Tetesi: Ubunge 2020: Wagombea CCM lazima wawe na makazi ya kudumu majimboni!

Tetesi: Ubunge 2020: Wagombea CCM lazima wawe na makazi ya kudumu majimboni!

Nimeelezwa na kada mmoja maarufu ambaye pia ni mjumbe wa vikao mbalimbali vya CCM ya kwamba, katika uchaguzi mkuu ujao wagombea wote wa chama chao ni lazima wawe ni wakazi wenye makazi ya kudumu katika majimbo wanayogombea. Amedai ile biashara ya wakazi wa Dar na miji mingine kutimba majimboni nyakati za uchaguzi na kununua uongozi imefikia tamati. Tusubiri muda utaongea!!Mytake; Ingependeza kama utaratibu huu ungetungiwa sheria ili ivibane vyama vyote vya siasa!
Hii ingewekwa kwenye sheria za uchaguzi kabisa.
 
Nimeelezwa na kada mmoja maarufu ambaye pia ni mjumbe wa vikao mbalimbali vya CCM ya kwamba, katika uchaguzi mkuu ujao wagombea wote wa chama chao ni lazima wawe ni wakazi wenye makazi ya kudumu katika majimbo wanayogombea. Amedai ile biashara ya wakazi wa Dar na miji mingine kutimba majimboni nyakati za uchaguzi na kununua uongozi imefikia tamati. Tusubiri muda utaongea!!Mytake; Ingependeza kama utaratibu huu ungetungiwa sheria ili ivibane vyama vyote vya siasa!
WEWE UTAKUWA KUWA UNAVUNJA AMRI YA MUNGU- USIMEME UONGO
 
Nimeelezwa na kada mmoja maarufu ambaye pia ni mjumbe wa vikao mbalimbali vya CCM ya kwamba, katika uchaguzi mkuu ujao wagombea wote wa chama chao ni lazima wawe ni wakazi wenye makazi ya kudumu katika majimbo wanayogombea. Amedai ile biashara ya wakazi wa Dar na miji mingine kutimba majimboni nyakati za uchaguzi na kununua uongozi imefikia tamati. Tusubiri muda utaongea!!Mytake; Ingependeza kama utaratibu huu ungetungiwa sheria ili ivibane vyama vyote vya siasa!
SAFI SANA HATA MIMI NITAWEZA KUWA MBUNGE KATIKA JIMBO LANGU NA KUWEZA KUTOA WAZIRI KWA MARA YA KWANZA MAANA ELIMU YANGU INATOSHA NA WANANCHI WANANIELEWA SANA. STAY TUNED
 
Mkuu issue siyo ukabila ila mambo ya kumfuata mbunge Guest House linapotokea tatizo ndio CCM hawalitaki!

Kwani hakuna Ofisi ya Mbunge hadi afuatwe Guest!!! Akili za hovyo sana hizi. Ina maana Mbunge atafuatwa nyumbani kwaken.. ?? Jamani tuwe objective na tutangulize masilahi ya nchi mbele dhidi ya masilahi ya watu wachache ambao wameshajiona kuwa ni miungu watu.

Tumevunja himaya za koo za viongozi, kwa nini tunataka kujenga nyingine???
 
Muulize Msigwa kama matatizo ya wananchi anayamalizia ofisini. Mbunge makini anakuwa na ofisi ndogo kwenye makazi yake kama alivyofanya Nyerere pale msasani. Usiishi kwa kukariri!!!
 
Muulize Msigwa kama matatizo ya wananchi anayamalizia ofisini. Mbunge makini anakuwa na ofisi ndogo kwenye makazi yake kama alivyofanya Nyerere pale msasani. Usiishi kwa kukariri!!!

Usipotoshe umma, Wabunge wangapi wana ofisi nyumbani kwao wewe? Unamtolea mfano Nyerere! Kwani hakuna taratibu za namna gani mbunge afanye kazi zake jimboni??
 
Mfano mgombea wa Urais inabidi awe mzaliwa wa Dodoma yalipo makao makuu ya Nchi na ccm kwa maana ingine ukabila huenda ukarejea kwa kasi kubwa
Hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa nimecheka sana
 
Nimeelezwa na kada mmoja maarufu ambaye pia ni mjumbe wa vikao mbalimbali vya CCM ya kwamba, katika uchaguzi mkuu ujao wagombea wote wa chama chao ni lazima wawe ni wakazi wenye makazi ya kudumu katika majimbo wanayogombea. Amedai ile biashara ya wakazi wa Dar na miji mingine kutimba majimboni nyakati za uchaguzi na kununua uongozi imefikia tamati. Tusubiri muda utaongea!!Mytake; Ingependeza kama utaratibu huu ungetungiwa sheria ili ivibane vyama vyote vya siasa!
Inabidi ufafanuzi utolewe kuhusu makazi ya kudumu ni yapi?
Wengi tunajua mtu mwenye mji sehemu fulani
unaotambulika kuwa ni makazi yake na si nyumba ya
kupangisha ni mkazi wa kudumu wa eneo hilo.

Bila kujali analala kwenye nyumba hiyo
mara ngapi kwa mwaka,ilimradi anashiriki
michango na majukumu yote ya kijiji husika
anayatimiza huyu anaitwa mkazi wa kudumu.
Wengi wa wabunge wetu wanaangukia
kwenye fungu hili,sasa bila ufafanuzi zaidi
hili tamko halitakuwa na nguvu hata kidogo.
 
Nadhani watakopa kile kipengere cha ukaazi katika sheria ya uchaguzi Zanzibar! Siku hizi wapemba wa kariakoo hawaendi Pemba kugombea sheria ya ukaazi inawabana!
 
Wanachama wanaotaka kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM, sasa watalazimika kuwa wakazi wa eneo wanalotaka kuliwakilisha, sharti ambalo linaweza kuwaondoa takriban nusu ya wabunge wa sasa.

Kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuruhusu mtu kwenda sehemu yoyote apendayo, imekuwa rahisi kwa mtu kuishi mji kama Dar es Salaam na kugombea ubunge wa jimbo lililoko katika mkoa mwingine.

Na uhuru huo umewawezesha watu kama Augustine Mrema, ambaye ni mwenyekiti wa chama cha TLP, kuwa mbunge wa Moshi Vijijini kwa tiketi ya CCM, Temeke (NCCR-Mageuzi) na Vunjo (TLP).

Na ni kutokana na uhuru huo, wabunge wengi wa vyama tofauti, wanaishi Dar es Salaam na kuwakilisha majimbo ya maeneo ya asili yao.

Hata wafanyakazi kutoka serikalini, hasa wakuu wa mikoa na wilaya na sehemu nyingine, huchukua likizo wakati wa uteuzi wa wagombea na kwenda maeneo yao asilia au waliyokulia kuomba wapitishwe na wasipopitishwa hurejea makazini.

Lakini masharti mapya ya CCM yanazuia mwanachama kugombea ubunge, udiwani au nafasi nyingine yoyote bila ya kuwa mkazi wa eneo hilo.

“Shika maneno yangu, mwaka 2020 wagombea ubunge watakuwa ni wale ambao wanatoka kwenye maeneo husika, wanaojua na kushughulika na shida za wananchi,” alisema katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole katika mahojiano na kituo cha redio cha Times FM jana.

Alisema hatua hiyo imetokana na chama hicho kujitathmini na kujisahihisha baada ya kugundua watu wanataka viongozi wanaotoka miongoni mwao ambao wanajua kero zao na hivyo wataweza kuzishughulikia.

Polepole, ambaye alipata umaarufu wakati wa Bunge la Katiba akitaka litumie rasimu iliyotokana na maoni ya wananchi, alisema wanachama watakaokuwa wakazi wa maeneo tofauti na wanayotaka kuyaongoza, hawataruhusiwa.

Akihojiwa katika kipindi cha Maisha Mseto, Polepole alisema ili mwanaCCM awe na sifa za kugombea, ni lazima awe mkazi wa eneo husika.

Polepole, ambaye alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, alisema suala hilo lilikuwa sehemu ya maoni ya wananchi wakati wa mchakato wa Katiba Mpya.

Alisema msisitizo mkubwa uliopo ni cheo kimoja kwa mtu mmoja jambo linalofundisha kuwa watu wenye kiasi.

“Haya mambo ndiyo watu wanayoyataka. Rais (John) Magufuli alienda mbele zaidi kwamba utagombea nafasi ya uongozi kwenye eneo ambalo wewe ni mkazi vinginevyo, marufuku kugombea,” alisema Polepole.

“Mwaka 2020 unakuja, si mtu upo zako Times FM unapiga kazi, halafu ikifika mwishoni unaenda Ileje eti unaenda kuchukua jimbo.”

Akizungumzia uamuzi huo, katibu wa wabunge wa CCM, Jason Rweikiza alisema sharti hilo litakomesha tabia iliyojengeka kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho kwenda kugombea ubunge maeneo ambayo hawajui yana matatizo gani.

“Unakuta wananchi wana shida ya maji, umeme na barabara anakuja mgombea kipindi cha uchaguzi na ahadi kemkem, kumbe yote ni kuwavutia wampigie kura na akishajihakikishia ushindi humumuoni tena,” alisema Rweikiza.

Rweikiza alisema hatua hiyo itasababisha watu wathamini kwao na kuelewa matatizo ya maeneo waliyotoka na uchaguzi utakuwa huru bila ya rushwa.

Credit: Mwananchi,
pole.jpg

Back
Top Bottom