Ubitozi huu wa suruali za wavulana wa Sekondari ni wa kipumbavu kuliko Enzi zetu

Ubitozi huu wa suruali za wavulana wa Sekondari ni wa kipumbavu kuliko Enzi zetu

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Wanavaa tusuruali hatufiki chini.
Hawavai soksi.
Kuimba vinyimbo vya kikekike

Enzi zetu (90s na early 2000s)

Uhuni ni kuvaa suruali inaitwa pisto. Hizi walivaa masteringi wa movie za Kachina na makachero wa mossad miaka ya themanini

Uhuni kunyanyua vyuma.

Hata hizi wanazovaa waheshimiwa suruali zisizo na marinda zilikuwa Uhuni.

Sasa Hawa vijana siku hizi wanavaa suruali za kipumbavu. Hizi Enzi zetu walivaa mabibi wa kichina kwenye movie.

Nimepita kijiwe cha shule flani hapa wavulana wa shule wahuni wote wameedit visuruali wapowapo tu, nimetsmani kuwalamba makofi wote.

Mkuu unakumbuka nini kuhusu Uhuni wa zamani ukilinganisha na Hawa wa kisasa.
 
matunduizi,
Mkuuu umetisha...
Nakumbuka enzi hizo ujanja ni kuvaa bonge ya buti mguuuuni halafu suruali chini bwangaaaaaa inafunika hadi hilo buti. Ndani ya buti palikuwa tunajaza matambala ili lieneee vizuri mguuuni. All in all kila zama na kitabu chake acha Vijana wajinafasi na fesheni ya wakati huu, hakuna namna.
 
Mkuuu umetisha...
Nakumbuka enzi hizo ujanja ni kuvaa bonge ya buti mguuuuni halafu suruali chini bwangaaaaaa inafunika hadi hilo buti. Ndani ya buti palikuwa tunajaza matambala ili lieneee vizuri mguuuni. All in all kila zama na kitabu chake acha Vijana wajinafasi na fesheni ya wakati huu, hakuna namna.
Fashion za vijana tatizo zinakua influenced sana na dada zao visuruali vya kubana makalio kupaka lipshiner kubeba vimkoba vidogo nk
 
Sisi wahuni wa zamani mashuleni ndo TULIKUWA WAHUNI KWELI, achana na hivi vihuni mayai mayai vya .com !

Mhuni wa school enzi zile nilikuwa nakula ugali mkubwa + maharage yenye wadudu, siyo hawa 'wapuuzi' wa leo wanakula chipsi + kuku shuleni halafu wanajiita wahuni.

Wazee wa kazi tulikuwa tunakula 'ndumu' vibaya mno, yet tunagonga division 1 & 2 za ukweli. Pale Tambaza,Tabora Boys,Mirambo,Mzumbe,Ilboru,Sengerema,Geita,Bwiru,Mara Sec, Musoma Tech, Iyunga, Mkwawa, n.k wahuni wengi walipita pale ndo walifika Universities na leo ni Watendaji waandamizi serikalini. Lakini leo dent mpuuzi mpuuzi anajiita mtuni halafu ufaulu wake mkubwa ni division 4.

Wahuni wa skonga enzi za 90s tulikuwa tunapenda miziki yenye message, siyo wahuni wa leo wanasikiliza wabana pua e.g akina Diamond, Harmonizer, etc wanaoimba nyimbo za kijinga kijinga e.g UNO na upuuzi mwingine. Sisi enzi zetu tulikuwa tunasikiliza 'mawe' ya akina Bob Marley,Lucky Dube,2Pac Shakur, Notorious B.I.G 'Big Popa' , Coolio, Wu-Tang Clan, Dr.Dre, Quuen Latifah, Mary J. Bridge, Miss Eliot, MC Light (huyu mdada nunda alikuwa na hip-hop kali sana). Hapa Bongo tulikuwa na akina GWM(Gangsters With Matatizo), Sos B (alikuja kuwa mtangazaji pale Radio One), Mr. 2 Sugu, na wakali wengineo. Hip- hop naipenda hadi leo maana mara nyingi ina message na inagusa maisha halisi ya watu, no room fo mapenzi, no room kujipendekeza kwa watawala, no room for kubana pua.

I wish I stay in the shadows of the 1990s for eternity.
 
The Sun-of-a Beach,
We mhuni wanikimbusha mbali wahuni wa boys school na ugomvi wao na mirambo boys wahuni wakazichapa pale ally Hasan Mwinyi alafu wakataka kufukuzwa shule mpka waalimu wakaogopa kufanya uhuni huo baada ya kuona wahuni hao wote 20 bora wangefanya paper la form four wangetoka na moja ya saba, ni kweli baada ya kushindikana kufukuzwa wahuni wabaki kilichotokea ziligongwa one ya 7 kama mvua hivyo jumla yake kukiwa na one 86.

Madogo wa siku hizi ni takataka tu hawana lolote kichwani ni zero uhuni watuachie sie wazazi wao maana tulitisha kichwani zimo na ukorofi juu,

Mliolala Bweni la Kimweri njoon hapa maana hilo bweni ndio lilikuwa na wahuni
 
Madogo siku hizi wanavaa visuruali vidogo sana

Na uhuni wao eti wanaweka zipu kwenye suruali upande wa mguuni ili akiwa anavua asihangaike.
 
Back
Top Bottom