Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Poti
wewe ndio una miss point ya mtanzania

ya kwamba kwanini mapigano yawepo?? Na utahubiri vipi demokrasia kwa wanakijiji wakati wewe ndani mwako kila siku mnachomana visu wewe na mkeo na watoto wenu??

Bado hatujakubaliana na Mtanzania kama mapigano yapo Tarime au ni uzushi tu kama ule uliowekwa hapa wakati wa mazishi ya Wangwe.

Tujifunze kuukubali ukweli .
Niemkuulizeni mbona kwenye maandamano ya amani hua kumejazana askari ??ulishawahi kuhoji hilo?

Ukweli upi huo? kama polisi wangekuja kwa ajili ya maandamano ya amani basi wangesema hivyo na sio kusema kuwa wamekuja "kutuliza fujo" ambazo huwa zinatokea wakati wa uchaguzi tu.

yeyote anayelata vurugu huko home lazima police wa deal naye perpendicularly na aadhibiwe vigorously.

Yalishatokea Pemba, Kiteto, na Dar es salaam. Sidhani kama hii itakuwa ni mara ya kwanza. Kama wewe unafurahia hili hiyo ni juu yako.
 
Magabe,

Ulichoandika ndicho hata mimi nimeandika hapo juu kwamba labda tofauti ni kwamba wakati wa Mwalimu, polisi walikuwa wanatumwa mara moja kwenda kutuliza wakati sasa hakuna anayejali.

Mtu akisema hivyo nitamwelewa lakini sio kusema wakati wa Mwalimu mapigano hayakuweko eti kulikuwa na wizi wa ng'ombe tu. Jamani tuwe wakweli vinginevyo wote tunajiingiza kwenye propaganda za akina RA.

Mtanzania,

naona umeamua kumwekea maneno Jasusi, alichosema jasusi ni hiki hapa:

Jasusi said:
Mtanzania,
Mimi naijua Tarime. It has nothing to do with CCM kubanwa, ila there is a leadership void that is being exploited by the 2 koos. Ndio maana nimeuliza mbona enzi za Mwalimu hukusikia uhasama wa aina hii? Mwalimu knew how to deal with it and he did. Waulize Wanatarime.

Amesema kuwa Mwalimu alijua namna ya kudeal with it. Sioni kama amesema kuwa hayakutokea. Kama alivyoandika tena hapa:

Jasusi said:
Mkamap,
Hapana. Enzi za Mwalimu alikuwa akipeleka FFU kule na kuzima wizi wa ng'ombe. There was law and order na Wakurya walijua mbele ya Nyerere hakuna mchezo. Hiyo ya Wamasai ni tofauti. Mimi nililenga wizi wa ng'ombe baina ya Wakurya kwa Wakurya wa koo mbalimbali.

waandishi wa habari wanaosema Tarime watu wanachinjana wanasema kuwa sababu ni wizi wa ngombe, kama wewe unataka kutenganisha wizi wa ngombe na mapigano na wakati ukisema kuwa mengine yote ni propaganda za RA, jibu lako linachanganya zaidi kuliko kufafanua position yako.
 
Wanchori ni kina nani tena?

Kwi kwi kwi, poti, wajita watapigana na wamasai kwa ajili ya nini? pamba au samaki?

Back to the issue, mimi ndiye nilimuuliza mtanzania swali la mapigano yameanza lini. Kama hana jibu anaweza kusema tu.

Poti.
teh teh teh teh
Sasa ni akina nani wanapigana na wamasai na kwa sababu zipi? umewataja wajita na JINSWI(samaki) sasa ni akina nani wanapigana na kwa sababu zipi?
 
Poti.
teh teh teh teh
Sasa ni akina nani wanapigana na wamasai na kwa sababu zipi? umewataja wajita na JINSWI(samaki) sasa ni akina nani wanapigana na kwa sababu zipi?

poti,

last time I checked, wajita na wakurya walikuwa wanatenganishwa na mto ambao makampuni ya madini yanachangia kuuchafua kila siku kwa sumu mbaya sana huku wakijua kuwa maji yake yanaelekea ziwa victoria (mto mara).
 
Mkuu Jasusi,

Mimi nimesikia mapigano ya kiukoo na kikabila Tarime tokea miaka ya Nyerere. Tena wakati huo tuna radio moja tu na control kubwa ya serikali. Labda uniambie RTD nao walikuwa wamenunuliwa RA, walikuwa wanatangaza propaganda.

Ila kusema wakati wa mwalimu hayo mapigano hayakuwepo ni uongo wa mchana, sorry nitarudia tena kusema ni uongo maana siamini mtu kama Jasusi unaweza kusema hayo mapigano hayakuwepo. Sio kweli hata wakati wa Nyerere yalikuwepo. Labda kilichotofauti ni wakati wa Nyerere polisi walikuwa wanaenda kushughulikia wakati sasa who cares? Kama baadhi ya wana Tarime wenyewe wanasema mapigano hayapo, hata CCM wanaweza kusema mapigano hayapo, kwanini wakahangaike kuyamaliza?

Miaka ya 80 watu tulikuwa secondary schools tena tukiwa active kwenye siasa na kusikiliza RTD kila siku. Sasa mtu unapokuja na uongo kama huo kwamba wakati wa Nyerere mapigano hayo hayakuwepo, ninajiuliza unataka kumdanganya nani?

Mtanzania,
Sikusema hayakuwepo. Kama yasingekuwepo kusingekuwa na haja ya Mwalimu kupeleka FFU kule. Nilisema hakukuwepo leadership vacuum.
Watarime walimwelewa na kumwogopa sana Mwalimu. Na Wakurya wanaheshimu sana authority. Kinachokosekana sasa ni hiyo authority, au CCM wameamua kuitumia kwa hila zao. Kwa hiyo haukuwa na sababu za kutumia lugha za "unataka kumdanganya nani." Siko hapa kudanganya hata siku moja. Enzi za Mwalimu wizi wa ng'ombe Tarime ulipungua sana, actually uliisha baina ya koo na koo.
 
poti,

last time I checked, wajita na wakurya walikuwa wanatenganishwa na mto ambao makampuni ya madini yanachangia kuuchafua kila siku kwa sumu mbaya sana huku wakijua kuwa maji yake yanaelekea ziwa victoria (mto mara).

teh teh teh
poti
Twende kwenye pointi naomba uwaambie hadhira humu ndani kua hizo nyumba zilizochomwa ni CCM kushirikiana na FFU.

Poti narudia tena.
Kamanda mzuri wa polisi hutuma vijana wake sehemu ambapo kuna sign ya usalama kua mdogo.

Harafu watu wanatuambia kua FFU wapo Tarime mjini tu kwa hiyo ina maana ccm wakiiba kura za hapo mjini wanakua wameshajihakikishia ushidi tayari??
 
Jasusi,

Maandishi yako kwa MkamaP umeandika HAPANA aliposema mapigano yalikuwepo hata wakati wa Nyerere. Ulichoandika sasa hapo juu ndio sahihi.

Binafsi nilishutushwe na maandishi yako hayo maana najua toka enze za Nyerere ulikuwa
sehemu ambayo usingelikosa kujua kwamba hayo mapigano yalikuwepo.

Binafsi napinga mapigano yoyote ya wananchi whether ni Kyela au Tarime. Nchi maskini hatuwezi kuendelea kupoteza hata resources ndogo tulizo nazo kwa kuchomeana moto au kuuana. Ni kweli serikali ina wajibu mkubwa, lakini hata sisi wananchi tuna wajibu wa kuondokana na ujinga huo.
 
poti,

last time I checked, wajita na wakurya walikuwa wanatenganishwa na mto ambao makampuni ya madini yanachangia kuuchafua kila siku kwa sumu mbaya sana huku wakijua kuwa maji yake yanaelekea ziwa victoria (mto mara).

Magabe Kibiti,
Ni sumu gani hiyo mbaya kiasi hicho? Imeshaua au kujeruhi wangapi? Hili jambo linaelekea ni muhimu sana kwa uchaguzi, hebu mwaga data.
 
teh teh teh
poti
Twende kwenye pointi naomba uwaambie hadhira humu ndani kua hizo nyumba zilizochomwa ni CCM kushirikiana na FFU.

Kama unakumbuka vizuri, sio mimi niliyesema kuwa nyumba zimechomwa. Nadhani unatakiwa kumuuliza aliyeleta hii habari hapa - Mtanzania?- maana hata mimi nina maswali ambayo hajayajibu.

Poti narudia tena.
Kamanda mzuri wa polisi hutuma vijana wake sehemu ambapo kuna sign ya usalama kua mdogo.

Kamanda mzuri wa polisi si yule anayesubiri miaka mitano kupeleka polisi wake "kutuliza fujo" ambazo zimekuwa "zinaendelea kwa miaka yote".

Harafu watu wanatuambia kua FFU wapo Tarime mjini tu kwa hiyo ina maana ccm wakiiba kura za hapo mjini wanakua wameshajihakikishia ushidi tayari??

Naona umeanza kuchanganya R na L kama kawaida yako. Vuta pumzi mkuu! kwi kwi kwi kwi
 
Magabe Kibiti,
Ni sumu gani hiyo mbaya kiasi hicho? Imeshaua au kujeruhi wangapi? Hili jambo linaelekea ni muhimu sana kwa uchaguzi, hebu mwaga data.

Angalau sasa hivi umerudi kwenye kujadili issues muhimu kwa taifa. Nitasubiri kwanza kuona muelekeo wako hapa (maana hukawii kuanza kugeuza kila kitu hapa kuwa anti-CHADEMA na anti - JF) kabla sijaanza kujadili hili jambo ambalo lilijadiliwa sana wakati wa msiba wa Wangwe hapa JF.

Subira huvuta heri.
 
Poti R na L lisikupe tatizo.

tunarudi kwenye pointi ya Mtanzania
Kwanini mapigano hayo yawepo na tena sisi kwa sisi? Huo ni UJUHA Mkubwa poti wangu

tutawezaje kusema tunajua DEMOKRASIA na tunauelewa wa hali ya juu wakati tunapigana na kuuana sisi kwa sisi? hiyo demokrasia tumeshindwa kuitumia majumbani kwetu??

NB naomba hili usinipe jibu wala usilijadili.
Watu wameshaanza kupotosha UMMA kwa kuaminisha watu ya kwamba anayechagua UPINZANI ndiye anayejua DEMOKRASIA na MDEMOKRASIA wa kweli .HII ni FALSAFA MFU.
MDEMOKRASIA ni yule anaye uziwa SERA KABABE na yeye ikamwingia akaipenda AKAINUNUA SERA hiyo kwa kumpa kura muuza SERA.
 
Popote pale Tanzania ambapo CCM huwa inabanwa kwenye uchaguzi hutokea fujo, tena fujo kubwa, na fujo zote hizi hufanywa na polisi kwa maelekezo ya CCM. CCM wataingiza hii nchi kwenye maafa. Kama hawapo tayari kwa ushindani wa kistaraabu wangefuta mfumo wa vyama vingi kulikoni kuendelea kuwadanganya watu.

Mkuu Kitila,

Hapa usemi wako hauna tofauti na mtu wa kijiweni. Sidhani kama unaweza kuuhakiki.
  1. Una ushahidi gani kuwa kila mahali CCM walipokuta ushindani walianzisha vurugu?
  2. Hivi kunapokuwepo na vurugu hao CCM inawasaidiaje kushinda uchaguzi?
  3. Kuna mtu yeyote humu mtandaoni aliyevutiwa na CCM na kuwapigia kura kutokana na kushuhudia vurugu zao?
Hebu waungwana tuachane na maneno ya magengeni na kutumia vichwa vyetu. Ni muhimu kwa waTZ kueleweshwa jinsi ya kupigania haki zao bila kuzua vurugu. Hiyo ndio demokrasia.
 
Poti R na L lisikupe tatizo.

tunarudi kwenye pointi ya Mtanzania
Kwanini mapigano hayo yawepo na tena sisi kwa sisi? Huo ni UJUHA Mkubwa poti wangu

tutawezaje kusema tunajua DEMOKRASIA na tunauelewa wa hali ya juu wakati tunapigana na kuuana sisi kwa sisi? hiyo demokrasia tumeshindwa kuitumia majumbani kwetu??

Hili swali ni ambalo nimeliuliza pia hapa. Wakati wa msiba wa Wangwe media nyingi Tanzania zilisema kuwa Tarime kutawaka moto na hata wengine wakasema kuwa kuna mapigano makubwa yanatokea - kitu ambacho baadaye kilionekana kuwa ni uongo.

Una hakika kuwa kuna mapigano Tarime au nawewe unasoma habari za magazetini?

NB naomba hili usinipe jibu wala usilijadili.
Watu wameshaanza kupotosha UMMA kwa kuaminisha watu ya kwamba anayechagua UPINZANI ndiye anayejua DEMOKRASIA na MDEMOKRASIA wa kweli .HII ni FALSAFA MFU.
MDEMOKRASIA ni yule anaye uziwa SERA KABABE na yeye ikamwingia akaipenda AKAINUNUA SERA hiyo kwa kumpa kura muuza SERA.

Naona sasa unataka kunichagulia cha kujadili hapa na wakati huo huo ukitoa somo la demokrasia ya kweli. Unashangaza kweli poti.
 
Angalau sasa hivi umerudi kwenye kujadili issues muhimu kwa taifa. Nitasubiri kwanza kuona muelekeo wako hapa (maana hukawii kuanza kugeuza kila kitu hapa kuwa anti-CHADEMA na anti - JF) kabla sijaanza kujadili hili jambo ambalo lilijadiliwa sana wakati wa msiba wa Wangwe hapa JF.

Subira huvuta heri.

Magabe,
Usiogope kuwa challenged. Kama unayoongea sio uzushi basi tupatie data za hiyo sumu kutoka migodini, maana nimeona kila uandikacho unaishurutishia hiyo sumu kuwa ndio tatizo kubwa la wanaTarime. Lau kama huna data, ni vema ukaongelea mambo mengine na kuacha kulalamikia jambo usilolijua.
 
Sidhani kama ninaogopa kuwa challenged mkuu, ninataka tu kuwa na hakika kuwa uko makini sasa hivi na sio kuanza kuleta habari za Mtikila na uzushi mwingine kama ulivyofanya last time (maana hapo juu nimeona ukibisha kuwa fujo hutokea wakati wa chaguzi Tanzania - Dar, Pemba, Kiteto, na sasa hivi kuna "hizi fujo" za Tarime ambazo zinahitaji mamia ya polisi kuzituliza).

Ukiwa tayari kwenye hilo niambie tu nitaanza dozi moja baada ya nyingine.
 
mambo yalivyo:

1222150687_ffuweb.jpg

Hivi kati ya mabloga wetu wote hakuna aliyekwenda Tarime?

Mbona watu wame-relax kiasi hiki, mpaka mikono mifukoni, au hao pichani ni makada wa CCM na polisi tu? Hakuna mwenye picha inayoonyesha wanaCHADEMA wanavyoonewa na dola?? Data za Mnyika za hao CHADEMA 50 walioonewa na polisi ziko wapi au ulikuwa ni uzushi tu??
 
Labda tumsubiri Lyunyungu, nikitumaini kuwa anayo cell phone yenye camera.
 
Sidhani kama ninaogopa kuwa challenged mkuu, ninataka tu kuwa na hakika kuwa uko makini sasa hivi na sio kuanza kuleta habari za Mtikila na uzushi mwingine kama ulivyofanya last time (maana hapo juu nimeona ukibisha kuwa fujo hutokea wakati wa chaguzi Tanzania - Dar, Pemba, Kiteto, na sasa hivi kuna "hizi fujo" za Tarime ambazo zinahitaji mamia ya polisi kuzituliza).

Ukiwa tayari kwenye hilo niambie tu nitaanza dozi moja baada ya nyingine.

Magabe,
Achana na hizo sababu za kitoto za oo juzi ilikuwa hivi na mwaka jana ilikuwa vile. Humu kila kitu kinajadiliwa iwe ni muhogo, sidiria, Mtikila, Tarime n.k., n.k. Kama yamekushinda usisingizie hoja nyingine. Kila posting na hoja zake na hujibiwa kama sio upupu.

Hapa unachotakiwa ni very simple, tufahamishe data za hiyo sumu uliyoilalamikia kwenye postings zako kibao kwa kiasi tu unachoweza. Sasa kama huna data, basi ueleze umma wa JF kuwa ulikuwa unababaisha na hatutaka tukusikie tena na hiyo sababu ya sumu ya migodini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom