Huenda una hoja ila umeshindwa kuiwasilisha, kimsingi uamuzi huu wa cdm wamechemka. Sitarajii cdm wafanye kosa la kijinga hivi, cdm walisusia uchaguzi vwa serikali za mitaa, mbona tuliwaunga mkono? Tunajua fika Magufuli sio mtu wa maridhiano, iweje cdm wasilijue hilo?
Unataka watu waende mahakamani kusikiliza kesi za viongozi wa cdm, je cdm hao hao sio ndio walitii siasa za kikondoo toka kwa Lowassa hatimaye wakaahirisha ukuta? Sasa wamepandikiza siasa za woga wenyewe kwa kufundishwa siasa za woga wakitarajia nini kwa sasa? Isitoshe hao viongozi wa cdm wanapokuwa wanakula hela na kupakia maVX watu huwa wanawafuata kula nao? Hao viongozi walivyompokea Lowassa na kula hela yake waliwagaia hao waliokuwa wanawasupport?
Cdm bado inapata support ya watu toka mitandaoni, huko mtaani hamasa hutokea humu humu mitandaoni. Mfano mrahisi wa cdm kushindwa kusoma upepo ni juu ya uchaguzi serikali za mitaa, watu waligoma kujiandikisha kutokana na uhuni wa wazi na mazingira yakiwa hayajabadilika, na hamasa ilitoka huku huku mitandaoni, lakini Mbowe na Mdee walihamasisha watu na bado watu hawakujitokeza. Wadanganye cdm waache kusikiliza sauti za watu wao, kisha useme wategemee huko mitaani bila nguvu yetu sisi watu wa mitandaoni.