Sisi wahuni wa zamani mashuleni ndo TULIKUWA WAHUNI KWELI, achana na hivi vihuni mayai mayai vya .com !
Mhuni wa school enzi zile nilikuwa nakula ugali mkubwa + maharage yenye wadudu, siyo hawa 'wapuuzi' wa leo wanakula chipsi + kuku shuleni halafu wanajiita wahuni.
Wazee wa kazi tulikuwa tunakula 'ndumu' vibaya mno, yet tunagonga division 1 & 2 za ukweli. Pale Tambaza,Tabora Boys,Mirambo,Mzumbe,Ilboru,Sengerema,Geita,Bwiru,Mara Sec, Musoma Tech, Iyunga, Mkwawa, n.k wahuni wengi walipita pale ndo walifika Universities na leo ni Watendaji waandamizi serikalini. Lakini leo dent mpuuzi mpuuzi anajiita mtuni halafu ufaulu wake mkubwa ni division 4.
Wahuni wa skonga enzi za 90s tulikuwa tunapenda miziki yenye message, siyo wahuni wa leo wanasikiliza wabana pua e.g akina Diamond, Harmonizer, etc wanaoimba nyimbo za kijinga kijinga e.g UNO na upuuzi mwingine. Sisi enzi zetu tulikuwa tunasikiliza 'mawe' ya akina Bob Marley,Lucky Dube,2Pac Shakur, Notorious B.I.G 'Big Popa' , Coolio, Wu-Tang Clan, Dr.Dre, Quuen Latifah, Mary J. Bridge, Miss Eliot, MC Light (huyu mdada nunda alikuwa na hip-hop kali sana). Hapa Bongo tulikuwa na akina GWM(Gangsters With Matatizo), Sos B (alikuja kuwa mtangazaji pale Radio One), Mr. 2 Sugu, na wakali wengineo. Hip- hop naipenda hadi leo maana mara nyingi ina message na inagusa maisha halisi ya watu, no room fo mapenzi, no room kujipendekeza kwa watawala, no room for kubana pua.
I wish I stay in the shadows of the 1990s for eternity.