Uber yasitisha huduma zake Tanzania, yazitaja nauli elekezi Latra kama sababu. Itarejea kanuni zikibadilishwa

Tumechukua uamuzi mgumu wa kusitisha kwa muda huduma za UberX, UberXL na UberX Saver nchini Tanzania, bidhaa hizi hazitapatikana kuanzia Alhamis ya tarehe 14 Aprili 2022. Kanuni za sasa za usimamizi wa sekta hii zimejenga mazingira ambayo si rafiki na zimekuwa changamoto kubwa katika uendeshaji wa biashara yetu, hadi pale muafaka utakapopatikana, hatutaendelea kutoa huduma za usafiri wa UberX, UberX Saver na UberXL nchini Tanzania.

Tunapenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa dhati - kwa kuchagua mfumo wetu kufanya safari zako jijini Dar es Salaam ambako tumekuwa tukitoa huduma zetu kwa kipindi cha miaka sita iliyopita.

Huu ni wakati mgumu kwetu sote, lakini hii haina maanai kwamba ndio mwisho wa kila kitu. Tuko tayari kushirikiana na mamlaka husika na kuwa na mazungumzo yatakayoleta tija na kujenga mazingira wezeshi na tutarudi na kuendelea na kukupa usafiri wa kutegemewa na wa uhakika ambao umekuwa ukiitumia, baada ya kujiridhisha kwamba mazingira ya kibiashara ni rafiki.

Tunafahamu kwamba hiki ni kipindi kigumu na usumbufu unaotokana na uamuzi huu na tunapenda kukuhimiza uwasiliane nasi kupitia kwenye app ikiwa una maswali yoyote.

Asante Sana, Tanzania!

Timu ya Uber
 
Vijana watakufa njaaa na viduku vyao
 
Hii imekuwa habari mbaya sana kwangu
 
Ni fitna tu za wabongo,
Wao hawawezi na wanaoweza wasifanye,
Tuna safari ndefu kweli
 
Naona kiwanda cha kipanya kitazaliza Uber zake sasa [emoji23][emoji23]
Watu na bahati zao jamani Yaani kiwanda kipya tu atawapita Toyota kama wamesimama
 
Noma sana ! Anaupiga mwingi sana .
 
Tutatumia Bolt
Kwa kifupi Uber walikuwa wanatafuta pa kufia, kibiashara wao walikuwa wameshatetereka baada mshindani wao kuwazidi.
Uber wako juu sana kwenye cost, mfano unarequest Uber kwa trip ya Posta-Mwenge unaambiwa 23,000 wakati Bolt ukiitisha same trip unaambiwa 10,000 kwa gari ndogo sedan kwa mawazo ya kawaida mteja aki request mara 2 au 3 na kuona hiyo tofauti ana haja gani tena ya kurequst tena hiyo Uber? Kwa kifupi wamejimaliza wenyewe!!!
 
Naona kiwanda cha kipanya kitazaliza Uber zake sasa [emoji23][emoji23]
Watu na bahati zao jamani Yaani kiwanda kipya tu atawapita Toyota kama wamesimama

Nachelea kusema hata hujui Uber ni nini….
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…