Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzimu! Kwa maoni yangu umegusa "kansa" ambayo imefikia kiwango cha kutotibika. Ninadhani tukubali matokeo kuwa Lugha yetu adhimu, Kiswahili, inapitia kipindi cha mpito kitakachopelekea kupatikana kwa Lugha nyingine kabisa, kama ambavyo Lugha yenyewe ya Kishwahili ilivyoanza.
Juzi hapa hapa JF kuna Mdau amemrekebisha Mchangiaji kuwa lugha sahihi ni "hela" na sio "ela", "halafu" na sio "alafu", "hebu" na sio "embu" n.k. na alichoambulia ni matusi. Wachangiaji ni Wasomi watarajiwa wa Nchi hii. Hiki ni Kizazi ambacho hakiwezi kuandika na kuongea lugha yoyote kwa ufasaha iwe Kiswahili au Kiingereza.
Umetaja Wadau na Makundi kadhaa yenye dhamana ya kukilinda Kiswahili yaani Wanamziki wa Mziki wa Kizazi Kipya (ambao wengi wao hata Elimu ya Kidato cha Nne hawana, kilihitimu Elimu hiyo ni majina tu), Waandishi wa Habari, Wahariri, Vyombo vya Habari na BAKITA (ambao naamini wamediwa nguvu na wako Dar tu, Mikoani hawajulikani). Ninaomba, kwa uchungu sana, kwenye watu na Taasisi wanaoongoza katika kuchefua Kiswahili, tumtaje Mh. Rais, Baraza la Mawaziri (ukiondoa Mh. Waziri Mkuu na baadhi ya Mawaziri wachache sana) na Bunge lote kwa ujumla wake, kwa kasumba zao mbaya za kuchanganya Kiswahili na Kiingereza!
Binafsi, ninapenda sana kuwasikiliza
watu kama Mwl. Nyerere (Marehemu), Dr. Salim A. Salim, Jaji Warioba, Dr. Shein, Mzee Mwinyi, Mzee Chissano, Dr. Magufuli, Dr. Mwakyembe, Dr. Migiro, Prof. Tibaijuka, Dr. Slaa, Prof. Shivj, Mh. (Dr?) Lissu na wengine wachache ambao hawalazimishi wasikilizaji wao kuwatambua kama Wasomi kwa kuchanganya Kiswahili na Kiingereza.
Umewahi kumsikiliza "Mh. Rais" wa TFF? Umewahi kuangalia na kusikiliza EATV (TV ya Vijana)?
Maneno mengine yanayo udhi kuyasikia ni kama haya:- Mdada, Mbaba, Mmama, Mkaka n.k. Mpaka hapo BAKITA, na Wahariri wa Magazeti bado wapo kimya tu.
Maneno mengine haya hapa: Noma, Kusepa, Kula nyoro, Ulabu, Kupiga chabo, Ndivyo sivyo n.k. Wahusika wenye dhamana wanaendelea 'kuchapa' usingizi.
Mimi naenda Tabola ntakaa kama li wiki li moja na ninategemea kuludi kupitia Alusha ntapumzika kama li saa limoja tu kisha ntaendedelaga na safari yangu mpaka kologwe ( Hiki ndio Kiswahili cha sasa ni upuuzi mtupu ukimsikia mtu anaongea namna hii ndio unajua sasa Kiswahili imekua lugha isiyokuwa na wakuiendeleza na BAKITA wamelala)Hali ya matumizi ya lugha ya kiswahili ilivyo sasa hasa kwa nchi ya Tanganyika, ambayo ndio inayotegemewa zaidi barani Africa kua ndio nchi inayoongea kiswahili fasaha, ipo hatarini hasa kutokana na vijana wetu wa muziki wa kizazi kipya na waandishi wetu wa habari ambao hupotosha maana na matamshi ya lugha hiyo, aidha kwa makusudi au bahati mbaya bila wahariri wa vyombo vya habari kukemea au vyombo husika kama BAKITA, na vyenginevyo kuendelea kulizibia masikio jambo hilo.
Kwa mfano ni jambo la kawaida sana, kusikia maneno kama Tupogo, hakunaga, safali, biashala n.k , yakitumika bila kukemewa.
Wachangiaji mnaweza kutoa mifano mingine.
Hali hii isipo dhibitiwa, kiswahili kitakua lugha isio nathamani tena duniani pamoja na Jamii nyingi duniani kupenda kujua na kutumia lugha yetu adhimu.
Mimi naenda Tabola ntakaa kama li wiki li moja na ninategemea kuludi kupitia Alusha ntapumzika kama li saa limoja tu kisha ntaendedelaga na safari yangu mpaka kologwe ( Hiki ndio Kiswahili cha sasa ni upuuzi mtupu ukimsikia mtu anaongea namna hii ndio unajua sasa Kiswahili imekua lugha isiyokuwa na wakuiendeleza na BAKITA wamelala)