Ubinafsishaji: Mkapa alikosea?

Ubinafsishaji: Mkapa alikosea?

wandugu,

..mashirika ya umma yaliuawa na wa-Tanzania wenyewe. matokeo yake yakawa ni mzigo kwa walipa kodi wa Tanzania.

..ubinafsishaji mimi nauchukulia kama TACTICAL RETREAT. kwamba ni hatua ya kurekebisha makosa na kujipanga upya.

..baada ya kuondokana na mzigo wa kutoa ruzuku kwa mashirika ya umma, na kuongeza bidii ktk kukusanya kodi, serikali sasa imeweza kutoa mchango mkubwa zaidi ktk miradi ya maendeleo kwa mfano ujenzi wa barabara.

..kwa upande mwingine sera ya ubinafsishaji siyo "maandiko matakatifu" yanayokataza serikali kuanzisha makampuni ya umma kama itaamua.

..naamini leo hii wa-Tanzania tuna nafasi nzuri zaidi ya kuanzisha makampuni ya umma, na kuyasimamia yasilitie taifa hasara na kuwa mzigo kwa wananchi.
 
Binafsi nafikiri hii statement imekuja too late. Kwa kawaida viongozi wanapoondoka madarakani kwenye exit interviews zao na wanahabari au katika kuaga wananchi wao, huwa wana assess mafanikio yao na mapungufu yao. Lakini katika kujenga legacy zao huwa wanataja mafanikio zaidi kuliko mapungufu. Kwa kesi ya Mkapa, angeweza kuwaita journalists aliowahi kuwakandia na kuwaachia mwamuulize maswali. Hakuwa na hiyo courage. Yeye alikuwa yuko radhi kufanya interview na Riz Khan aliyekuwa CNN kuliko hawa local reporters wetu ambao pia nakiri wengi wao wanahitaji "msasa". Lakini that should have been a start.

Pia alikuwa na venues nyingine. Kuna hotuba ya Rais, angeweza kusema naondoka na nina furaha kukabidhi utawala wa nchi kwa successor wangu kutoka kwenye chama changu, na mambo niliyoyafanya yanayonifanya nitoke kifua mbele ni x,y, na z. Na yale ambayo natamani ningeweza kuyafanya kwa ufanisi zaidi ni a,b, na c. Still he couldn't do that.

Vile vile angeweza kutumia Sherehe za kiserikali kama za Muungano, Mei Mosi, na Uhuru kufikisha ujumbe...lakini aliona watanzania hawajui chochote na hawana haki ya ku muuliza maswali so pale criticism ilipoanza yeye akajificha na kukimbia nje ya nchi kwa excuses za kuwa mediator wa mgogoro wa Kenya na other international affairs. Lakini baada ya wananchi kuanza kupiga debe sana na hayo madebe kuwa echoed na actions za associates wake kufikishwa mahakamani, then he sees the need to speak about the weakness of his administration. Nafikiri ni too little, too late.
 
wandugu,

..mashirika ya umma yaliuawa na wa-Tanzania wenyewe. matokeo yake yakawa ni mzigo kwa walipa kodi wa Tanzania.

..ubinafsishaji mimi nauchukulia kama TACTICAL RETREAT. kwamba ni hatua ya kurekebisha makosa na kujipanga upya.

..baada ya kuondokana na mzigo wa kutoa ruzuku kwa mashirika ya umma, na kuongeza bidii ktk kukusanya kodi, serikali sasa imeweza kutoa mchango mkubwa zaidi ktk miradi ya maendeleo kwa mfano ujenzi wa barabara.

..kwa upande mwingine sera ya ubinafsishaji siyo "maandiko matakatifu" yanayokataza serikali kuanzisha makampuni ya umma kama itaamua.

..naamini leo hii wa-Tanzania tuna nafasi nzuri zaidi ya kuanzisha makampuni ya umma, na kuyasimamia yasilitie taifa hasara na kuwa mzigo kwa wananchi.
Swali kwako mkuu wangu, katika hii trial and error taifa la Tanzania limeingia hasara kiasi gani? Je tukifanya cost benefit analysis ya huu uwekezaji..tukachukua mashirika yote makubwa, je tuko better off leo hii, au ni bora tungeendelea kuyafadhili kwa fedha za Serikali na hivyo kuendelea kulibebesha taifa mzigo mzito wakati tukijifunza kutoka kwa wenzetu Benchmark (nchi zilizofanya ubinafsishaji successfully) na kufanya feasibility studies ya namna ya kuingia kwenye zoezi la ubinafsishaji?

Nafikiri Administration iliyajua haya na these people did not do their homework. Hawakuwa na plan ambayo ilikuwa ni yenye manufaa kwa umma wa waTanzania. Plan yao ilikuwa ni ya wao (wachache) ku get wealthy quickly na kuachia regimes nyingine zije zi clean messy walizoziacha.
 
FMES,

Mkuu, wapo watu hutubu madhambi yao wakiwa mahututi kitandani (kina Nyerere) na wengine hutubu madhambi yao wakiwa kanisani (Mkapa)..wote wametubu mkuu wangu pamoja na kwamba makosa na madhambi yao hayalingani..hivyo tutawahukumu kulingana na makosa yao wengine watasameheka na wengine watakiona cha moto..

Mkuu hapo juu nimeandika kwamba Nyerere hawezi kujutia Ujamaa kwa sababu objectives zake ni ktk kujenga society yetu (restoration of Africa's humanist and egalitarian principles of our society) kuondokana na adui wetu watatu.. UJINGA, UMASKINI na MARADHI based upon human dignity, respect and social justice kulingana na mazingira yetu..

Mkuu ktk hotuba yake mwaka 1984 kabla ya kung'atuka, Nyerere mwenyewe ndiye aliye abolish strategic political functions ambazo zilikuwa primarily distributive badala ya kuwa productive..forceful applied badala ya re-asserts itself in a modern technical world - market economy..

Lakini pamoja na kukubali kufungua milango alituonya kuwa uchumi wa haki ni lazima uendane na social development, na hatuwezi kufikia hayo ikiwa hakuna real socialisation of productive and distributive processes..Kwa hiyo Ujamaa bado upo pale pale..makosa yake sio malengo ya Ujamaa isipokuwa zile means to achieve the same ends!

Ukitaka nakala zake nadhani watembelee HAKI ELIMU, hawa wana hotuba nyingi sana za mwalimu..
 
- Mkuu Bob, nimekusikia sana nilichouliza ni kwamba unasema kuna mahali Mwalimu alikubali hadharani mbele yetu wananchi kuwa Ujamaa wake ulishindwa? Alisema exactly that au?
 
Jokakuu,
Ubinafsishaji wa Mkapa ni sawa na yule Model - Miss Brazil aliyekatwa miguu na mikono kujaribu kumponya lakini matokeo yake amekufa..
Leo hii wataalam wa maradhi yake wanasema hapakuwepo na haja ya kukatwa miguu wala mikono, maradhi yake yaliwezekana kabisa kutibiwa bila kumwondoa viungo!..
 
Capital Hill said:
Swali kwako mkuu wangu, katika hii trial and error taifa la Tanzania limeingia hasara kiasi gani? Je tukifanya cost benefit analysis ya huu uwekezaji..tukachukua mashirika yote makubwa, je tuko better off leo hii, au ni bora tungeendelea kuyafadhili kwa fedha za Serikali na hivyo kuendelea kulibebesha taifa mzigo mzito wakati tukijifunza kutoka kwa wenzetu Benchmark (nchi zilizofanya ubinafsishaji successfully) na kufanya feasibility studies ya namna ya kuingia kwenye zoezi la ubinafsishaji?
Nafikiri Administration iliyajua haya na these people did not do their homework. Hawakuwa na plan ambayo ilikuwa ni yenye manufaa kwa umma wa waTanzania. Plan yao ilikuwa ni ya wao (wachache) ku get wealthy quickly na kuachia regimes nyingine zije zi clean messy walizoziacha.

Capitol Hill,

..kwanini tuangalie cost-benefit analysis ya yaliyopita, badala ya ku-focus on the future?

..tatizo lingine wananchi mnafanya cost-benefit analysis ya matatizo ya zamani ktk mazingira ya leo hii.

..ninavyoelewa mimi tulikuwa na hali mbaya sana kiuchumi na kifedha na ndiyo maana tukalazimika kuyabinafsisha mashirika ya umma.

..serikali imefanya iliyofanya, na tumefika mahali taifa lina uwezo wa kuchangia kifedha ktk miradi mbalimbali ya maendeleo.

..kwa msingi wa hoja hiyo hapo juu ina maana tunaweza ku-invest tena kwenye makampuni ya umma kama kuna ulazima huo.

..hakuna haja ya kuendelea kulalamika. kinachopaswa kufanyika ni kuchukua hatua za kurekebisha mapungufu na matatizo yaliyotokana na ubinafsishaji.

NB:

..hakuna hatua yoyote ile ya uchumi ambayo itafanikiwa by 100%. kwa msingi huo kazi ya kurekebisha pale tulipokosea, na kuboresha zaidi pale tulipopatia, inapaswa kuendelea as long as we exist as a nation.
 
Mkandara said:
Jokakuu,
Ubinafsishaji wa Mkapa ni sawa na yule Model - Miss Brazil aliyekatwa miguu na mikono kujaribu kumponya lakini matokeo yake amekufa..
Leo hii wataalam wa maradhi yake wanasema hapakuwepo na haja ya kukatwa miguu wala mikono, maradhi yake yaliwezekana kabisa kutibiwa bila kumwondoa viungo!..

Mkandara,

..haitoshi kumlaumu Mkapa tu bila kuchukua hatua za kurekebisha makosa aliyoyafanya.

..tunafahamu kwamba mikataba yetu ya madini ina matatizo makubwa. kitu cha ajabu hatuiirekebishi tumeishia kumlaumu Mkapa tu.

..tuendelee kumzomea Mkapa na mafisadi, lakini pia tutumie the same efforts and energy kuipigia mayowe na kuishinikiza serikali iliyoko madarakani irekebishe mikataba ya madini.

NB:

..hivi unafahamu kwamba Kikwete alimtimua kazi CEO[mtu wa mkapa] wa PSRC[taasisi ya ubinafsishaji] na kuweka mtu wake, ambaye ameendeleza madudu[ubinafsishaji wa TRC] yaleyale kama ya mtangulizi wake???
 
Jokakuu,
Ubinafsishaji wa Mkapa ni sawa na yule Model - Miss Brazil aliyekatwa miguu na mikono kujaribu kumponya lakini matokeo yake amekufa..
Leo hii wataalam wa maradhi yake wanasema hapakuwepo na haja ya kukatwa miguu wala mikono, maradhi yake yaliwezekana kabisa kutibiwa bila kumwondoa viungo!..

Ni kweli kabisa. Kurekebisha makosa yaliyofanyika na Mkapa katika sera zake za ubinafsishaji na kuwaleta wageni 'wawekeze' hakutafanikiwa bila kuyajua kwa undani matatizo yaliyotufikisha hapa tulipo ili marekebisho hayo yaweze kuzaa matunda ambayo Watanzania tunayategemea na pia kutorudia tena matatizo ya awamu ya tatu au hata ya nne.
 
Jokakuu,

Swala la Mkapa kumlaumu litaendelea kuwepo, lakini binafsi nimemkubali tu pale alipoonyesha kwamba swala la mikataba yote ikiwa ni pamoja na madini inaweza kurekebishwa tofauti na viongozi au Kikwete alkivyokuwa akidai..

Kwa hiyo hii ni hatua nzuri alochukua na nadhani imetokana na majuzi Bush alipokuwa akihojiwa amekubali baadhi ya makosa ktk Utawala wake, hivyo akaona umuhimu wa yeye pia kukubali makosa.... unajua tena sisi kwa kuiga.

Tofauti inakuja tu kwamba wenzetu waliyaona haya mapema na wakamchagua mtu ambaye anaweza kurekebisha, wakati sisi ndio kwanza utawala mzima umeziba masikio na kusema kelele za mlangoni haziwazuii kulala..Hizi sio kelele tu ila mjenzi wa nyumba hiyo ametuhadharisha hatari iliyopo sio ya kelele za watu ila Uimara wa nyumba nzima...

Ni mwanzo mzuri sana kiuchumi, na Mkapa mwenyewe ataendelea kulaumiwa kama Bush na utawala wake.
 
JokaKuu,

nilichokuwa nasisitiza pale juu ni fact kwamba Serikali haiku plan vyema ubinafsishaji. Kama wangekuwa wamefanya kazi nzuri ya ku plan basi hii mikataba inayowanyonga watanzania ingeweza kuwa avoided. Lakini zoezi zima liliruhusu mianya ya rushwa na watu wachache wakataka kujinufaisha kwa haraka zaidi bila kujali effects za hiyo mikataba waliyoingia kwa niaba ya Taifa, miaka 10, 20 baadae.

Naamini kama Mkapa and his regime wangechukua muda ku study zoezi zima la uwekezaji na kufanya mambo kwa uwazi, hali ingekuwa better kuliko sasa hivi. Sisemi kwamba tungekuwa tumefanikiwa 100% hapana, lakini kwa kiasi kikubwa tatizo la mikataba miref
u, isiyo na manufaa kwa Serikali lingekuwa sio la magnitude kubwa kama sasa hivi.
 
zamani tulikuwa tunasema "gia ya kuingilia".. naamini hii ni mojawapo.., ya pili itakuwa ni kusikitikia wafanyakazi wa umma kujinufaisha kutokana na nafasi zao na atasikitika sana hawakuweza kusimamia maadili kwani waliamini kila mmoja ni mzalendo..


Ha Ha ha mkulu mwanakijiji hii inahuhuzunisha vile vile inafurahisha. lakini pamoja na IMF na WB study nyingi za ndani zilikuwa zinaonyesha mashirika ya uma hayaperform na mapendekezo yakitolewa yabinafsishwe. Nakumbuka nilikuwa nafanya dissertation yangu kama partial fulfilment ya shahada yangu ya uchumi Bongo miaka hiyo na mpaka paper nyingi za Profs. wa bongo pia zilikuwa zikizumgumzia swala hilo hilo la ubinafsishaji. Pengine Mkapa kwa kusikiliza ushauri wakitaalam akaamua kutekeleza hilo.

Kosa kubwa hapa ni namna zoezi la ubinafsishaji lilivyofanyika maana haukuwa ubinafsishaji bali redistribution ''come and take''. Hapo dnipo alipolikoroga sijui kama ilikuwa kwa kutojua au maksudi kutimiza mission fulani. nakwa hili nadhani PSRC pia inabidi iwajibike kwani ilipaswa kuwa na utaratibu endelevu wa kufanya ubinafsishaji na si kubinafsisha hata visivyobinafsishwa.

May be muungwana anamaanisha kujutia hili ''Dramatugical!!!!!!!!!!!!!''
 
Ya kweli haya ama Mkapa anatania?. Arudishe kiwira kwanza kwa watanzania ndipo tutaamini kwamba anajutia alichokifanya.
 
Pasco ni kweli ni hearsay, lakini tunaweza kufuatilia ili kuhakikisha je, kulikuwa na kikao kilichofanyika Z'bar kilichoandaliwa na UVCCM. Je, Thabo Mbeki hivi karibuni alikuwa Z'bar? kwa shughuli ipi? na je alihudhuria kikao cha UVCCM kilichofanyika Z'bar hivi karibuni? Je, Mkapa alikuwa Z'bar hivi karibuni? kwa shughuli ipi? Tukipata majibu ya maswali hayo ama tunaweza kuukaribia ukweli au kuzidi kuwa mbali nao.

Sasa majina ya baadhi ya waliohudhuria kikao hicho yamewekwa hadharani. Basi ni wajibu wao kukanusha habari hii kama Mkapa hakutamka maneno hayo. Kukaa kwao kimya kuhusiana na habari hii ni ufisadi wa aina yake.

Kwa vile news break imetolewa leo, naamini UVCCM watafanya Press Conference kesho na kukanusha hakuna kitu kama hicho kwenye mkutano wao. Kwa vile kilikuwa ni kikao cha siri, watasema Tanzania Daima ni waongo na story itaishia hapo.

Kati ya marais wetu, hakuna rais sturborn kama Mkapa. Huyu jamaa hata kama kweli aliyasema hayo, he is too sturborn to addmit mistakes. Kwa waliowahi kuiona Hard Talk ya Mkapa na Tim Sebastian kwenye BBC watakumbuka alikasirika na kuvimba kama anataka kupigana. Kisa aliulizwa swali kuhusu ubinafsishaji was a mistake. Leo siamini ni Mkapa huyo huyo kaja kukubali eti "It was a mistake. Leys wait for the reaction"

By the way, nimeipitia Katiba yetu na kugundua Mkapa hana kinga kwa hayo aliyotenda. Ibara ya 46 imempa kinga. Ibara ya 46.A (2)(a) imeiondoa kinga na kusema rais anaweza kushtakiwa kama amevunja katiba au kama amekiuka maadili ya uongozi.

Hii maana yake Mkapa hajaburutwa Kisutu kwa sababu wanamstahi tuu na sio sababu ya kinga.
 
Mkuu Pasco , pamoja na kuwa inawezekana kuwa ni hearsay laikini habari imeandikwa na haijakanushwa.
Lets wait and see.
Hata hivyo inaelekea the sentiments are geunine hata kama hazikuwa for public consumption.

Mkuu Gwakisa, kwa vile habari ni ya leo tusubirie kesho. Uwezekano wa Mkapa kuyasema haya kwenye closed meeting upo ila yakitoka nje, siyo Mkapa atayekanusha ni UVCCM watakanusha tena ni kesho tuu. Mkapa mwenyewe ni kiburi na jeuri, he is too sturborn to addmit his mistakes.
 
- Mkuu Bob, nimekusikia sana nilichouliza ni kwamba unasema kuna mahali Mwalimu alikubali hadharani mbele yetu wananchi kuwa Ujamaa wake ulishindwa? Alisema exactly that au?


Kwenye hotuba/press conference,sikumbuki katika tukio gani nyerere alisema 'tulifanya makosa,tulifanya makosa,hatukuwa malaika sisi,tulichukua nchi tukiwa na wasomi wachache,kama kitoto kilichotupwa baharini kinatapatapa,hakina msaada...lakini sasa hawa wenzetu wanaacha kuendeleza yale mazuri tuliyoyafanya wanachukua mabaya..'
Halafu aliulizwa sikumbuki kama na BBC au la na sikumbuki vizuri swali lilikuwaje lakini muulizaji alitaka kujua kama nyerere angeweza kurudi tena na kuongoza tanzania,nyerere akasema kama alishindwa na ujamaa wake kwa miaka zaidi ya ishirini itakuwa wakati huu wa kuongoza kwa vipindi vya miaka mitano mitano..
Kitu kama hicho.Wanaokumbuka vizuri watatufahamisha.
 
Pasco,

Hiki ki-habari cha TanzaniaDaima ni udaku mtupu. Mkapa ana soo la kubinafsisha mgodi na partner in crime wake Daniel Yona ana kesi mahakamani kuhusiana na haya haya ma hanky-panky ya dealings za serikali na wawekezaji, hawezi kujitia kitanzi kukiri makosa saa hizi.

Sio principle za journalism tu, hata za stori za mtaani haziendi hivyo. Hivi tukiwa tunamtafuta Juma atujibu kuhusu mali zetu halafu tunakuja kuambiwa kuna fulani kasema Juma kakiri kosa, hatutataka kujua huyo fulani anaesema Juma katubu ni nani, na nani mwingine alisikia wakati anatubu? Halafu alipokubali makosa alisema nini kuhusu mali zetu going forward? You know?

Halafu ki-habari kina misrepresent ukweli kwa kusema pressure ya kumshitaki Mkapa imeongezeka. Kila kukicha tunasikia padri so and so mbunge huyu na yule wanasema let this Mkapa character alone, sasa hiyo pressure iko wapi? Na Pinda keshapayuka kwamba it's a complicated process.

Kinga yenyewe walivyoiongelea ni misrepresentation tupu. Hakuna sehemu kwenye Katiba paliposema Wabunge wanaweza kuondoa kinga. Itabidili Wabunge waandike kipengele hicho cha Katiba upya, na hiyo ndio itahitaji theluthi mbili za wabunge, tena inabidi ipatikane kote Zanzibar na Bara separately.

Halafu Pasco, notice kwamba kwenye misingi journalism, ilibidi pale kwenye paragraph ya kwanza, au ya pili at the latest, waseme kwamba wanaripoti based on stori ya kuambiwa na anonymous source. Walivyoiweka ni kama wao Tanzania Daima ndio wanaripoti wakati hawana uhakika. Wakishitakiwa watasema sisi tumeambiwa na mtu, lakini hapa wameitengeneza kuwa-fool unwary readers kama wana uhakika vile. Wadaku.

Halafu, notice vi-taarifa ambavyo hawana uhakika hawatoi jina la mwandishi, wanavunja cardinal rule of journalism, inayotakiwa kuleta credibility na accontability.

Eti gazeti linaripoti kwa kuambiwa na mjumbe mmoja, udaku, uzushi, vilaza wakutupwa nje ya press room.
Mkuu Kuhani, heshima mbele.
Yote uliyasema ni kweli tupu, naomba tuwasamehe waandishi wetu wa habari, fani imevamiwa, ila hata ikivamiwa, ma editor nao wamevamiwa?. Hii ilikuwa kazi ya editor ku double chech na cross check hiyo story ili aibalance hata kiuongo uongo kwa just a line, 'juhudi za kumpata Mkapa kuthibitisha hazijazaa matunda sambamba na kuwapata maofisa wa UVCCM hawakupatikana'. Hii ilitosha kubalance na kuwathibitishia wasomaji, this is developing story na itaendelea.

Hili la kinga ya Mkapa kutoshitakiwa, nimethibitisha kwa katiba halipo. Yaani hana kinga!.
Natafuta muda muafaka nilianike vizuri tuu in black and white. Kinga sio issue, Pinda nae hana lolote, angesema tuu wazi, Mkapa ni binadamu, kwa heshima za Kiafrika/Kitanzania, tunawaheshimu wakubwa na wazee, hivyo Mkapa tunamstahi kwa heshima tuu na sio ka mujibu wa kinga Katiba.
 
Kwenye hotuba/press conference,sikumbuki katika tukio gani nyerere alisema 'tulifanya makosa,tulifanya makosa,hatukuwa malaika sisi,tulichukua nchi tukiwa na wasomi wachache,kama kitoto kilichotupwa baharini kinatapatapa,hakina msaada...lakini sasa hawa wenzetu wanaacha kuendeleza yale mazuri tuliyoyafanya wanachukua mabaya..'
Halafu aliulizwa sikumbuki kama na BBC au la na sikumbuki vizuri swali lilikuwaje lakini muulizaji alitaka kujua kama nyerere angeweza kurudi tena na kuongoza tanzania,nyerere akasema kama alishindwa na ujamaa wake kwa miaka zaidi ya ishirini itakuwa wakati huu wa kuongoza kwa vipindi vya miaka mitano mitano..
Kitu kama hicho.Wanaokumbuka vizuri watatufahamisha.
Mwalimu alikubali makosa alipotangaza Azimio la Arusha alisema itatuchukua miaka 30 kuujenga ujamaa. Baada ya miaka 20 akakubali tulikosea, akasema itachukua muda mrefu kuujenga ujamaa, hata hivyo akasisitiza, kuna makosa mengi tumefanya huko nyuma ila nanukuu"Kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa". Mwisho wa kunukuu.
 
Heshima mbele sana Wakuu wote JF, juzi nimeangalia kwa mshangao mkubwa sana the so called wasomi wetu wakiongozwa na Shivji, wakimshambulia Rais mstaafu Mkapa, kuhusu Ubinafsishaji, I mean let me say this:-

- Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake apewe, sijawahi kuwa a big fan wa siasa za Mkapa, lakini this one I must say with my clear mind kwamba he was 100% right, Shivji na wenzake wako not only wrong isipokuwa ni professionals cying babies, wamezoea kila Awamu huwapa ujumbe wa bodi na kamati kamati za mlo, sasa ikitokea aawamu kama ya Mkapa ikawanyima mlo, basi huanza kuiandama ile Awamu wee na vilio vyao vya machozi ya mamba, kumbe ni waongo wakubwa!

- Mkapa was right kubinfsisha kwa the FACT ya kuyaondoa mashirika na viwanda vilivyokuwa vimeathirika na utawala unaofuata siasa za sera zilizoshindwa za Azimio la Arusha, utawala ulikuwa mbovu na uliokufa. Ili kujenga uchumi imara unahitaji kuwa na Capital, Markets, na Leadership, ambavyo vyote havikuwepo under mfumo wa Azimio la Arusha tulilokuwa nalo then, ambalo haliwa freindly na wageni kuja kuwekeza, kwa hiyo ilikuwa ni sawa kwa Mkapa, kuyauza na mengine kuwauzia wazawa ili yaweze kusimama na kuendelea tena. In the process Mkapa alibinafsisha mashirika na viwanda 330, 180 aliwauzia wazawa ambayo ni more than 50%, 23 tu aliwauzia wageni na 127 alitoa kwa ubia wa wageni na wazawa, matokeo yamekuwa Serikali kukusanya Shillingi Billioni 250 kwa mwezi kwa mashirika machache tu kama NBC, CRDB, TCC, na TBL as opposed to Shillingi Billion 10 tu zilizokuwa zikikusanywa kabla ya Mkapa kubinafsisha.

- It is about time sasa Shivji na wenzake wakajitokeza kwenye nafasi za uongozi wa taifa ili tuone uwezo wao wa kufikiri kuliko kulia lia kwa kila awamu. Ni lini watajikita kwenye kutoa solutions badala ya kulaumu tu kila siku kwa sababu ya kukosa mlo? I mean hili taifa wengine tumechoshwa sana na hawa crying babies wasiokuwa na jipya zaidi tu ya kulilia defeated theories ambazo tumezijaribu na zimtufikisha hapa tulipo pabaya sana hili taifa.

NINASEMA TENA KWENYE KUBINAFSISHA, MKAPA WAS RIGHT 100%, SHIVJI NA WENZAKE SHOULD APOLOGIZE KWA KUMSHAMBULIA MKAPA BILA SABABU KWENYE KIGODA!


William.

-
 
Back
Top Bottom