Ubinafsishaji: Mkapa alikosea?


Hilo ndio lilikuwa tatizo la mashirika mengi ya umma. Management, Bodi, na serikali kuingilia maamuzi ya bodi/management.

Mifano mizuri bado tunayo, TANESCO. Walipokuwa wanakuja NetGroup Solution, Management, Board na TUICO walipinga kwa nguvu zote mpaka wakamsomesha Waziri wa Nishati na Madini zama hizo Maokola Majogo na akawaelewa na kukubaliana na TANESCO kwamba NetGroup wasije. Mkapa alipoona home-boy wake Maokola Majogo ame-side na TANESCO, Majogo alitupwa ofisi ya Makamu wa Rais (Kuondoa Umasikini) akaletwa mwingine ili kuja kukamilisha deal. Kilichoendelea wote tunajua, na hata Richmond nayo hivyo hivyo, ni serikali kuilingilia kila kitu.

TPA na wao hawakuachwa, kuna siku DG wa TPA nimesahau jina lake, alimwambia Mkapa wakiwa Mtwara, kwamba kama yeye (DG wa TPA) angepewa mamlaka ambayo wanapewa wageni ya kufanya maamuzi bila kuingiliwa, ana uhakika TPA ingekuwa mbali. Tatizo la mashirika mengi ya umma, kila unachofanya lazima kipate approval kutoka wizarani, na huko wizarani wanaangalia kwanza maslahi. Hilo ndilo lililikuwa kikwazo kwa mashirika mengi sana. Utahangaa GM au DG yule yule aliyekuwa anaongoza shirika kwa hasara, once likibinafsishwa kampuni inaanza kutengeneza faida, hakuna cha kuongeza mtaji wala nini, na si ajabu hata teknolojia ni ile ile.
 

- Thank you great thinker!

William.
 
Prof. Shivji aliwahi kupewa u RDD (Regional Development Director) katika Mkoa wa Rukwa enzi za Mwalimu, akachemka.
 

unauza njia kuu za uchumi then unategema nchi kupaa kiuchumi?

ktk dunia hii sijawahi ona nchi iliyoendelea kwa kuuza viwanda vyake,haipo mahali popote pale,yaani serikali inauza mashirika ya umma na viwanda vyake ili ijikite ktk ukusanyaji kodi na hata ktk ukusanyaji kodi bado unampa mwekezaji miaka mitano ya majaribio na kumlipiza TSH 250/H kt ardhi then unategemea utatoka ktk umasikini,haiwezekani hata siku moja
 
Bahati mbaya si rahisi sasa kumdanganya mtwana anaeguswa na athari za maamuzi ya kipuuzi na hasa anapojua haki zake.

1. Mwinyi was a disaster

2. Mkapa was a calamity

3. JK is both a disaster, a calamity and a liability

4. CCM is the devil himself engineering all the above

My uncle Willy you are a right product of the above
 

- Katika dunia hii sijawahi kuona taifa liliondelea kwa serikali yake kumiliki viwanda na mashirika, ila nimeona mataifa yakiendelea kwa kukusanya kodi tu! na kusimamia sheria!

William.
 

- Sure I live with that!

William.
 
- Katika dunia hii sijawahi kuona taifa liliondelea kwa serikali yake kumiliki viwanda na mashirika, ila nimeona mataifa yakiendelea kwa kukusanya kodi tu! na kusimamia sheria!

William.

nakupa mfano mdogo sana

china
serikali inamiliki china mobile,china unicom,usafirishaji wa reli,barabara na majini,viwanda(baadhi inamili kwa 100% na baadhi imeshare na wawekezaji)

nimekupa mfano mdogo sana
 
nakupa mfano mdogo sana

china
serikali inamiliki china mobile,china unicom,usafirishaji wa reli,barabara na majini,viwanda(baadhi inamili kwa 100% na baadhi imeshare na wawekezaji)

nimekupa mfano mdogo sana

- Mkuu nimewahi kuishi Shanghai, China wana utawala unaoheshimu Sheria hakuna mahali wanamiliki 100% anything katika hayo mashirika machache ambayo Serikali yao imeamua kwamba ni lazima yawe chini ya serikali, infact hata US shirika la post na amtrack Train, bado yapo chini ya serikali na ni baada a mabunge ya nchi zao kuamua kwamba hayo mashirika machache walioyaacha under serikali yakipewa private wananchi watateseka sana,

- Otherwise sio hata 1% ya mashirika yote ya mataifa yao, hiyo inakubalika ninaamini hata sisi bado tuna umiliki mkubwa kwenye posta yetu, hilo wala sio ishu mkuu!

William.
 

haya rudi tanzania,tunajivunia kwa kiwanda kipi,migodi wanamiliki wawekezaji(china pale inner mongolia ambako ndiko kwenye upatikanaji wa madini -serikali inamiliki 100%)

usafirishaji wa abiria (daladala) serikali inamiliki 100% ingawaje na wawekazaji wapo) UDA tumeuza,

faida ya ubinafsishaji tanzania haipo ,zaidi ya kusaidia wajanja wachache
 
Mkapa alibugi mambo mengi sana.Alitumia kivuli cha so called utandawazi kwenye Mkt Economy kufanya uchafu alioufanya kipindi cha utawala wake.Alidanganya uma kuwa alichokuwa anakifanya ni matakwa ya utandawazi.Utandawazi aliokuwa anaushabikia Mkapa ni ufisadi na uporaji rasilimali kwa nchi na kuwapa wageni.

Ukipitia kabrasaha kutoka IMF kuhusu ubinafsishaji vipo vipengele, wazi vinaeleza kuhusu vitu ambavyo serikali inaweza kuacha kubinafsisha. Hii ni kwa ustawi wa nchi kuweza kuwa na nguvu/sauti kwenye uchumi . Pia ni njia ya kulinda rasilimali za nchi-Mfano Bank ya taifa,Ports ,Railwayz.Pia imeelezea wazi kuhusu rasilimali kama madini kuwa serikali inaweza ingia ubia kulinda maslahi ya wananchi kutokuporwa rasilimali zao moja kwa moja.

Suala la kustaajabu Mkapa na genge lake la wezi wakadanganya uma kwa manufaa yao. Wakati huo huo baadhi ya wasomi walikuwa wanatumiwa kuwapumbaza wananchi kuwa mashirika ya fedha duniani IMF na WB ndio yanatoa muongozo huo unaotunyonya(wakimsafisha Mkapa)
 
....Duh enzi hizo!!!! kaka Mbu naye alikuwa anachangia kwenye siasa...siku hizi yuko kwenye football na MMU kwingine hachezi kabisa 🙂🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…