Ubinafsi wetu wanawake ndio chanzo cha wanaume kutuumiza

Wanawake karibu wote ndiyo wako hivyo. Na ndiyo maana mwanaume akioa mke asiye na kazi husikii kelele ila wako mwanaume ufukuzwe kazi halafu mkeo awe na kazi au pesa

utapata tabu sana

mshauri huyo jamaa apambane na maisha yake na ajifunze
 
Kwenye mahusiano yao kuna kitu hakipo sawa

Ukiacha swala la roho mbaya kwa wanawake

Hakuna roho mbaya ya kiasi hicho kwa watu wanaopendana
Upendo una nguvu sana

Hakika nawaambia kama mahusiano yao yangekuwa yako sawa huyo jamaa angejivunia kuwekeza kwa mpenzi wake

Mpenzi wako aliyekusaidia ufike hapo ulipo tena kiuchumi leo kapata changamoto unasema apambane na hali yake??

Mbona jamaa hana ujasiri wa kwenda kwa mpenzi wake ambaye anajua hapo alipofika ni kwa sababu yake? Had analala na njaa?

Kuna kitu bado hujakijua kipo nyuma ya panzia, chunguza.
 
Nina shost yangu ni mfanyabiashara mzuri tu wa nafaka na anaingiza faida nzuri kwa sasa.
Ana mtu wake ambaye alisimama bega kwa bega kuhakikisha anafika hapo alipo. Huyo mtu wake kipindi hicho aliamua kuwekeza akili, mawazo na hela kwaajili ya kuhakikisha mpenzi wake anasimama kibiashara. Kweli bi shost wangu alifanikiwa kufikia malengo kwa msaada wa huyo shem.

Bahati mbaya mwaka jana mtu wake akasimamishwa kazi ghafla. Mpaka hivi sasa hajafanikiwa kupata kazi sehemu nyingine. Kama mmavyofahamu hapa dar maisha yalivyo magumu...mkaka wa watu anaishi kwa kuunga unga. Kinachonishangaza ni kuwa huyu mtu wake ambaye ni shost yangu, haonyeshi ushirikiano kwenye matatizo aliyonayo mtu wake. Kwa bahati mbaya, anamsema vibaya akiwa na sisi mashost zake.

Kwa story zake anadai mtu wake inafikia hatua anaweza kushinda siku mbili hajala kwa kukosa hela ya chakula. Na anachosema huyu best yangu ni kuwa huyo mtu wake wala hajawahi kumuomba msaada wowote. Mimi namuambia akuombe msaada kivipi wakati hali yake unaijua na unaweza ukamsitili? Anachojibu ndicho kilichonifanya nije nianzishe thread hapa. Anasema apambane na hali yake.

Huu ubinafsi tulionao utatufanya tuendelee kuona wanaume hawafai japo na mimi nimetendwa na mwanaume kiasi cha kunifanya niogope kuingia kwenye mahusiano mengine.

Ushauri wangu kwa wanawake wenzangu. Wanaume ni bidhaa adimu ambayo kipata na kuishikilia ikawa yako, ni bahati sana. Ndio maana mimi wa kwangu nilitaka nianze naye chini, lakini alinigeuka. Sijui alifikwa na nini, mpaka leo sipati jibu
Nakupenda
344671.jpg

❤❤❤
 
Wanawake ni wabinafsi sana, dawa ya mwanamke ni kuishi nae na kumuacha kama ulivyo mkuta. Usimfungulie biashara wala kumuendeleza muache kama alivyo. Unapo muimarisha mwanamke anakuona wewe ni mjinga hasa ukiyumba au kupata changamoto yotote
 
Ushauri wangu kwa wanawake wenzangu. Wanaume ni bidhaa adimu ambayo kipata na kuishikilia ikawa yako, ni bahati sana. Ndio maana mimi wa kwangu nilitaka nianze naye chini, lakini alinigeuka. Sijui alifikwa na nini, mpaka leo sipati jibu
Sometimes kuna mahala hua mnakosea bt hua n wabishi kukubali mnakosea mkiamn mpo right ila Ur man ndo hayupo right ....wasopenda kubishana hujiengua kimya kimya..
 
Mwanaume unaweza kuihudumia familia mda wote ,kama hamna kitu ndani mwanamke anaagiza tu ,hata awe na hela utakuta hata chumvi hanunui. Ikitokea huna hela haelewi zaidi atafanya mambo yake binafsi.
 
Nina shost yangu ni mfanyabiashara mzuri tu wa nafaka na anaingiza faida nzuri kwa sasa.
Ana mtu wake ambaye alisimama bega kwa bega kuhakikisha anafika hapo alipo. Huyo mtu wake kipindi hicho aliamua kuwekeza akili, mawazo na hela kwaajili ya kuhakikisha mpenzi wake anasimama kibiashara. Kweli bi shost wangu alifanikiwa kufikia malengo kwa msaada wa huyo shem.

Bahati mbaya mwaka jana mtu wake akasimamishwa kazi ghafla. Mpaka hivi sasa hajafanikiwa kupata kazi sehemu nyingine. Kama mmavyofahamu hapa dar maisha yalivyo magumu...mkaka wa watu anaishi kwa kuunga unga. Kinachonishangaza ni kuwa huyu mtu wake ambaye ni shost yangu, haonyeshi ushirikiano kwenye matatizo aliyonayo mtu wake. Kwa bahati mbaya, anamsema vibaya akiwa na sisi mashost zake.

Kwa story zake anadai mtu wake inafikia hatua anaweza kushinda siku mbili hajala kwa kukosa hela ya chakula. Na anachosema huyu best yangu ni kuwa huyo mtu wake wala hajawahi kumuomba msaada wowote. Mimi namuambia akuombe msaada kivipi wakati hali yake unaijua na unaweza ukamsitili? Anachojibu ndicho kilichonifanya nije nianzishe thread hapa. Anasema apambane na hali yake.

Huu ubinafsi tulionao utatufanya tuendelee kuona wanaume hawafai japo na mimi nimetendwa na mwanaume kiasi cha kunifanya niogope kuingia kwenye mahusiano mengine.

Ushauri wangu kwa wanawake wenzangu. Wanaume ni bidhaa adimu ambayo kipata na kuishikilia ikawa yako, ni bahati sana. Ndio maana mimi wa kwangu nilitaka nianze naye chini, lakini alinigeuka. Sijui alifikwa na nini, mpaka leo sipati jibu
Duuuh....

Kweli maisha yanataka ukweli na UHALISIA wa 2+2=4.....

Ukijifanya kukumbatia HISIA tu basi binafsi utayashuhudia ya huyo SHEMEJI YAKO.....

Wanaume hatuwajui vyema wanawake mpaka yatufike kama hayo......🤣
 
Mwanaume unaweza kuihudumia familia mda wote ,kama hamna kitu ndani mwanamke anaagiza tu ,hata awe na hela utakuta hata chumvi hanunui. Ikitokea huna hela haelewi zaidi atafanya mambo yake binafsi.
🤣
 
Hivi haiwezekani wanaume wote tukagoma kuoa kisiri siri ili tunyoshe hivi viumbe yaani unamuweka kwenye reli unapita ila kuzaa lazima

Sent from my TECNO KD7h using JamiiForums mobile app
 
Huyo dada hakumpenda jamaa,ila mwanamke akikupenda NYIEEEE
Back to me mama watoto hana kazi ni mama wa nyumbani,ila can u imagine huwa anabana hela ninayomuachia then ananichukulia zawadi kali sana,,halafu ukichek hela ninayomuachia ni kuduchuu mno
Anahongwa ili kutop up matumizi ys familia.
 
Back
Top Bottom