Habarindiyohiyo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 263
- 16
Sauli Giliard
NINA ndoto ya kuikomboa Wilaya ya Tarime. Naamini anahitajika mtu makini, jasiri na asiyeogopa katika kutetea ukweli ili kuibadilisha Tarime. Nimejipima na kuridhika kuwa mtu kwa wakati huu ni mimi.
Elimu niliyo nayo kuhusu uchumi, biashara na fedha ni silaha ya kutosha ya kuwapigania Wanatarime ili maisha yao yafanane na wananchi wengine hapa nchini, kwani kiuchumi bado tuko nyuma sana.
Naamini naweza kushiriki kuikomboa jamii yangu kwani ipo nyuma. Ni kama vile imetengwa, Chacha Wangwe alianza, sasa hayupo, anahitajika mtu wa aina yake na pengine zaidi yake kuendeleza yale aliyoyaanzisha. Mimi ndiye mtu huyo. Naweza kuongoza jahazi hili kuwakomboa Wanatarime.
Hiyo ni kauli nzito ya Esther Matiko, mwanasiasa kijana na mhadhiri msaidizi katika Chuo Kikuu cha Dar er Salaam, aliyejitosa kuwania ubunge wa Tarime kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), nafasi iliyoachwa wazi na Wangwe, aliyefariki dunia mwezi uliopita kwa ajali ya gari.
Katika mahojiano na gazeti hili, Matiko, ambaye wakati wote alikuwa akizungumza kwa umakini wa hali ya juu huku akionekana kuchagua zaidi maneno ya kuzungumza, anasema iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Tarime, atakuwa tayari kupambana na lolote kukabiliana na kero za wananchi.
Atawatetea wananchi wa Tarime dhidi ya dhuluma ikiwamo kunyanganywa maliasili zao. Nia yake ni kuhakikisha kuwa Wanatarime wanarejeshewa utu wao unaopotea kwa kukosa uhuru wa kunyanganywa ardhi waliyoachiwa na babu zao.
Matiko, mwanadada pekee miongoni mwa wagombea wengine kupitia CHADEMA, alieleza kuwa ameamua kuingia katika kinyanganyiro hicho kwa sababu anaamini wanawake nao wanaweza kugombea nafasi za uongozi na kuwashinda wanaume.
Nina moto wa kuleta mapinduzi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika Jimbo la Tarime kupitia CHADEMA. Naamini nitaweza kwa sababu Wangwe ameacha msingi mzuri, nitaanzia hapo.
Tarime pamoja na kuwa na madini yenye thamani, haijafanikiwa kujikwamua katika lindi la umaskini, hii ni changamoto yangu ya kwanza nikiwafanikiwa kuwa mbunge nitakakopigana kuhahakisha kuwa madini yaliyopo Tarime yatumika ipasavyo na kuwasaidia Wanatarime kujikwamua katika umaskini unaowaandama.
Ubovu wa miundombinu, hasa barabara ni jambo jingine linaloniumiza kichwa, natamani kuona barabara za Tarime zinapitika kaktika kipindi chote cha mwaka.
Hili litakuwa jambo jingine ambalo nitalipa kipaumbele iwapo CHADEMA itanipa ridhaa ya kuwa mgombea wake kwa sababu nina hakika nikiteuliwa, wapiga kura wa Tarime hawataniangusha, watanichagua. Ninaamini hivyo.
Lipo pia suala la elimu, ninaifahamu Tarime ni kwetu, kodi za Wanatarime zimenisomesha na ndiyo maana ninataka kuwalipa kwa kuwatumikia kama mbunge wao. Sikubaliani na hali ilivyo katika ufundishaji katika shule za msingi na sekondari jimboni Tarime.
Shule inakuwa na walimu wachache hizo shule za kata na wananchi, wasichana wanakatizwa masomo kutokana na vishawishi vya aina mbalimbali, anasisitiza.
Hakubaliani na hali ilivyo kwa wananchi wa Tarime alioeleza kuwa wanakosa uhuru wa kutembea wakiwa ndani ya ardhi waliyozaliwa, kisa kutukuza wawekezaji.
Anaeleza zaidi kuwa kodi zisizo na msingi na kilimo kisicho na tija, kwake ni changamoto ambazo amejiandaa kukabiliana nazo hadi kieleweke.
Anakiri kuwapo kwa mabadiliko ya hali ya maisha kwa wananchi wa Tarime, hasa kupitia CHADEMA kuanzisha mpango wa kuwalipia wanafunzi wote wanaofanikiwa kujiunga na elimu ya sekondari. Anaamini utawasaidia watoto wengi wa Tarime kuwapata elimu waliyokuwa wakiikosa kwa muda mrefu.
Mjue Esther Matiko
Esther Matiko alizaliwa Novemba 1976 katika Kijiji cha Nyabirongo, wilayani Tarime, akiwa mmoja wa watoto wanne wa familia ya mzee Nicholas Matiko.
Alisoma na kuhitimu elimu ya msingi katika Shule ya Kiongera kati ya mwaka 1985 na 1991. Mwaka 1992 hadi 1995 alisoma elimu ya sekondari Msalato, Dodoma.
Baadaye alisoma elimu ya juu ya sekondari kati ya mwaka 1996 na 1998 katika Shule ya Wasichana Nganza mkoani Mwanza.
Alifaulu vizuri masomo ya sayansi (Fizikia, Kemia na Baiolojia). Mwaka 1999 alichaguliwa kujiunga na Chuo Cha Kilimo cha Sokoine kuchukua shahada kwanza ya Sayansi katika fani ya Maarifa ya Nyumbani na Lishe, alihitimu mwaka 2002.
Mwaka 2003 hadi 2005 alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikosoma shahada ya Uzamili katika fani ya uongozi wa biashara akiegemea zaidi kwenye masuala ya fedha na kuhitimu mwaka 2005.
Baada ya kuhitimu, alibaki chuoni hapo katika kitengo hicho kama mhadhiri msaidizi, kazi anayoifanya hadi sasa.
Pamoja na umri mdogo alio nao, Matiko amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi - uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya Kuondoa Umaskini (TWAAP).
Alijiunga na CHADEMA mwaka 1992 akiwa mwanafunzi na kwa maneno yake mwenyewe, tangu akiwa shule ya sekondari alikuwa karibu na Wangwe kutokana na wote kuwa wakereketwa katika masuala ya siasa.
Nakumbuka wakati wazazi wangu wakinifanyia sherehe ya kunipongeza kujiunga na Chuo Kikuu cha Sokoine, Wangwe alikuwapo na aliniusia mambo mengi harakati zake za kupigania haki kwa Wanatarime ziliniweka karibu naye sana nami niliamini iko siku nitapata nafasi ya kuwa mwanasiasa.
Katika uchaguzi mkuu uliopita, Matiko aligombea ubunge kwa viti maalumu kupitia CHADEMA bila mafanikio. Hata hivyo, jambo hilo halikumkatisha tamaa kwa kile alichoeleza kuwa aliamini anao muda na nafasi ya kuwa kiongozi kutokana na umri wake.
Hivi wakurya wanaweza kumchagua mwanamke!
.....ndiyohiyo