Tetesi: Ubunge 2020: Wagombea CCM lazima wawe na makazi ya kudumu majimboni!

Walidhani wanaoisoma mamba ni wanaukawa pekee??

Katika awamu hii ya tano kila mtu anasugua benchi!
 
Hili linatakiwa liigwe na vyama vyote au liwekwe kabisa kwenye sheria ya uchaguzi.Sababu ukiangalia sehemu kubwa ya wabunge wa vyama vyote CCM na upinzani wengi ni wakazi wa Dar es salaam wilaya ya kinondoni.Ona akina zitto kabwe,Tundu Lisu ,akina mbowe,Mbatia,NK wote wakazi wa dar ambao huenda mikoani kulaghai kisha wakipataa kura na wakipata miposho watumbulie maisha dar es salaam.

BUNGE la jamhuri ya muungano wa tanzania limejaa wabunge wakazi wa wilaya ya kinondoni dar es salaaam.Wilaya ya kinondoni ndio inaongoza tanzania nzima.Hii sio sawa.Iwekwe na itamkwe kabisa kuwa awe mkazi aliyekaa eneo husika kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo eneo hilo kabla ya kugombea.
 
Naongezea hapo;

Wakija dar waombe visa kabisa.
 
Ofisi za wabunge muda wote zimefungwa..nyingine zimeota hadi majani kama jimbo la mtama pale..watu wakiwataka wabunge wanawatafuta majumbani..sasa balaa inakuja pale anapokuwa sio mkazi..ndio msahau kabisa
 
Nakubaliana na wewe mkuu!
 
Ofisi za wabunge muda wote zimefungwa..nyingine zimeota hadi majani kama jimbo la mtama pale..watu wakiwataka wabunge wanawatafuta majumbani..sasa balaa inakuja pale anapokuwa sio mkazi..ndio msahau kabisa
Kweli mkuu unakuta wananchi wamejaa Guest house kumsubiria mheshimiwa mbunge!
 
Mawazo finyu ya Polepole. Alipobanwa kwamba sasa itakuwaje kwa maDED na maDC wanaoamua mwaka wa mwisho kwenda jimboni kugombea wakati hawajaishi pale? Majibu yake ilikuwa utumbo tu.
 
Mawazo finyu ya Polepole. Alipobanwa kwamba sasa itakuwaje kwa maDED na maDC wanaoamua mwaka wa mwisho kwenda jimboni kugombea wakati hawajaishi pale? Majibu yake ilikuwa utumbo tu.
Utumbo ndio nini?!!!!
 
Nani aunge huu ushenzi mkono?Huu ni mtamu kwa wanaccm tuu. Ktk yule Yahya wa Moshi alimwaga pesa wenye mji wakamtosa? Sio shida ya Wengie ni ya CCM?
 
Mfano mgombea wa Urais inabidi awe mzaliwa wa Dodoma yalipo makao makuu ya Nchi na ccm kwa maana ingine ukabila huenda ukarejea kwa kasi kubwa
Hivi umemuelewa kweli? Kwani kasema uwe mzaliwa wa eneo husika au UWE NA MAKAZI ENEO HUSIKA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…