Habari.
Wote ni wazima wa afya na vyema tuendelee kumshukuru Mungu Kwa wema wake kwetu.
Twende kwenye mada Moja kwa Moja juu ya mchezaji bora mwenye nguvu na kasi akiwa uwanjani.
Clement Mzize amekuwa akifanya vizuri sana Kwa sasa hata kwa takwimu zinaonekana mbali na ubunifu ulioungana na unyumbulifu wa stadi ulioambatana na kipaji kilichoongezwa bidii.
Huyu Clement Mzize wa sasa Ubora na umahili wake unaonekna baada ya Juhudi na bidii na sasa mpira safi unaonekana awapo uwanjani, amekuwa mchezaji machachali kweli kweli na bora zaidi.
Ila mnamkumbuka Clement Mzize baada ya mechi ya Young Africans Vs Mamelod Sundowns mkondo wa kwanza Ligi ya mabingwa Africa baada ya mechi kuisha kwa matokeo ya bila kufungana?
Clement Mzize alipigwa vita vikali na hata Baadhi ya watu Kusema anatakiwa kuondolewa hata kwa mkopo baada ya kukosa magoli mengi kwenye mechi hiyo.
Clement Mzize alijifunza na kutulia Hadi Sasa tumeanza kuona makali yake pamoja na Ubora wake akiwa Young Africans.
Hilo ni funzo kwa wachezaji wetu wengine wazawa wajifunze kwa kinda mdogo Clement Mzize.
Nawasilisha Mzee Mkoloni.
View attachment 3391476