Ubinafsishwaji wa tanesco

Ubinafsishwaji wa tanesco

mutate

Member
Joined
Mar 12, 2014
Posts
7
Reaction score
1
Ubinafisishwaji ni tendo ambalo linahusisha kuamisha mali ya umma ama moja kwa moja au sehemu ya mali hiyo kutoka kwa serikali kwenda kwa wadau binafsi. Lengo kuu ni kutaka kuleta wadau wengi zaidi katika shughuli au mali husika. mfano kama shirika linalotoa huduma ya jamii kama Tanesco ubinafsishaji ungelenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

lengo jingine kuu la ubinafsihsji ni kuongeza ushindani wa soko na ubunifu. ambapo mashirika au shughuli mbali mbali za serikali upata nafasi ya kushindana na zile za binafsi zenye kufanya biashara. sera hii imekuwepo hapa Tanzania kuanzia miaka ya 1980 lakini imepata urasmi kuanzia mwaka 1992 ambapo mashirika kama Benki, shirika la posta, na mashirika mengine yalianza kubinafsishwa ili kuongeza ubora. TANESCO kwa upande wake jenyewe limeendelea kumilikiwa na serikali kwa asilimia mia moja.

jambo la kampuni hili muhimu mno kwa uchumi wa nchi kuendelea kumilikiwa na serikali kwa asilimia mia moja linasababisha kkuzolota kwa uchumi na huduma kwa jamii. shirika linakosa uwezo wa kubuni njia mbadala za kuzalisha umeme wa kutosha na njia za kujishirikisha na jamii yake.

sasa swali langu ni kitu gani kinazuia shirika hili lisitolewe katika mikono y aserikali japo kwa asilimia?
 
Watanzania tuna ulimbukeni sana na neno "ubinafsishaji" na halafu upungufu ulioko katika lugha yetu ya kiswahili, ndipo tunapozidi kuchanganyikiwa. Katika kiingereza kuna maneno State Ownership (Parastatal), Public Ownership na Private Ownership. Katika Kiswahili tuna "Mali ya Umma" na "Mali ya Binafsi", kwa hiyo hapo ndipo tunapokorogekewa sana, kwa sababu tunaamini kuwa ni ama mali ya umma kama ilivyo Tanesco au ni mali binafsi kama ilivyo IPP. Tulliingia katika soko la kubinafsisha mali za umma bila kujua tofauti baina ya State Ownership na Public Ownership na ndiyo maana tukaruka grupu hilo na kuishia kwenye Private Ownership kuwa ndiyo maana ya "Ubinashaji." Tuna ugonjwa wa ubinafsi sana leo, kwani process yote ilienda kibinafsi. Kila siku utasikia tunamtafuta mwekezaji anunue shirika fulani halafu process yote ya ununuzi inafanywa siri.

Wakati Kenya walipobinsfaidha Kenya Airways, waliitoa kwenye state ownership na kuiweka kwenye public ownership, na kwa hiyo hakuna mtu anayedai kuwa KQ ni mali yake binafsi. Na kweli KQ imekuwa ni mfano mkubwa sana wa mafanikio ya public ownership. Lakini Tanzania utashangaa hakuna enterprise yoyote ambayo kweli ni public, zote ama ni private au ni State Owned.

Sasa sijui ndugu yangu alikuwa ana maana ya kuifanya TANESCO kuwa Private, au kuwa Public au ubaki kuwa State owned. Makampuni makubwa karibu yote ya nchi zilizoendelea ni Public owned; ni machache sana ambayo ni private, na ni kiduchu sana ambayo ni State Owned isipokuwa huko China ambapo bado makampuni mengi ni state owend ingawa wamekuwa waki-transition kuyafanya kuwa public owned.
 
shida yangu sio tofauti ya "state" au "public" shida yangu ni ufanisi. kwa sababu hata hiyo state inaown kwa interest ya nani? kimsingi state/dola ni la kila mtu hata huyo private. lakini ukiangalia tafsiri ya state owned interprise kwenye enterprise management utaona inamaana sawa na public enterprise. sheria ya makampuni ya mwaka 2002 inaonyesha hivyo na inatfsiri hivyo. inashida kuwa na jina la majumuisho au la tafsiri ya majumuisho bali uendeshaji unafananaje. mfano IPP ni private company ambalo kwa tafsiri yoyote halina aina ya public ownership au state ownership. lakini TANESCO ni state owned company lakini lina sense ya public and state ownership, na hakuna single entity ndani ya public anweza kuassume ownership. hivyo majina hapa sio tatizo nadhani.
'
 
shida yangu sio tofauti ya "state" au "public" shida yangu ni ufanisi. kwa sababu hata hiyo state inaown kwa interest ya nani? kimsingi state/dola ni la kila mtu hata huyo private. lakini ukiangalia tafsiri ya state owned interprise kwenye enterprise management utaona inamaana sawa na public enterprise. sheria ya makampuni ya mwaka 2002 inaonyesha hivyo na inatfsiri hivyo. inashida kuwa na jina la majumuisho au la tafsiri ya majumuisho bali uendeshaji unafananaje. mfano IPP ni private company ambalo kwa tafsiri yoyote halina aina ya public ownership au state ownership. lakini TANESCO ni state owned company lakini lina sense ya public and state ownership, na hakuna single entity ndani ya public anweza kuassume ownership. hivyo majina hapa sio tatizo nadhani.
'


Nafikiri unakubaliana nami kuhusu ugumu wa uendeshaji wa biashara kubwa Tanzania: ni ama iwe state owned au private owned. Sijasoma sheria hiyo ya makampuni ya mwaka 2002 kwa hiyo sintapenda niseme kitu nisichiokijuwa, ila jambo ambalo nami nakubaliana nawe ni kuwa Shirika likiwa la Umma kwa maana ya kuwa state owened, linakuwa linawajibika kwa waziri mhusuika pamoja na bodi yake. Kwa hiyo likiwa katika matatizo ya kipesa ni rahisi kuhamishiwa pesa za kodi kulilinda kama ambavyo Tanesco ilivyo leo, na likitaka kupandisha gharama kwa wateja wake basi linakuwa na urahisi kufanya hivyo. Kuna haja kubwa sana ya kuindolea Tanesco kinga ya serikali lisiwe linamilikiwa na serikali. Hata hivyo kulifanya Tanesco kuwa mali biansfsi isiyokuwa na ushindani ndilo litakuwa ni tatizo kubwa zaidi. Njia pekee ni kuivunja Tanesco kuwa makampuni mawili au matatu na kuyafanya kuwa public. Halafu baada ya hapo serikali inayapa kila msaada, kwa mfano infrastructure, ili yashindane katika kuwahudumia wanamchi.
 
Back
Top Bottom