KERO Ubovu uliopindukia wa barabara ya kutoka Mbalizi - Songwe Viwandani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Barabara ya lami kutokea junction pale Mbalizi kuelekea Songwe viwandani ina mashimo mengi sana ambayo yamechangia kuharibu vyombo vya usafiri.

Mamlaka husika imekuwa ikiziba mashimo hayo kwa kutumia malighafi isiyokuwa na ubora, ambayo imepelekea mashimo yaliyozibwa kuibuka tena.

Lakini kuna sehemu mashimo yamezibwa kwa kujaza malighafi ya lami kupita kiwango na kufanya barabara isiwe level sawa, hii inafanya barabara ya lami iwe kama rough road kwa sababu haipo level sawa.

Tunazitaka mamlaka husika na barabara zitimize wajibu wao ipasavyo, waache kufanya kazi kwa mazoea.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…