KERO Responded Ubovu wa Barabara Kimanga, Daladala zatishia kusitisha huduma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Wakazi wa Kimanga, Dar es Salaam, wataanza kukumbana na adha ya usafiri kuanzia kesho baada ya wamiliki wa daladala zinazotoa huduma katika barabara hiyo kutishia kuanza kugoma.

Hatua hiyo imefikiwa kama njia mbadala ya kushinikiza mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kutengeneza barabara ya Kimanga ambayo imeharibika, ikiwa na mashimo hasa kuanzia Madukani hadi Mawenzi yanayojaa maji mengi kipindi hiki cha mvua.

Screenshot 2026-05-10 at 12-06-59 Instagram.png

Baadhi ya wamiliki wa daladala wamedai hali ya barabara imekuwa changamoto, kwani imekuwa ikisababisha uharibifu wa magari yao pamoja na kuhatarisha usalama wa abiria na madereva kila siku.

Si hivyo tu, baadhi yao wamedai kuwa magari yamekuwa yakikwama mara kwa mara katika barabara hiyo na kuongeza gharama za matengenezo pamoja na uendeshaji.

Hivi karibuni, Mbunge wa Segerea (Chaumma), Agnesta Kaiza, aliuliza swali bungeni kuhusu barabara za jimboni humo, ikiwemo eneo hilo ambalo limekuwa korofi, akitaka kufahamu mkakati wa Serikali ni upi.

Pia soma: KERO - Barabara ya Tabata - Kimanga kutokea Tabata Bima ina hali mbaya, Daladala nyingi zinakatisha ruti

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk Festo Dugange, alisema mvua zinazoendelea maeneo mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, zimeharibu miundombinu ya barabara na madaraja na kumwagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini (Tarura) Mkoa wa Dar es Salaam kufuatilia na kuchukua hatua.

Akizungumza na Mwananchi leo Mei 10, 2026, Katibu wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), Shifwaya Lema, amesema taarifa ya kuanza kugoma kwa wamiliki hao ameipata.

Pia soma:
~
DC Mpogolo: Kipindi cha mwezi mmoja Barabara ya Tabata Bima–Kimanga itakuwa na lami
 
Naishi Tabata ...... Kumbe Tabata Kimanga😂
 
Hii barabara ni mbovu kitambo sana. Ata ikifixiwa ni baadhi ya sehemu na anaepewa kazi hawi serious.
 
Back
Top Bottom