NCCR na TLP ni waganga njaa hao. Kwa kutokuwa na wabunge, vyanzo vyao vya mapato ni vya kubabaisha. Si ajabu wakanunuliwa na LISISIEMU. Who knows?
Ben na wana JFJoka Kuu,
Heshima yako mkuu,
Nakubaliana na wewe lakini tatizo watu wanaanza kupotosha kauli ya Dr.Slaa ili ionekane amehalalisha lakini infact hata yeye amesema haungi mkono hizo vurugu.Lakini kwa kuwa Dr ni member wa hapa na asiyechoka kufafanua jambo liliomuhusu yeye au Chama nadhani akipata fursa ya kuuona huu mjadala bila shaka hatasita kufafanua
Mtanzania,
CCM wakichukua Tarime nitakupa chupa moja ya Johnny Walker (Green)
Ben na wana JF
Kwanza naomba radhi kwa muda mrefu sikuonekana kwenye jamvi. Majukumu ya mitaani yalikuwa mengi baada ya kuwa Bungeni kwa zaidi ya miezi mitatu hivi. Nimefuata mjadala kwa karibu sana. Nadhani tatizo ni kuwa wengi wame react kwenye kilichokuwa posted kwenye thread hii na hawakusoma aliyoyasema Dr. Mvungi, ambayo hajayakanusha. We need to be scientific in our approach to issues.
i) Kauli ya Dr. Mvungi niliyoijibu ilitoka kwenye TBCl, Daily News na Mtanzania ya September, 4th, 2008. Dr. Mvungi hajakanusha.
2) Dr. Mvungi ametoa pia Kauli kali dhidi ya "Chadema" kama Chama. Dr. Mvungi ni msomi aliyebobea anapaswa kujua tofauti kati ya Mashabiki, na Wanachama wa Chadema, na Chadema anayoituhumu na kutaka imwombe msamaha.
3)Dr. Mvungi amenukuliwa akisema " Chama cha Ushindani kimekiri kuwa hakitaki washindani wengine wawepo, hivyo vyama vingine vitoweke kibaki chenyewe tu na chama cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Upinzani kiitwacho CHADEMA, kimetumia hoja ya mawe badala ya kudhihirisha demokrasia". Haya ni maneno mazito, hasa yanapotoka kwa msomi. Ni hatari, na yakiachwa hivi hivi, ndiyo Taifa hili linapelekwa korongoni na wanasiasa wa aina hii. Dr. Mvungi anatakiwa atamke Chadema imekiri wapi, na kwa njia gani? na wapi? Dr. Mvungi anatakiwa aeleze umma wa Tanzania ni wapi Chadema imesema haiwataki wapinzani au vyama vingine? Wananchi wanaosoma magazeti lakini si wachambuzi wanaelewa nini? Siasa ni Sayansi na si udanganyifu ndio maana Chadema haiko tayari kuvumilia upotoshwaji wa aina hii.
4) Dr. Mvungi angekuwa mkweli angelieleza ni katika hatua ipi alipigwa mawe, na neno gani alikuwa amelitamka lililoamsha hasira ya Wananchi. Anataka kumdanganya na kumpotosha nani?
5) Kauli ya Dr. Slaa imetanguliwa na kulaani watu, wananchi wanaochukua sheria mikononi mwao na kuwa sikubaliani na mashabaki au wanachama kupiga watu. Nilichoeleza ni kuwa Dr. Mvungi akumbuke kwenye nchi jirani watu wameenda msituni kutokana na kauli za viongozi na wanasiasa. Nikakemea viongozi wote wanaotumia vibaya ndimi zao, kama Dr. Mvungi. Nikaeleza kuwa "uvumilivu una mwisho" na mtu akashawishika kuchukua hatua baada ya kuwa provoked kwa kiasi alichofanya Dr. Mvungi, asilalamike wala kumtafuta mchawi ila aulaumu ulimi wake. Haya ndiyo niliyoyasema on the basis of statements za Dr. Mvungi. Ningeweza ku analyse zaidi hotuba ya Dr. Mvungi na kutoa kasoro nyingi. Lakini kwa sasa niishie hapo. Dr. Mvungi angeliwalaumu mashabiki au watu wanaodhaniwa kuwa mashabiki mimi nisingelikuwa na tatizo sana. Lakini Chadama katika ujumla wake, ni lazima mtu yeyote makini ahoji nia nzima ya Dr. Mvungi? Ni vema JF wanaopenda kuendelea na mjadala wapate taarifa kamili ya Hotuba Dr. Mvungi na Statement ya Dr. Mvungi jana katika Press Conference.
Heshiama yako mh.Ben na wana JF

Mtanzania nadhani unazungumza hisia. Una haki kuzungumzia hisia zako. Kuna kulaani mara mbili. Kama hujasoma gazeti, basi soma angalau hayo maelezo mara mbili ili uweze ku comment objectively. Usiposoma vizuri unabaki na hisia na bias tu. Kiongozi yeyote makini akiisha kulaani, anapaswa kukemea mtindo wa siasa unaotumika na viongozi wanaopotosha siasa na kuichafua mbele ya Jamii.Mheshimiwa Dr. Slaa,
Pamoja na kukubaliana na yote uliyoyaandika hapo lakini two wrongs don't make a right.
Hao vijana kuamua kumpiga Dr. Mvungi mawe ni makosa na kiongozi yeyote wa siasa au dini lazima alaani vitendo kama hivyo.
Kama Dr. Mvungi ameongea uwongo au kuchochea vurugu, sheria zipo na inabidi zifuatwe lakini sio watu kujichukulia sheria mikononi kwa visingizio vyovyote vile.
Hivi kama umeshindwa kuwalaani hao vijana leo, utakuwa na moral authority gani kuwalaani vijana wa CCM wakiamua kuwashambulia viongozi wa CHADEMA wakihutubia?
Mwita,Heshiama yako mh.
Pamoja na maelezo yako mazuri, jambo la msingi ni kuwa wanachama na washabiki wa CHADEMA wanawaona wagombea wa vyama vingine vya upinzani kuwa wametumwa na CCM.Na haya maneno yanzungumzwa kwa uwazi bila kificho, labda kwa wale wasiofika tarime na kusubiri magazeti tu ndio wanaweza wasikubaliane namimi.
Mwita,
Sina tatizo kabisa na statement yako. Perception ya mitaani haitawaliwi na Chama as a matter of policy. Ugomvi wetu hapa ni kugeuzwa kwa vurugu zinazofanywa na mob ambayo hata mtu akiambiwa thibitisha ni wa chama fulani itamwia ngumu kuthibitisha. Lakini Chadema kama Chama haina policy wala ya kukataa vyama vingine, wala ya kuchochea na kupanga vurugu. Analysis ni muhimu ili kutoa comment ya uhakika. Hii haizuii kila mmoja kutoa kauli anavyofikiri, lakini inapunguza uzito.
Jasusi,
Upinzani wakichukua hilo jimbo mimi nitafurahi sana. msimamo wangu ni ule ule, sitaki chama kimoja kiwe na majority kama walivyo CCM sasa.
Mimi naamini akili ya mwanadamu inafanya kazi pale inapokuwa challenged. CCM wamebweteka kwasababu ya kuwa na wabunge wengi. Ndio maana mwaka 1994 nilifurahia uamuzi wa Mandela kutkubali kupika matokeo ili ANC wasishinde theluthi mbili. Afrika tungelikuwa na watu wengi kama yule mzee labda tungelipona.
Ila kwa ninayoyaona sasa huko Tarime, kweli sitashangaa CCM wakilitwaa hilo jimbo. Kuna watu wanajiita wanasiasa lakini inaelekea hawajui siasa. Wanarudia makosa yale yale kila siku.
Nitakukubusha chupa ya John MTEMBEZI, maana ahadi ni deni.
Masatu,Dr Slaa,
Ushirikiano wa vyama ndio m-mesha uzika rasmi? if thats the case u can just forget abt winning Tarime
Masatu,
You do not win Tarime kwa kushirikiana na watu wanaohubiri shari.
Mkulu hii ilinipita unaweza kue expand kidogo pls.