Ubinafsi wa Mayele unavyoighalimu Yanga

Ubinafsi wa Mayele unavyoighalimu Yanga

Yanga mna matatizo......
Ni lini mliwahi kuwa bora dgidi ya Simba?
Mara zote mmekuwa mkiponea tundu la sindano.
Twende na takwimu.
 

Attachments

  • Screenshot_2023-04-16-21-09-19-67.png
    Screenshot_2023-04-16-21-09-19-67.png
    174.8 KB · Views: 1
Kule mbele anaecheza kitimu ni yule Kenedy Juma sorry nani vile Musonda
Jamaa huwa hana tamaa, anatoa mapande tu ya upendo. Mayele yeye anachowaza ni kujipigia tu golini. Hata kama yupo mbali na goli.
 
Inashangaza kocha alimwacha hadi dk za mwisho
Labda aliogopa asionekane kama Robertinho alivomtoa Chama akazomewa na watu wa Simba. Mimi kwa mtazamo wangu, inaonekana Inonga ameshamsoma Mayele na anammudu. Jana Gemu ilimkataa na labda Aziz Ki, mudathir na Morrison waliingizwa wakati jua limeshachwea na jahazi limeanza kuzama. Labda angewaingiza mapema matokeo yangekuwa tofauti.
 
Mayele ni mchezaji mzuri hasa kwa jitihada zake za kujituma awapo uwanjani. Ila kwa mtazamo wangu licha ya mazuri yake kwa upande mwingine amekuwa akiighalimu sana timu kutokana na uchoyo uliopitiliza. Mechi ya leo na Simba amepiga mashuti mengi akiwa katikati ya uwanja badala ya kuwapa wenzake waliokuwa wamefungua.

Njoo kwenye mechi zile mbili na Al Hilal (home & away) ubinafsi wake ulichangia Yanga kufunga magoli machache hapa nyumbani na kupelekea kutolewa. Amekuwa akilazimisha kufanya vitu vingi peke ake akisahau kuwa mpira ni mchezo wa timu.

Anacheza kutafta "Personal glory" kuliko "Team success". Mara kadhaa nimekua nikimuona kocha akimkumbusha lakini habadiliki.

Mechi ya Dabi km ya leo ni mechi inayochezwa kimkakati sana. Ukicheza kibinafsi vile unawaraisishia wapinzani kukukaba na ndivyo Simba walivyofanikiwa. Kutokana na sifa anazosifiwa Mayele amekuwa akicheza kifadha sana.

Anapoteza mipira mingi na kwa uzembe kabisa! Siamini kama Nabi ameshindwa kumbadilisha na kama ni hivo basi uongozi uingilie kati kwa manufaa ya timu.

Namkumbusha Mayele, mashabiki wa Simba na Yanga huwa hawana mapenzi ya kudumu. Asione watu wapo kimya siku wakilipuka asishangae akianza kuzomewa, kama haamini amuulize Boko. Licha ya timu nzima kutocheza vizuri leo ila Mayele kazingua sana.

Hongereni Simba though, na poleni Utopolo.
Kabisaa upo sahihi sana!MAKOLO jana wangekufa mapema tu kama mayele angeacha ubinafsi
 
Back
Top Bottom