Ubovu wa product ya Mo ukwaju

Ubovu wa product ya Mo ukwaju

Sijaona point hapa. Kwenye biashara ni kitu cha kawaida, na ndio mana kuna mtaa unaweza kupita ukakuta maduka hata kumi ya bidhaa za jumla, hata wauza maandazi mitaani wanaigana tu sembuse Mo na Bakhresa!
 
Huyu mtu sijawahi kuona ubunifu wake hata bidhaa 1. Kila kitu Azam anachofanya yeye anakuja nyuma yake anatofautisha kidogo tu ujazo au bei. Babake alijitahidi sana lakini huyu kijana naona anazingua sokoni tu.

Ameiga Ukwaju wa Azam lakini yeye ya kwake sio juisi ni ladha ya ukwaju anauza sh 300 (maalum kwa watoto) unaambiwa hata watoto wameiona hii soda ni mbaya. Sasa sijui atamuuzia nani?

Kwanini asibuni bidhaa zake mwenyewe? Atengezene hata juisi ya ubuyu basi tujue ni yake! Yupo Simba lakini naona anachuma hela tu na kujitangazia biashara zake basi lakini hana faida yeyote.
WEWE SIO MKWELI HIZI JUICE ZA UKWAJU NI NZURI KWELI NA ZINAPENDWA KWELI,MPAKA STOCK KIWANDANI ILIKWISHA KABISA MAJUZI.
:::TUACHE UONGO.
 
Nafikiri timu ya bakhressa iko vizuri sana kwa utafiti wa bidhaa na mpaka quality zao
Kila kitu kinapoingia sokoni lazima kiwe kimefanyiwa majaribio hata kwa watoto pia ili kujua wameipenda au la
Na ni gharama kubwa inatumika kabla ya bidhaa kuingia sokoni
Sasa hawa wengine business strategy zao ziko chini sana kwa kuogopa kuajiri wataalamu wa biashara
 
Poor strategy mo ajiri Watu wabunifu azam ukwaju inatishaaaaaa Angalia hata maeenerg ya mo wanywa mopombe ya ajabu ndo wanatumia tatizo Hana wabunifu wafanyakazi wenyewe kitonga Kama mashabiki WA gonga wazi
 
Kwaniii uzinzi na WEWE usilicopy kuna aliefundishwa mapenzi

Embu tulieni na NYIE wafanyakazi WA.....mmetumwaaa

Pambanenii muachane na kuajiriwa allah

#Basiasi left
kama huo uzinzi nilifanya na Ma......yako sawa!!
 
Nasikitika sijawahi na sitegemei kutumia hizo bidhaa, japo namtakia mafanikio katika kusaka pesa
 
Habari za muda huu wana bodi.

Moja kwa moja nijikite katika mada leo mchana nimepata kutumia bidhaa hii mpya sokoni kutoka kampuni ya uzalishaji wa vyakula, vinywaji na vitu vingine (inayosimamiwa na Mohamed Dewji)

BEI YA BIDHAA
Bidhaa hii mpya sokoni inaenda kwa bei ya Sh 300 tu pesa taslimu ya kitanzania hivyo kuifanya iweze kupenya ipasavyo kwa watumiaji wengi yaani watu wa market tunasema ametumia penetration pricing strategy kuifanya bidhaa yake ikubalike kwa haraka ili kutengeneza customer base kubwa ukilinganisha na bei ya Azam ukwaju inayouzwa kwa Tsh 600 kwa 500 Tsh.

BIDHAA YENYEWE
Uongo mbaya na nisiwe mnafiki katika sehemu Mo alipofeli na team yake ni katika product hii kwa 100% zipo nyingine pia japo makosa yake sio makubwa sana kama hii,kwanza kabisa ubovu wa bidhaa hii ni

1. Ladha ya bidhaa
Sijajua fomula iliyotumika kutengeneza hii kitu asee yaani haieleweki ni chungu au tamu yani ladha yake ni mbaya kiukweli haielezeki watengeneza juice na lamba lamba wa mtaani wanatengeneza vitu vizuri zaidi ya hii ya Mo mara 200.

2. Muonekano wa bidhaa
Kiukweli bidhaa ya Mo inamuonekano mbaya sana (yaani namaanisha packaging yake imekaa kilocal sana) mithili ya kinywaji pendwa cha vijana wa mtaani au wapiga debe kinachoitwa double kick hivyo kupoteza mvuto na hamu machoni kwa mtumiaji.

UBUNIFU
Kiukweli Nimekuwa insipred sana na vitu Mo anavyofanya japo huwa nakwazika sana pale ninapoona anakosa ubunifu katika bidhaa badala yake anakopi kila kitu kwa mshindani wake Azam.

Mfano: MO PASSION= AZAM JUICE/AZAM COLA, UHAI=MASAFI, AZAM ENERGY DRINK= MO ENERGY, AZAM UKWAJU = MO UKWAJU

Ila pia katika bidhaa za unga na mafuta. Kiukweli MO amekosa watu wa Business Reserch na Marketing walio na weledi wakujua kitu gani soko linaitaji badala ya kusubiri mwingine alipowekeza juhudi zake ndipo na yeye apate wigo wa kukopi watu wa biashara wanasema kwa ufupi sio mtu wa kurisk sana.

Ni mtu anaetegea mpinzani aanzishe jambo yeye aje kukopi ila pia nlitegemea akikopi ideas aje na vitu bora kuliko mshindani wake mfano COCA COLA na PEPSI badala yake jina ndilo linauza kuliko bidhaa yenyewe.

NB: Ubora wa kitu unapimwa na bei pia kwa watu wa segment fulani hivyo kuweka price ndogo sio suruhisho bali kwa watu wengine uchukulia bidhaa kuwa ni mbovu sana.

Nawasilisha wanabodi

View attachment 1249397
Hivi mbona kama Mo anamuiga sana Bakharesa ktk Bidhaa au wote n wamoja!???
 
Wewe huna akili. Hakuna mtu anaweza fanya huo ujinga. Viwanda vyote vya soda na vinywaji Tz hununua flavours nchi tofauti na kuja tengeneza syrup hapa Tz na kupack.
Muwe hata mnasoma au kutembelea youtube

Ndio maana sijawahi kukiona kiwanda cha MO
 
Hope december Mungu akipenda nta introduce kitu changu katika market since nimemaliza fanya reserch yake for six month so stay tune

Alafu kingine boss sijasema kwa nia mbaya ila ukweli umuweka mtu wazi najua atapata wasaha wakupitia mawazo ya uzi huu na atajua wapi pakurekebisha
Sina tatizo na bidhaa za Mo ila mimi ni mtu ninaependa vitu vizuri skuzote hivyo sioni aibu kusema kuwa kitu fulani nikibaya na ukweli ni kua BIDHAA HII NI MBAYA kwa mtu aliekunywa Azam ukwaju anaweza toa comment zake na ukweli ni kuwa Azam amewekeza sana na yuko na watu makini katika maswala ya food production
mo hatumii jf
 
Hyo chupa ya mo ukwaju ina ujazo wa lita ngap?
 
Back
Top Bottom