Uber yasitisha huduma zake Tanzania, yazitaja nauli elekezi Latra kama sababu. Itarejea kanuni zikibadilishwa

Uber yasitisha huduma zake Tanzania, yazitaja nauli elekezi Latra kama sababu. Itarejea kanuni zikibadilishwa

Huu ni mwanzo tu,daladala na mabasi yatafuata

LATRA waache soko lenyewe liamue bei ya nauli,mbona watawala wanajipangia tu tozo kwenye mafuta na hatuoni hao CCC wakiongea.

Mbona hakuna bei elekezi kwenye usafirishaji wa mizigo na maisha yanaenda.
 
1. Mwomba huduma sie anaepanda kwa chombo cha kusafiria, bali anamwombea rafiki/nduguu usafiri na kulipia
2. Madereva waliojiunga na Uber ili kutoa huduma kwa wateja kukosa uaminifu/uadilifu etc
3. Mazingira ya biashara kila uchao taratibu zabadilika za uendeshaji biashara kwa tz
4. Gharama na mifumo ya barabara kwa tz

Hizi sio sababu mkuu..
 
Kawaida hawa mpinzani akiwazidi wanarusha taulo
 
Wakuu,

Usiku huu Uber wametuma ujumbe unaosomeka hivi:
👇🏾

Huduma ambayo ilianza kama wazo tu — la kutumia simu yako kupata usafiri ndani ya dakika chache— Mfumo wa Uber umeenea duniani kote na zaidi ya safari milioni 15 hufanyika kila siku kupitia kwenye mfumo huu. Imekuwa ni heshima kubwa kupata nafasi ya kusaidia watu kupata usafiri duniani wanapofanya shughuli zao na kutangamana na watu wengine.

Lakini, maandalizi ni sehemu muhimu katika kufikia malengo ya siku za usoni.
Siku zote, lengo letu ni kuwa mshirika muhimu katika miji mbalimbali kwa kutoa usafiri wenye ufanisi, kutengeneza fursa za kiuchumi zinazowapa madereva uhuru wa kujiingizia kipato kwa muda wanaotaka wao na kuchangia katika mapato ya serikali. Na tumelisimamia lengo hili tangu tulipofungua milango yetu katika jiji la Dar es Salaam mwaka 2016.

Sera za usimamizi zinapaswa kuwa chachu wala sio kikwazo cha ubunifu

Tumefanya uamuzi mgumu wa kusitisha huduma zetu nchini Tanzania kuanzia Alhamisi ya Tarehe 14 Aprili 2022. Nauli elekezi iliyowekwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesababisha changamoto kubwa kwa mifumo kama Uber kuendelea kutoa huduma kwa wateja wetu. Inakua ngumu kwetu kuendelea kutoa huduma. Hatuta weza kutoa huduma mpaka pale mazingira yatakapo kua rafiki kwa sisi kuendelea kutoa huduma.

Kipaumbele Chetu: kuwasaidia Madereva Watanzania
Uamuzi huu umekuja baada ya mamlaka kuweka kanuni ambazo ni changamoto kubwa kwa mifumo kama Uber kuendesha biashara yake. Tutafanya kazi kwa karibu na madereva kwenye mpito huu.

Tuweke Wazi: Tungependa sana kuendelea kutoa huduma zetu nchini Tanzania

Nchi ya Tanzania kupitia Dira ya Maendeleo ya 2025 imedhamiria kujenga uchumi imara, anuwai, himilivu na shindani ambao unaendana na mabadiliko ya masoko na kiteknolojia kikanda na kimataifa. Tulitegemea kwamba hii ingejumuisha kujenga mazingira wezeshi ili biashara ya ndani na kimataifa inawiri katika njia nzuri na yenye usawa, lakini kwa bahati mbaya, hali ni kinyume na matarajio.

Tutarudi kuzindua huduma zetu mara tu kutakapokuwa na kanuni mpya.

Ingawa tumefunga huduma za UberX, UberXL na UberX Saver nchini Tanzania, tuko tayari kushirikiana na mamlaka husika katika kuunda kanuni ambazo zitawezesha teknolojia kunawiri, ili tuanze tena kutoa huduma zetu zinazopendwa na watu wengu.

Asante, Tanzania!
Ni vigumu sana kwa nchi yetu kuendelea kwa mfumo hovyo wa ccm uliopo madarakani, yubsdilishe.
 
Madereva taksi zenye mstari walilaani mno ujio wa Uber.
 
Kwa hiyo sasa hivi kutoka Airport kwenda Kinondoni tutegemee zile nauli za 70,000/- Tsh kurudi?
Maana kama Uber karusha taulo kwa madai mazingira ya biashara si rafiki basi kuna uwezekano wenzake kina Bolt, Taxify and co kufuata nyayo.
 
Sasa mama atawaweza wabongo.
Wabongo wanataka Magu.

Ili la mtu kumuitia uber mtu mwingine muitaji si mpandaji, madereva sio aliyesajiliwa na chombo yaani kampa deiwaka.

Madereva Wana namna yao ya kucheza unapewa bei tofauti na uliyoomba ukosefu wa uaminifu.
Naomba kuuliza, hivi nikirequest uber akaitumia mtu mwingine shida inakua ni nini hapo? mie ilikua ndio zangu hizo.
 
Tutulie tu...

Hapo ishaundwa kampuni mpya...zitakuja Uber Ila kivingine...

Tumefunguliwa pingu Ila tutafungwa minyororo ..na huu ubole wetu!
 
Tutakoma na nauli za Tax za kawaida hasa kwa sisi wageni wa miji husika na tunahitaji usafiri private!
 
Back
Top Bottom