Ubunge EALA, Wito Kwa CCM, Msiangalie Ukwasi, Tuteulieni, Wazalendo wa Kweli wa Taifa Hili, Wenye Uwezo na Uzoefu wa Kimataifa Kutuwakilisha Ipasavyo

Mimi naomba tu kuchukua nafasi kukupongeza kushiriki kwenye huo mchakato.

Lakini pia nikupe pole mapema kabisa! Maana uwezekano wa kupita kwenye huo mchakato, kiukweli ni mdogo sana. Na hii yote ni kwa sababu ccm ya sasa ina wenyewe! Na wewe si mmoja wao bila shaka.

Wenyewe kamwe huwezi kuwaona wakilalamika au kuingiwa na mchecheto huu wa kwako! Wenye ccm yao, huwa wanasubiri tu siku ya tukio ifike, ili wapitishwe.
 
Wewe si mgombea acha kudictate Chama, subiri upimwe kwa sifa zako
 
Ili uweze kupata nafasi hakikisha una godfather ndani ya kikao cha maamuzi, la sivyo utalia na kusaga meno.

Technically know who ndio mpango mzima CCM. Hata kama una uwezo na ushawishi kiasi gani kama huna mtu anayekujua kwenye vikao vya maamuzi ambaye atatetea jina lako basi sahau mkuu.
 
The then TANU and later CCM was the party of "HAVE NOTS" but the CCM of nowadays is party of "HAVES AND THEIR FAMILIES & FRIENDS".
Kwaiyo unapotaka kugombea Hakikisha umefanya networking na Hilo kundi la pili vinginevyo jihesabu huna nafasi kwenye Political Freemarket of CCM.
"Wakina Nape wameshasema wenye Chama chao wamerudi,wewe Mwandishi wa habari Nguli ujaelewa tu!!, Kaka Pascal unatuangusha"
 
Sasaivi tunaanza kuangalia elimu na uwezo wa mtu kiakili na kingine ni ukwasi na exposure!

Tumechoka na maskini ambao hamna lolote zaidi ya kuishi kwa nadharia za kijamaa kumbe mnataka kupiga hela tu
 
Watuletee shyrose bhanji
 
Huyu ni mzalendo asiekua na hela...πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Wazalendo wote wa Nyerere type ndivyo tulivyo. Hata Mwalimu ile nyumba ya Butiama asingejengewa na serikali, sijui ingekuwaje!. Enzi hizo kuwa na mali was a disqualifications, siku hizi, ukwasi ndio qualification No. 1.!.

P
 
Mkuu Mega Mind Nyerere, mimi ni muumini wa ukweli na uwazi, na ndicho kitu ninachokifanya ndani ya chama changu CCM, we can afford kumpitisha mgombea yoyote mwenye sifa zozote kwenye ubunge na udiwani, but not in EALA!. Tunataka CCM ishindanishe sifa na vigezo na sio mambo ya Godfather!.

Wagombea tumefika 186!, kama kila mtu atalobby na kuwa na Godfather, watapitishwa wangapi wakati nafasi za CCM ni 6 tuu?!. Kiukweli kabisa, kwenye Eala huko nyuma, tulifanya makosa, lakini EALA ya sasa inayokwenda ku implement AfCFTA, na mtanganano wa Afrika Mashariki, kiukweli kabisa, tunahitaji wawakilishi wazuri wenye elimu, sifa uwezo na exposure bila kujali mambo ya u Godfather.
Pasco
 
Mkuu tafuta pesa ndio ugombee uchaguzi ccm..

CCM wanakwenda vizuri maana hata huko Kenya hakuna maskini ameshinda uchaguzi Wala kugombea..

Maskini watakuwa kama Magufuli wataharibu kila kitu na kujisifu kwa wajinga na cheap politics.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…