KERO Ubovu wa barabara Wilaya ya Temeke; Barabara kutoka Kituo cha Polisi Chang'ombe hadi Buza ina mashimo 46!

KERO Ubovu wa barabara Wilaya ya Temeke; Barabara kutoka Kituo cha Polisi Chang'ombe hadi Buza ina mashimo 46!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Bani Israel

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
1,775
Reaction score
3,593
Nisikuchoshe usinichoshe..! Wasalaam.

Mimi ni mkazi wa maeneo ya Buza ambaye katika harakati zangu kila siku usafiri wangu ni daladala kutoka Buza kwenda mjini kujitafutia mkate wa kila siku

Kero zetu kubwa huku ni usafiri na inayotunyemelea ni ya barabara kuharibika pasipo marekebisho tangu Serikali ya Magufuli ipotee kuna mambo hayako sawa upande wa Serikali zetu ndogo ndogo hata zile kubwa hapa Buza.

Kero kuu ni usafiri ila naona kabisa hali itaenda kuwa mbaya zaidi ikiwa miundombinu yetu itaendelea kuharibika bila kuwepo kwa ukarabati wa hizi barabara hasa hii yetu inayokuja Buza ina mashimo zaidi ya 46 yaliyo ndani ya barabara kutoka mataa ya Serengeti kuja hadi Buza. Mwanzo wake ni zile mvua za mwezi wa 3 ambapo Mkuu wa Mkoa aliahidi mvua zikiisha watarekebisha ila hakuna lililofanyika Mkuu wa Mkoa ametundanganya barabara zinaelekea kuwa madimbwi makubwa mvua nyingine zikija.

Eneo la Chang'ombe Polisi, Mataa kabisa mbele ya Kituo kuna shimo kubwa lipo tangu Januari ila halirekebishwi kwa viwango vya lami wanajaza tu changarawe baada ya muda shimo linarejea. Eneo la barabara ya Mwembeyanga ndio limekuwa eneo bovu kuliko yote ambapp barabara hii imearibika

Chuo cha Bandari Mwembeyanga mbele ya chuo kuna bonge la shimo liliochukua nusu ya barabara na kuendelea kuimega barabara kwa kasi. Eneo la Tandika Foma pekee lina mashimo 7 ya wastani na moja kubwa nusu ya barabara.

Davis kona eneo hili round about mashimo kama yote likifuatiwa na eneo la Chama, Mwinyi na Abiola ambapo mashimo ni mengi barabarani huku kubwa kuliko ni round about ya Kwa Mama Kibonge mashimo ambayo huwezi kuyakwepa na ni mengi pia Kwa Lulenge kuna mashimo makubwa mawili yanayochukua nusu ya barabara

Mashimo haya sio kwamba wahusika hawayaoni ila wameyavalia miwani ya mbao hii ni hatari na ni hasara kwa Serikali kuja kutengeneza barabara nzima. Nimeweka picha za eneo la round about ya Kwa Mama Kibonge kama mfano wa mashimo ambayo yanakula barabara huku serikali ikijisifia inakusanya kodi kubwa pasi na kujali watu walipakodi wanaishije.

IMG_20240711_112041_112.jpg

IMG_20240711_112043_238.jpg

IMG_20240711_112038_810.jpg

IMG_20240711_112033_030.jpg
 
Back
Top Bottom