Brojust
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 349
- 1,024
Salamu kwa nyote mnaosoma uzi huu.
Baada ya kufikiria kwa kina basi haya ni maswali yangu matano kuhusu ubongo wa binadamu.
Swali 1: Kama binadamu amegundua computer, na haya mambo yote tunayoyaona kuhusu teknolojia, Je ni kitu gani kitakuja kuvumbuliwa na binadamu ambacho kitashinda uwezo wa ubongo wa binadamu ?
Swali 2: Je, ni kweli au si kweli kwamba ubongo wa binadamu ndio chanzo cha uhai wa mwanadamu ? Mimi sio daktari lakini nilisikia kwamba kuna uwezekano kwamba viungo vyote vya mwanadamu vikizima ubongo ndio unakuwa kiungo cha mwisho kuzima na hapo ndio madaktari wanatoa declaration kwamba huyu amekufa.
Swali 3: Ubongo wa binadamu ndio umegundua sayansi zote kama ile sayansi ya kutuma darubini kubwa kushinda zote kwenye space inayoweza kuona vitu vilivyo kuwa mbali kwenye ulimwengu kwa bilions light years, Je kwanini mwanadamu mpaka leo ameshindwa kuwa na jibu la uhakika kuhusu chanzo cha ulimwengu ? Je tuamini ni kati ya IMANI na SAYANSI.
Tuanze kwanza na maswali haya, nitaendelea na swali la 4 na 5.
Nawatakia weekend njema na tuzingatie sana lugha rafiki kwenye uzi huu.