Ubunge sio the Comedy; Kwako Steve Nyerere

 
safi kabisa ni ujinga kuwa na bunge la vilaza kichwana kwakwe unakuta hana article yoyote ambayo aliwa soma zaid ya mesej za kuchambana insta
 

Watu wanadharau sana, yaani kuruhusu watu kama hawa bungeni ni kudharau bunge na nchi kwa ujumla
 

Pigia mstari hapo kuanzia aya ya pili.Ndipo penye jibu kwanini watu kama Steve wanapata uthubutu wa kufikiria kwamba wanamudu kazi ya ubunge Tanzania.

Ni kwamba bunge lenyewe limeshajishusha viwango.

Kwa sasa bungeni panaonekana kama sehemu ya kupiga soga na kupitisha muda tu huku ukisubiri miaka mitano iishe upate kiinua mgongo chako.

Naamini kwa aina ya bunge letu na mijadala inayofanyika mule ndani,sio Steve tu hata msela yeyote wa mtaani anamudu kabisa kazi ya ubunge.
 
Halafu ni kwa nini tusifikirie kuwa na wabunge walio kwenye standard kama za kina Zitto, Heche na hata kina Seleli na Filikunjombe wa siku za nyuma?
 
Kunywa Maji Mwanangu sio kwa povu hilo umetoa mpaka nguo zimetakata! Ata pia umetoa ya Moyoni yanayokusumbua
 
Acha mambo ya kibwege, kila mtu ana haki ya kugombea ubunge awe tu ametimiza masharti!
 
Watu wanadharau sana, yaani kuruhusu watu kama hawa bungeni ni kudharau bunge na nchi kwa ujumla
Hakika ila tukisema wengine wanakuja juu. Fikiria, tumekuwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB) aliyepata div-0 form six na baadaye kuwa DJ kwenye kumbi za disco (bilcanas). Matokeo yake hahudhurii vikao vya kamati ya uongozi, kamati ya bajeti, n.k na kusababisha bunge na nchi kukosa uwakilishi mzuri na safu ya upinzani kudorora.

Ni wakati sasa wa kuchagua wabunge wenye upeo. Kujua kusoma na kuandika ni minimum standard ili kukidhi demokrasia za kinafiki duniani basi. Ila ukweli unajulikana bunge linahitaji wasomi na sio cereblities.
 
Ujinga ndo mtaji wa chama cha mapinduzi kuendelea kutawala...

Fikiria Bunge likiongozwa na Spika linaacha kujadili bajeti ya serikali wanaanza kujadili ulevi wa mtu...Ni sahihi hao kina Steve na Shilole waone ubunge ni kazi rahisi kwa maana kujadili watu ndo kazi zao.
 
CCM ipeleke bungeni wabunge mahiri, wenye maarifa na uwezo wa kuisaidia serikali ya chama chao kuongoza vizuri nchi.
Bungeni kusijae watu ambao hakuna linaloenda vila fitna, majungu na mambo yanayoendana na hayo. Tusidanganyane, tunahitaji wabunge ambao hata wakipewa uwaziri, watajituma kutimiza wajibu wao
 
Kazi ya kua mbunge kwa nchi hii ni kama zawadi kutoka kwa viongozi wa vyama vya siasa. Sio upinzani sio chama tawala... Wale wabunge wa viti maalum hata sijui ni wa kazi gani? Nchi hii bado kuna sehemu hatupo serious. Bunge ni chombo muhimu cha kuinyoosha serikali inapopinda, sio kushangilia na kutukana tu au kufanya fujo. Bado naiona nchi yangu ina safari ndefu sana ya kwenda kwenye uchumi wa kati
 
Huyu si ndiye wanayemtaja kuwa ni KUWADI WA MADADA wa Bongo na baadhi ya watu maarufu bongo.

Au siye?
 
Shida sio kutokusoma kwao, wanagombea ubunge kupitia chama gani?, kama ni kupitia vyama pinzani imekula kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…