuni ambazo zitawezesha teknolojia kunawiri, ili tuanze tena kutoa huduma zetu zinazopendwa na watu wengu.

Asante, Tanzania!
 
Huu ni ujunbe ambao wateja wametumiwa mapema leo ...

IMG_20220414_025245.jpg
IMG_20220414_025303.jpg
IMG_20220414_025317.jpg


Sent from my Redmi Note 9S using JamiiForums mobile app
 
1. Mwomba huduma sie anaepanda kwa chombo cha kusafiria, bali anamwombea rafiki/nduguu usafiri na kulipia.

2. Madereva waliojiunga na Uber ili kutoa huduma kwa wateja kukosa uaminifu/uadilifu etc.

3. Mazingira ya biashara kila uchao taratibu zabadilika za uendeshaji biashara kwa Tanzania.

4. Gharama na mifumo ya barabara kwa tz
 
Tanzania bado kuna sera mbovu na rudia tena tanzania bado kuna sera mbovu.

Hiki chama cha ccm stage ilipofikia ni kuuza nchi.

viongozi wameshindwa kukabiliana na maisha ya nchi kwenye mitikisiko ambayo wamegeuza upigaji kwao na mitaji ya kisiasa huko mbeleni.

Kama wanashindwa kutatua vitu ambavyo visije kuleta hasi huko mbeleni kwenye vitu vingi.

huu ni mfano tosha leo uber,kesho nani !
 
Back
Top Bottom