Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
..kuna mwaka Mrema alitoa maneno ya kejeli kwa kabila fulani la hapa Tanzania.

..wananchi wa kabila hilo walisikitishwa sana na kauli hiyo ya Mrema.

..siku Mrema alipokwenda kuomba kura za Uraisi ktk wilaya yao, majority ya wananchi waligoma kuhudhuria mkutano wake. Mrema aliishia kupata waganga-njaa wachache.

..huo ndiyo ustaarabu ktk DEMOKRASIA. kama hukubaliani na kauli/maneno/hoja za Chama fulani basi unapaswa kuwanyima kura.

..vurugu zilizotokea Tarime ni dalili mbaya sana za hali ya kisiasa iliyopo huku.

..wale wote wenye nia njema na demokrasia yetu watanzania hawapaswi kuihalalisha hali hiyo kwa namna yoyote ile.
 
Joka Kuu,
Heshima yako mkuu,

Nakubaliana na wewe lakini tatizo watu wanaanza kupotosha kauli ya Dr.Slaa ili ionekane amehalalisha lakini infact hata yeye amesema haungi mkono hizo vurugu.Lakini kwa kuwa Dr ni member wa hapa na asiyechoka kufafanua jambo liliomuhusu yeye au Chama nadhani akipata fursa ya kuuona huu mjadala bila shaka hatasita kufafanua
 
Dr. Mvungi, pia alishawahi kupigwa na wanafunzi wa uhandisi Mlimani...again kwa kauli zake!
 
Mtanzania,
CCM wakichukua Tarime nitakupa chupa moja ya Johnny Walker (Green)
 
Tumesema mara nyingi sana siasa sio mchezo rahisi sana kama unavyoonekana, mwanasiasa mzuri ni yule anayeweza kupima upepo wa mazingara ailpo kabla ya kuongea, ndio maana tunaambiwa kwenye kitabu kimoja cha George Stephanapolus, kwamba Bill Clinton alikuwa so ggood of a politician kwamba kuna wakati walipokuwa kwenye kampeni mwaka 1992,

Alikuwa anaweza kuiangalia crowd, halafu kuamua kama hotuba aliyoandikiwa inafaa kwa ile crowd au haifai, na akiamua haifai basi huamua kutoa houtba yake mwenyewe binafsi kichwani, ili ilingane na wananchi waliopo mbele yake,

ni clear kua hawa kina Mvungi ni waganga njaa, wasioelewa kua ni majuzi tu kiongozi wa hawa wananchi amefariki katika hali ya utatanishi sana, sasa leo anapokwenda kusema maneno ya kutonesha kidonda alitegemea nini hasa?

Na what Dr. Slaa has to do with it? kwamba asiseme maoni yake kama alivyooona huko Tarime? Nani kati yetu aliyeko huko kama Dr. Slaaa? Ni chama gani cha siasa duniani kinaweza kuwa-control wafuasi wake?

Dr. Slaa heshima mbele kwa kusimamia ukweli, halafu siasa itakuja baadaye!
 
Ben,

..bora Dr.Slaa aje hapa afafanue hiyo kauli yake.

..unajua Dr.Slaa ni Mtaalamu wa Theolojia. zaidi alikuwa mtumishi wa ngazi za Juu za Kanisa Katoliki.

..sasa unaposikia anatetea na kuhalalisha vurugu na ukatili ktk kampeni za siasa inashangaza kidogo.
 
Kinachoendelea Tarime ni "Vita ya Panzi". Dhambi waliyoifanya Chadema ya kuukana ushirikiano wa vyama itai neemesha CCM.

Katika kinyang'anyiro hichi serikali isipokuwa makini maisha ya watu yatapotea na mali kuharibiwa. Finger-crossed tusifike huko
 
NCCR na TLP ni waganga njaa hao. Kwa kutokuwa na wabunge, vyanzo vyao vya mapato ni vya kubabaisha. Si ajabu wakanunuliwa na LISISIEMU. Who knows?

Mbona CHADEMA wana vyanzo vya mapato lakini yanaishia makao makuu na kulipana madeni?
hata huo uafadhali wa kupata ruzuku kwa CHADEMA, hakujawasaidia kukua(kuongeza idadi ya wanachama) zaidi ya kukimbiwa kila kukicha.

Najua wengi wetu hapa hatukubali kuona CHADEMA na viongozi wake wakikosolewa.Wakiguswa tu mnakuja juu kama vile wao ni malaika.
Hebu tuache kuwa na double standards kwa wanasiasa na vyama vyao.
Wangekuwa ni wafuasi wa CCM ndio walimshambulia Dr. Mvungi, lawama zingetiririka kama mto Mara!!

Kwa namna Dr. Slaa alivyojibu malalamiko ya Dr. Mvungi ni wazi kuwa yeye na CHADEMA wenzake wamefurahia kitendo hicho cha mashambulizi dhidi ya NCCR MAGEUZI.
Hata kama anasema haungi mkono vurugu, kusema kuwa mdomo wake umemponza ni kuwa anasherekea kimoyo moyo kupigwa kwa akina Dr. Mvungi.
Inaonekana watu mnahalalisha kuwa Tarime ni halali kwa CHADEMA, vyama vingine haviruhusiwi!!!
Basi mimi nawasubiri CHADEMA wakavamie mkutano wa CCM, kwasababu hayo aliyoyazungumza Dr. Mvungi yakawakera yatakuwa ndio kifungua kinywa katika kipindi chote cha kampeni.
 
Joka Kuu,
Heshima yako mkuu,

Nakubaliana na wewe lakini tatizo watu wanaanza kupotosha kauli ya Dr.Slaa ili ionekane amehalalisha lakini infact hata yeye amesema haungi mkono hizo vurugu.Lakini kwa kuwa Dr ni member wa hapa na asiyechoka kufafanua jambo liliomuhusu yeye au Chama nadhani akipata fursa ya kuuona huu mjadala bila shaka hatasita kufafanua
Ben na wana JF
Kwanza naomba radhi kwa muda mrefu sikuonekana kwenye jamvi. Majukumu ya mitaani yalikuwa mengi baada ya kuwa Bungeni kwa zaidi ya miezi mitatu hivi. Nimefuata mjadala kwa karibu sana. Nadhani tatizo ni kuwa wengi wame react kwenye kilichokuwa posted kwenye thread hii na hawakusoma aliyoyasema Dr. Mvungi, ambayo hajayakanusha. We need to be scientific in our approach to issues.
i) Kauli ya Dr. Mvungi niliyoijibu ilitoka kwenye TBCl, Daily News na Mtanzania ya September, 4th, 2008. Dr. Mvungi hajakanusha.
2) Dr. Mvungi ametoa pia Kauli kali dhidi ya "Chadema" kama Chama. Dr. Mvungi ni msomi aliyebobea anapaswa kujua tofauti kati ya Mashabiki, na Wanachama wa Chadema, na Chadema anayoituhumu na kutaka imwombe msamaha.
3)Dr. Mvungi amenukuliwa akisema " Chama cha Ushindani kimekiri kuwa hakitaki washindani wengine wawepo, hivyo vyama vingine vitoweke kibaki chenyewe tu na chama cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Upinzani kiitwacho CHADEMA, kimetumia hoja ya mawe badala ya kudhihirisha demokrasia". Haya ni maneno mazito, hasa yanapotoka kwa msomi. Ni hatari, na yakiachwa hivi hivi, ndiyo Taifa hili linapelekwa korongoni na wanasiasa wa aina hii. Dr. Mvungi anatakiwa atamke Chadema imekiri wapi, na kwa njia gani? na wapi? Dr. Mvungi anatakiwa aeleze umma wa Tanzania ni wapi Chadema imesema haiwataki wapinzani au vyama vingine? Wananchi wanaosoma magazeti lakini si wachambuzi wanaelewa nini? Siasa ni Sayansi na si udanganyifu ndio maana Chadema haiko tayari kuvumilia upotoshwaji wa aina hii.
4) Dr. Mvungi angekuwa mkweli angelieleza ni katika hatua ipi alipigwa mawe, na neno gani alikuwa amelitamka lililoamsha hasira ya Wananchi. Anataka kumdanganya na kumpotosha nani?
5) Kauli ya Dr. Slaa imetanguliwa na kulaani watu, wananchi wanaochukua sheria mikononi mwao na kuwa sikubaliani na mashabaki au wanachama kupiga watu. Nilichoeleza ni kuwa Dr. Mvungi akumbuke kwenye nchi jirani watu wameenda msituni kutokana na kauli za viongozi na wanasiasa. Nikakemea viongozi wote wanaotumia vibaya ndimi zao, kama Dr. Mvungi. Nikaeleza kuwa "uvumilivu una mwisho" na mtu akashawishika kuchukua hatua baada ya kuwa provoked kwa kiasi alichofanya Dr. Mvungi, asilalamike wala kumtafuta mchawi ila aulaumu ulimi wake. Haya ndiyo niliyoyasema on the basis of statements za Dr. Mvungi. Ningeweza ku analyse zaidi hotuba ya Dr. Mvungi na kutoa kasoro nyingi. Lakini kwa sasa niishie hapo. Dr. Mvungi angeliwalaumu mashabiki au watu wanaodhaniwa kuwa mashabiki mimi nisingelikuwa na tatizo sana. Lakini Chadama katika ujumla wake, ni lazima mtu yeyote makini ahoji nia nzima ya Dr. Mvungi? Ni vema JF wanaopenda kuendelea na mjadala wapate taarifa kamili ya Hotuba Dr. Mvungi na Statement ya Dr. Mvungi jana katika Press Conference.
 
Mtanzania,
CCM wakichukua Tarime nitakupa chupa moja ya Johnny Walker (Green)

Jasusi,

Upinzani wakichukua hilo jimbo mimi nitafurahi sana. msimamo wangu ni ule ule, sitaki chama kimoja kiwe na majority kama walivyo CCM sasa.

Mimi naamini akili ya mwanadamu inafanya kazi pale inapokuwa challenged. CCM wamebweteka kwasababu ya kuwa na wabunge wengi. Ndio maana mwaka 1994 nilifurahia uamuzi wa Mandela kutkubali kupika matokeo ili ANC wasishinde theluthi mbili. Afrika tungelikuwa na watu wengi kama yule mzee labda tungelipona.

Ila kwa ninayoyaona sasa huko Tarime, kweli sitashangaa CCM wakilitwaa hilo jimbo. Kuna watu wanajiita wanasiasa lakini inaelekea hawajui siasa. Wanarudia makosa yale yale kila siku.

Nitakukubusha chupa ya John MTEMBEZI, maana ahadi ni deni.
 
Mheshimiwa Dr. Slaa,

Pamoja na kukubaliana na yote uliyoyaandika hapo lakini two wrongs don't make a right.

Hao vijana kuamua kumpiga Dr. Mvungi mawe ni makosa na kiongozi yeyote wa siasa au dini lazima alaani vitendo kama hivyo.

Kama Dr. Mvungi ameongea uwongo au kuchochea vurugu, sheria zipo na inabidi zifuatwe lakini sio watu kujichukulia sheria mikononi kwa visingizio vyovyote vile.

Hivi kama umeshindwa kuwalaani hao vijana leo, utakuwa na moral authority gani kuwalaani vijana wa CCM wakiamua kuwashambulia viongozi wa CHADEMA wakihutubia?
 
Heshiama yako mh.

Pamoja na maelezo yako mazuri, jambo la msingi ni kuwa wanachama na washabiki wa CHADEMA wanawaona wagombea wa vyama vingine vya upinzani kuwa wametumwa na CCM.Na haya maneno yanzungumzwa kwa uwazi bila kificho, labda kwa wale wasiofika tarime na kusubiri magazeti tu ndio wanaweza wasikubaliane namimi.
 
Mtanzania nadhani unazungumza hisia. Una haki kuzungumzia hisia zako. Kuna kulaani mara mbili. Kama hujasoma gazeti, basi soma angalau hayo maelezo mara mbili ili uweze ku comment objectively. Usiposoma vizuri unabaki na hisia na bias tu. Kiongozi yeyote makini akiisha kulaani, anapaswa kukemea mtindo wa siasa unaotumika na viongozi wanaopotosha siasa na kuichafua mbele ya Jamii.
 
Heshiama yako mh.

Pamoja na maelezo yako mazuri, jambo la msingi ni kuwa wanachama na washabiki wa CHADEMA wanawaona wagombea wa vyama vingine vya upinzani kuwa wametumwa na CCM.Na haya maneno yanzungumzwa kwa uwazi bila kificho, labda kwa wale wasiofika tarime na kusubiri magazeti tu ndio wanaweza wasikubaliane namimi.
Mwita,
Sina tatizo kabisa na statement yako. Perception ya mitaani haitawaliwi na Chama as a matter of policy. Ugomvi wetu hapa ni kugeuzwa kwa vurugu zinazofanywa na mob ambayo hata mtu akiambiwa thibitisha ni wa chama fulani itamwia ngumu kuthibitisha. Lakini Chadema kama Chama haina policy wala ya kukataa vyama vingine, wala ya kuchochea na kupanga vurugu. Analysis ni muhimu ili kutoa comment ya uhakika. Hii haizuii kila mmoja kutoa kauli anavyofikiri, lakini inapunguza uzito.
 
Dr Slaa,

Ushirikiano wa vyama ndio m-mesha uzika rasmi? if thats the case u can just forget abt winning Tarime
 
Jasusi,

Upinzani wakichukua hilo jimbo mimi nitafurahi sana. msimamo wangu ni ule ule, sitaki chama kimoja kiwe na majority kama walivyo CCM sasa.

Mimi naamini akili ya mwanadamu inafanya kazi pale inapokuwa challenged. CCM wamebweteka kwasababu ya kuwa na wabunge wengi. Ndio maana mwaka 1994 nilifurahia uamuzi wa Mandela kutkubali kupika matokeo ili ANC wasishinde theluthi mbili. Afrika tungelikuwa na watu wengi kama yule mzee labda tungelipona.

Ila kwa ninayoyaona sasa huko Tarime, kweli sitashangaa CCM wakilitwaa hilo jimbo. Kuna watu wanajiita wanasiasa lakini inaelekea hawajui siasa. Wanarudia makosa yale yale kila siku.

Nitakukubusha chupa ya John MTEMBEZI, maana ahadi ni deni.

Mkulu hii ilinipita unaweza kue expand kidogo pls.
 
Dr Slaa,

Ushirikiano wa vyama ndio m-mesha uzika rasmi? if thats the case u can just forget abt winning Tarime
Masatu,
You do not win Tarime kwa kushirikiana na watu wanaohubiri shari.
 
Dr.Slaa,

..mimi nadhani ungelaani vurugu zilizotokea na kuviomba vyombo vya sheria vichunguze na kuchukua hatua zinazostahili.

..unapokuja hapa na kudai Dr.Mvungi alitoa "kauli fulani" zilizoibua hasira za wananchi ni kana kwamba unahalalisha kipigo alichokipewa mwanasiasa mwenzako.

..ni kana kwamba "unauma na kupuliza." yaani unacheza na akili na hisia za watu.
 
Mkulu hii ilinipita unaweza kue expand kidogo pls.

Masatu,

Hukulijua hilo? Mwaka 1994, ANC kwenye ubunge walishinda zaidi ya asilimia 66. Wengi walikuwa na wasiwasi kwamba ile katiba ambayo walijadiliana Makaburu, ANC na vyombo vingine vya dunia, ANC wangeweza kuibadili baada ya kuwa na zaidi ya theluthi mbili ya wabunge.

Kwa kifupi walipika matokeo na ANC ikashinda kwa asilimia chini kidogo tu ya 66.

Ukiwauliza watakataa lakini kwenye nyanja za kisiasa na diplomasia za dunia inajulikana ilikuwa hivyo na mzee Madiba aliruhusu hilo.

Hata mimi nilikuwa naombea ANC wasiwe na uwezo huo ili katiba yao isirudi kule kwenye katiba zingine za sisi Waafrika ambazo kwa kiasi fulani ndio mwanzo wa matatizo yetu mengi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom