Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Sauli Giliard


“NINA ndoto ya kuikomboa Wilaya ya Tarime. Naamini anahitajika mtu makini, jasiri na asiyeogopa katika kutetea ukweli ili kuibadilisha Tarime. Nimejipima na kuridhika kuwa mtu kwa wakati huu ni mimi.

“Elimu niliyo nayo kuhusu uchumi, biashara na fedha ni silaha ya kutosha ya kuwapigania Wanatarime ili maisha yao yafanane na wananchi wengine hapa nchini, kwani kiuchumi bado tuko nyuma sana”.

“…Naamini naweza kushiriki kuikomboa jamii yangu kwani ipo nyuma. Ni kama vile imetengwa, Chacha Wangwe alianza, sasa hayupo, anahitajika mtu wa aina yake na pengine zaidi yake kuendeleza yale aliyoyaanzisha. Mimi ndiye mtu huyo. Naweza kuongoza jahazi hili kuwakomboa Wanatarime”.

Hiyo ni kauli nzito ya Esther Matiko, mwanasiasa kijana na mhadhiri msaidizi katika Chuo Kikuu cha Dar er Salaam, aliyejitosa kuwania ubunge wa Tarime kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), nafasi iliyoachwa wazi na Wangwe, aliyefariki dunia mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Katika mahojiano na gazeti hili, Matiko, ambaye wakati wote alikuwa akizungumza kwa umakini wa hali ya juu huku akionekana kuchagua zaidi maneno ya kuzungumza, anasema iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Tarime, atakuwa tayari kupambana na lolote kukabiliana na kero za wananchi.

Atawatetea wananchi wa Tarime dhidi ya dhuluma ikiwamo kunyang’anywa maliasili zao. Nia yake ni kuhakikisha kuwa Wanatarime wanarejeshewa utu wao unaopotea kwa kukosa uhuru wa kunyang’anywa ardhi waliyoachiwa na babu zao.

Matiko, mwanadada pekee miongoni mwa wagombea wengine kupitia CHADEMA, alieleza kuwa ameamua kuingia katika kinyang’anyiro hicho kwa sababu anaamini wanawake nao wanaweza kugombea nafasi za uongozi na kuwashinda wanaume.

“Nina moto wa kuleta mapinduzi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika Jimbo la Tarime kupitia CHADEMA. Naamini nitaweza kwa sababu Wangwe ameacha msingi mzuri, nitaanzia hapo.

“Tarime pamoja na kuwa na madini yenye thamani, haijafanikiwa kujikwamua katika lindi la umaskini, hii ni changamoto yangu ya kwanza nikiwafanikiwa kuwa mbunge nitakakopigana kuhahakisha kuwa madini yaliyopo Tarime yatumika ipasavyo na kuwasaidia Wanatarime kujikwamua katika umaskini unaowaandama.

“Ubovu wa miundombinu, hasa barabara ni jambo jingine linaloniumiza kichwa, natamani kuona barabara za Tarime zinapitika kaktika kipindi chote cha mwaka.

“Hili litakuwa jambo jingine ambalo nitalipa kipaumbele iwapo CHADEMA itanipa ridhaa ya kuwa mgombea wake kwa sababu nina hakika nikiteuliwa, wapiga kura wa Tarime hawataniangusha, watanichagua. Ninaamini hivyo.

“Lipo pia suala la elimu, ninaifahamu Tarime ni kwetu, kodi za Wanatarime zimenisomesha na ndiyo maana ninataka kuwalipa kwa kuwatumikia kama mbunge wao. Sikubaliani na hali ilivyo katika ufundishaji katika shule za msingi na sekondari jimboni Tarime.

“Shule inakuwa na walimu wachache…hizo shule za kata na wananchi, wasichana wanakatizwa masomo kutokana na vishawishi vya aina mbalimbali,” anasisitiza.

Hakubaliani na hali ilivyo kwa wananchi wa Tarime alioeleza kuwa wanakosa uhuru wa kutembea wakiwa ndani ya ardhi waliyozaliwa, kisa kutukuza wawekezaji.

Anaeleza zaidi kuwa kodi zisizo na msingi na kilimo kisicho na tija, kwake ni changamoto ambazo amejiandaa kukabiliana nazo hadi ‘kieleweke’.

Anakiri kuwapo kwa mabadiliko ya hali ya maisha kwa wananchi wa Tarime, hasa kupitia CHADEMA kuanzisha mpango wa kuwalipia wanafunzi wote wanaofanikiwa kujiunga na elimu ya sekondari. Anaamini utawasaidia watoto wengi wa Tarime kuwapata elimu waliyokuwa wakiikosa kwa muda mrefu.

Mjue Esther Matiko

Esther Matiko alizaliwa Novemba 1976 katika Kijiji cha Nyabirongo, wilayani Tarime, akiwa mmoja wa watoto wanne wa familia ya mzee Nicholas Matiko.

Alisoma na kuhitimu elimu ya msingi katika Shule ya Kiongera kati ya mwaka 1985 na 1991. Mwaka 1992 hadi 1995 alisoma elimu ya sekondari Msalato, Dodoma.

Baadaye alisoma elimu ya juu ya sekondari kati ya mwaka 1996 na 1998 katika Shule ya Wasichana Nganza mkoani Mwanza.

Alifaulu vizuri masomo ya sayansi (Fizikia, Kemia na Baiolojia). Mwaka 1999 alichaguliwa kujiunga na Chuo Cha Kilimo cha Sokoine kuchukua shahada kwanza ya Sayansi katika fani ya Maarifa ya Nyumbani na Lishe, alihitimu mwaka 2002.

Mwaka 2003 hadi 2005 alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikosoma shahada ya Uzamili katika fani ya uongozi wa biashara akiegemea zaidi kwenye masuala ya fedha na kuhitimu mwaka 2005.

Baada ya kuhitimu, alibaki chuoni hapo katika kitengo hicho kama mhadhiri msaidizi, kazi anayoifanya hadi sasa.

Pamoja na umri mdogo alio nao, Matiko amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi - uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya Kuondoa Umaskini (TWAAP).

Alijiunga na CHADEMA mwaka 1992 akiwa mwanafunzi na kwa maneno yake mwenyewe, tangu akiwa shule ya sekondari alikuwa karibu na Wangwe kutokana na wote kuwa wakereketwa katika masuala ya siasa.

“Nakumbuka wakati wazazi wangu wakinifanyia sherehe ya kunipongeza kujiunga na Chuo Kikuu cha Sokoine, Wangwe alikuwapo na aliniusia mambo mengi…harakati zake za kupigania haki kwa Wanatarime ziliniweka karibu naye sana nami niliamini iko siku nitapata nafasi ya kuwa mwanasiasa”.

Katika uchaguzi mkuu uliopita, Matiko aligombea ubunge kwa viti maalumu kupitia CHADEMA bila mafanikio. Hata hivyo, jambo hilo halikumkatisha tamaa kwa kile alichoeleza kuwa aliamini anao muda na nafasi ya kuwa kiongozi kutokana na umri wake.

Hivi wakurya wanaweza kumchagua mwanamke!


.....ndiyohiyo
 
Hivi wakurya wanaweza kumchagua mwanamke!


.....ndiyohiyo


Hawawezi...wakurya karibu wote ninaowafahamu (nawafahamu wengi, nimekua nao..!!!) bado wana mtazamo wa kumuangalia mwanamke kuwa hawezi kuwa kiongozi.

Kwa sababu hiyo sitegemei Chadema wampitishe Esther Matiko kugombea kwa tiketi ya Chama chao. Ila naamini hii kutaka kugomea Tarime ni plan ya Esther kujiweka kwenye top ranks za Chadema ili 2010 agombee tena Viti Maalum.
 
Hawawezi...wakurya karibu wote ninaowafahamu (nawafahamu wengi, nimekua nao..!!!) bado wana mtazamo wa kumuangalia mwanamke kuwa hawezi kuwa kiongozi.

Kwa sababu hiyo sitegemei Chadema wampitishe huyu Dada kugombea kwa tiketi ya Chama chao. Ila naamini hii ni plan huyu dada kujiweka kwenye top ranks za Chadema ili 2010 agombee tena Viti Maalum.

Viti maalum Chadema vina wenyewe...
 
Masatu,Gustanza-The,Mwanakijiji,Rev.K,FMES,YeboYebo,Habari-ndiyo-hiyo,.....

..kwa kweli huyu Dada amenifurahisha na kunipa matumaini.

..kwanza hoja zake zimetulia, halafu elimu imepanda kiuhakika.

..wana-Tarime wakimchagua Esther Matiko watafuta ile dhana kwamba mwanamke hana nafasi sawa na mwanaume huko kwao.
 
Masatu,Gustanza-The,Mwanakijiji,Rev.K,FMES,YeboYebo,Habari-ndiyo-hiyo,.....

..kwa kweli huyu Dada amenifurahisha na kunipa matumaini.

..kwanza hoja zake zimetulia, halafu elimu imepanda kiuhakika.

..wana-Tarime wakimchagua Esther Matiko watafuta ile dhana kwamba mwanamke hana nafasi sawa na mwanaume huko kwao.

Well, I'd rather vote for this woman than voting for Mwita whatever anayedhani kuwa tatizo la Tarime ni ukosefu wa viongozi ambao wanaweza kushirikiana na serikali kuu.

P.S. But she need to be fully vetted kabla ya kupata endorsement yangu.
 
Hatari hatari Tarime.

Vurugu zilizomkuta Dr. Mvungi zinaashiria kitu kikubwa sana katika siasa za Tanzania.
Kwanza watanzania wanaamini kuwa upinzani ni dawa ya kutosha ya kuondoa matatizo ya watanzania.
Pili watanzania wanaamini kuwa nguvu ya upinzania iko katika kuungana. Kwa hiyo kama kukitokea lolote linaloashiria kutokuungana watanzania wanapata hisia mbaya kuwa huo utakuwa upenyo wa CCM kushinda.

Na mimi ninaamini kuwa watanzania walifarijika sana vyama vinne vilipoanzisha ushirikiano. Waliamini kuwa taratibu vyama vingine ambavyo si vya kimamluki vitajiunga. Nguvu ya vyama hivyo kwa pamoja itakuwa kubwa wanaposhirikiana katika majukwaa. Mtizamo wa wananchi kwa vyama hivyo unakuwa kwamba vyama vya upinzani sasa vinafanya siasa ya kulinda maslahi ya taifa zaidi kuliko ya vyama vyenyewe na ya watu binafsi.

DR. Mvungi Rabsha iliyokukuta katika uwanja wa Sabasaba ni ujumbe kuwa wananchi wanawataka mrudi haraka mkakae kwa kuheshimu ushirikiano wa vyama 4 muweke mgombea mmoja. Ni hakika kuwa wanaTarime wanajua chama kilicho na nguvu zaidi pale kwao. Wahojini mapema.

Dr. Mvungi wananchi wanajua mbinu zinazotumiwa na CCM kudhoofisha vita dhidi ya mafisadi. Hatua zinazochukuliwa na wananchi ni utambuzi wa heshima ya makamanda wa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ufisadi.
Chonde chonde lipeni chochote ili muiimarishe vita dhidi ya ufisadi.
 
Hawawezi...wakurya karibu wote ninaowafahamu (nawafahamu wengi, nimekua nao..!!!) bado wana mtazamo wa kumuangalia mwanamke kuwa hawezi kuwa kiongozi.

Kwa sababu hiyo sitegemei Chadema wampitishe Esther Matiko kugombea kwa tiketi ya Chama chao. Ila naamini hii kutaka kugomea Tarime ni plan ya Esther kujiweka kwenye top ranks za Chadema ili 2010 agombee tena Viti Maalum.

Viti maalumu? Labda abadili jina au aolewe na mtu wa mkoa mmoja kaskazini! kwi kwi kwi!!!
 
kushambuliwa kwa Dr. Mvungi wa NCCR huko Tarime Mara na wanaosemekana ni wafuasi wa CHADEMA Dr. Slaa amebuka na kuwaunga mkono wananchi wa Tarime kweani kauli za mvungi ndio zilimponza. Dr. Slaa amesema haungi mkono vurugu lakini uvumilivu ukifika kikomo yanaweza kutokea yaliyotokea. ameambambia Dr. Mvungi asilaani wananchi bali alaani ulimi wake
 
kushambuliwa kwa Dr. Mvungi wa NCCR huko Tarime Mara na wanaosemekana ni wafuasi wa CHADEMA Dr. Slaa amebuka na kuwaunga mkono wananchi wa Tarime kweani kauli za mvungi ndio zilimponza. Dr. Slaa amesema haungi mkono vurugu lakini uvumilivu ukifika kikomo yanaweza kutokea yaliyotokea. ameambambia Dr. Mvungi asilaani wananchi bali alaani ulimi wake

Sasa hivi imekuwa war for Tarime!Kila chama kinaona ndio wakati wake!
Jamani wapinzani sasa kama jimbo moja tuu ndilo linalowagombanisha mtaweza kweli kuungana na kuwa kitu kimoja kwenye uchaguzi mkuu?
Mnavunja watu moyo kweli ndio maana hata morale ya kuwaunga mkono inapungua watu wanaamua CCM wapete tuuuuuuuu!
 
kwa kauli hizi na yaliyomtokea Dr. Mvungi huko... nini hatma ya upinzania nchini?
 
kwa kauli hizi na yaliyomtokea Dr. Mvungi huko... nini hatma ya upinzania nchini?

Ndivyo upinzani unavyotakiwa kuwa, na sio vyama kuungana na kushindana na CCM tu
Bali kila chama kitumie jitihada zake kukishinda chama kingine chochote kilichosajiliwa
 
Kwa mtindo huu CCM itarudisha jimbo la Tarime katika himaya yake.Vita ya panzi furaha ya kunguru.
 
Ndivyo upinzani unavyotakiwa kuwa, na sio vyama kuungana na kushindana na CCM tu
Bali kila chama kitumie jitihada zake kukishinda chama kingine chochote kilichosajiliwa

That will nevr happen in TZ.Unless they unite they will never get anyway coz as they always put it "Stand Together Coz You Are Stronger United"
 
Taabu ni kuwa kuna viongozi wa upinzani ambao ni mamluki na haya yalionekana hata wakati wa msiba wa Wangwe,walipotumika kuwachafua wengine kwa kutumia kifo kile.
Sasa msiba umekwisha na watu wametulia na kutafakari nini kilitokea, Kiongozi akija na kutaka kutumia Habari ya kifo cha Wangwe(RIP) kama karata ya kupata kura anajitafutia kupigwa mawe bure.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom