Ubora wa Lugha ya Kiswahili " Kwishnei"

Ubora wa Lugha ya Kiswahili " Kwishnei"

Hata hizo alama za uandishi ("....." ) *funga,fungua semi*, unazoziita mabano nao ni upotoshaji upotoshaji na uharibifu wa lugha yetu.....!!

Usahihi wake ni upi, mkuu?
 
Mzimu! Kwa maoni yangu umegusa "kansa" ambayo imefikia kiwango cha kutotibika. Ninadhani tukubali matokeo kuwa Lugha yetu adhimu, Kiswahili, inapitia kipindi cha mpito kitakachopelekea kupatikana kwa Lugha nyingine kabisa, kama ambavyo Lugha yenyewe ya Kishwahili ilivyoanza.

Juzi hapa hapa JF kuna Mdau amemrekebisha Mchangiaji kuwa lugha sahihi ni "hela" na sio "ela", "halafu" na sio "alafu", "hebu" na sio "embu" n.k. na alichoambulia ni matusi. Wachangiaji ni Wasomi watarajiwa wa Nchi hii. Hiki ni Kizazi ambacho hakiwezi kuandika na kuongea lugha yoyote kwa ufasaha iwe Kiswahili au Kiingereza.

Umetaja Wadau na Makundi kadhaa yenye dhamana ya kukilinda Kiswahili yaani Wanamziki wa Mziki wa Kizazi Kipya (ambao wengi wao hata Elimu ya Kidato cha Nne hawana, kilihitimu Elimu hiyo ni majina tu), Waandishi wa Habari, Wahariri, Vyombo vya Habari na BAKITA (ambao naamini wamediwa nguvu na wako Dar tu, Mikoani hawajulikani). Ninaomba, kwa uchungu sana, kwenye watu na Taasisi wanaoongoza katika kuchefua Kiswahili, tumtaje Mh. Rais, Baraza la Mawaziri (ukiondoa Mh. Waziri Mkuu na baadhi ya Mawaziri wachache sana) na Bunge lote kwa ujumla wake, kwa kasumba zao mbaya za kuchanganya Kiswahili na Kiingereza!

Binafsi, ninapenda sana kuwasikiliza
watu kama Mwl. Nyerere (Marehemu), Dr. Salim A. Salim, Jaji Warioba, Dr. Shein, Mzee Mwinyi, Mzee Chissano, Dr. Magufuli, Dr. Mwakyembe, Dr. Migiro, Prof. Tibaijuka, Dr. Slaa, Prof. Shivj, Mh. (Dr?) Lissu na wengine wachache ambao hawalazimishi wasikilizaji wao kuwatambua kama Wasomi kwa kuchanganya Kiswahili na Kiingereza.

Umewahi kumsikiliza "Mh. Rais" wa TFF? Umewahi kuangalia na kusikiliza EATV (TV ya Vijana)?

Kuhusu Dr. Magufuli hapo umekwenda kombo. Yeye ni mtaalamu wa kuchanganya lugha ya kiingereza na kiswahili katika hotuba zake.
 
Maneno mengine yanayo udhi kuyasikia ni kama haya:- Mdada, Mbaba, Mmama, Mkaka n.k. Mpaka hapo BAKITA, na Wahariri wa Magazeti bado wapo kimya tu.

Maneno mengine haya hapa: Noma, Kusepa, Kula nyoro, Ulabu, Kupiga chabo, Ndivyo sivyo n.k. Wahusika wenye dhamana wanaendelea 'kuchapa' usingizi.
 
Maneno mengine haya hapa: Noma, Kusepa, Kula nyoro, Ulabu, Kupiga chabo, Ndivyo sivyo n.k. Wahusika wenye dhamana wanaendelea 'kuchapa' usingizi.

Lakini nadhani Neno ULABU na NDIVYO SIVYO, Ni kiswahili fasaha. Sijui kuhusu KUPIGA CHABO. Nadhani hata Neno KUPIGA CHABO, ni msemo sahihi wa Kiswahili.
 
Tena ilitakiwa hawa wasanii wa muziki na filamu wakitoa kazi mpya tu lazima kwanza zipitiwe na wataalam wa lugha ili kuboreshs lugha yetu tukufu
 
Hali ya matumizi ya lugha ya kiswahili ilivyo sasa hasa kwa nchi ya Tanganyika, ambayo ndio inayotegemewa zaidi barani Africa kua ndio nchi inayoongea kiswahili fasaha, ipo hatarini hasa kutokana na vijana wetu wa muziki wa kizazi kipya na waandishi wetu wa habari ambao hupotosha maana na matamshi ya lugha hiyo, aidha kwa makusudi au bahati mbaya bila wahariri wa vyombo vya habari kukemea au vyombo husika kama BAKITA, na vyenginevyo kuendelea kulizibia masikio jambo hilo.

Kwa mfano ni jambo la kawaida sana, kusikia maneno kama Tupogo, hakunaga, safali, biashala n.k , yakitumika bila kukemewa.

Wachangiaji mnaweza kutoa mifano mingine.

Hali hii isipo dhibitiwa, kiswahili kitakua lugha isio nathamani tena duniani pamoja na Jamii nyingi duniani kupenda kujua na kutumia lugha yetu adhimu.
Mimi naenda Tabola ntakaa kama li wiki li moja na ninategemea kuludi kupitia Alusha ntapumzika kama li saa limoja tu kisha ntaendedelaga na safari yangu mpaka kologwe ( Hiki ndio Kiswahili cha sasa ni upuuzi mtupu ukimsikia mtu anaongea namna hii ndio unajua sasa Kiswahili imekua lugha isiyokuwa na wakuiendeleza na BAKITA wamelala)
 
Mimi naenda Tabola ntakaa kama li wiki li moja na ninategemea kuludi kupitia Alusha ntapumzika kama li saa limoja tu kisha ntaendedelaga na safari yangu mpaka kologwe ( Hiki ndio Kiswahili cha sasa ni upuuzi mtupu ukimsikia mtu anaongea namna hii ndio unajua sasa Kiswahili imekua lugha isiyokuwa na wakuiendeleza na BAKITA wamelala)

Nikweli ndugu yangu. Na watu hawa sasa hivi wengi wao wamo kwenye uandishi wa habari. Na wenyewe wanadhani wapo sahihi.
 
Nakushukuru mleta mada. Ni dhahiri kuwa unaguswa vilivyo na tabia hii mbovu ya kuharibu lugha yetu iliyo tamu kinywani kama titi la mama mzazi.
Nami binafsi ninaumia katika hilo. Jambo hili kwa mawazo yangu lina mizizi kwa wadau wawili:
1. Hatuna au kuna uhaba wa walimu bora wa kufundisha watoto kusoma na
kuandika lugha hii ( hasa matamshi )
2. Tasnia ya habari hasa waandishi wengi hawana ujuzi wa lugha hii hivyo
wanakuwa wabanangaji tu.
Makundi haya mawili kama yangelikuwa na umakini katika maeneo yao nina hakika lugha yetu isingelifikia hapa ilipo. Ni aibu kuwa na watangazaji au waandishi wa habari na walimu wasio na ujuzi wa lugha yao, tena kibaya zaidi hii lugha kwa sasa ni lugha ya kwanza kwa wengi wetu!
Ushauri:
Kama kweli tunaipenda lugha hii, tutafute,tununue na tuvisome kwa wingi vitabu vya waandishi mahiri wa lugha ya Kiswahili akina Almarhum Shaaban Ufuko Robert, Profesa Abdallah Safari, Mohamed S. Abdullah na wengineo ili tujifunze msamiati halisi wa lugha hii na kuutumia mahala na wakati sahihi na si kubananga au kuchanganya lugha ovyo ovyo kama vile wewe ni mgeni na ndio umeanza kujifunza lugha hii.
Binafsi sijawahi kumuona au kumsikia raia wa bara la Ulaya tena mzungu akichanganya labda kiingereza na kifaransa wakati akiongea. Ugonjwa huu tunaumwa sisi.
Kwa walimu muwe tayari kujifunza kila wakati hasa matamshi sahihi ili watoto wetu wajifunze kutamka maneno kwa usahihi kutoka kwenu kwani wao ndio waandishi na walimu wa baadaye.
Asante mleta mada!
 
Back
Top Bottom