Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Mtanzania,
Badala ya kulaumu victims lawama zako ungezielekeza kwa dola. Polisi na FFU waliomwagwa Tarime wako wapi kuhakikisha uhasama wa aina hii haufanyiki? Wenyewe wamejibanza Tarime mjini tu kuwabana wana Chadema wasifanye mikutano yao. Hebu jiulize mbona enzi za Mwalimu hatukusikia uhasama huu wa kikabila? Leo chini ya CCM kuna lawlessness ambayo dola imeshindwa(makusudi) kuidhibiti.

Mkuu Jasusi,

Sikubaliani kabisa na hoja yako kwamba hao wanaochinjana na kwenda kuibiana ni victims.

Wala sio mmoja wa watu ambao wanaona serikali lazima itufanyie kila kitu. Ninatimiza wajibu wangu kwanza na kisha kuilaumu serikali kwa kushindwa kutimiza wajibu wao.

Kama kuna lawlessness ambayo imeletwa na CCM kwanini sehemu zingine watu hawachinjani?

Ujinga ndio unawafanya CCM watanue na ili kufuta ujinga huo ni pamoja na kuondoa huo ujinga wa kuchinjana bila sababu.
 
Hii lawlessness ilisemwa sana kuwa itatokea kwenye mazishi ya Wangwe na badala yake mambo yakawa tofauti kabisa. Huku kuchinjana nako kulisemwa sana na magazeti ya Rostam lakini hakukutokea.

Leo hii uchaguzi umekaribia na ili kuhalalisha sababu ya kuwa na mamia ya polisi Tarime, habari za "kuchinjana" zimeanza tena kutokea mtandaoni na magazetini.

Inatisha kwelikweli.
 
Mtanzania,
Mimi naijua Tarime. It has nothing to do with CCM kubanwa, ila there is a leadership void that is being exploited by the 2 koos. Ndio maana nimeuliza mbona enzi za Mwalimu hukusikia uhasama wa aina hii? Mwalimu knew how to deal with it and he did. Waulize Wanatarime.

Huijui Tarime ama Meatu.

Enzi za mwalimu mapigano yalikuwepo ILA kwa nini hayakusikika ni kwa sababu kulikua hakuna simu TV kulikuwepo RADIO TZ tu ililipoti waliyopenda.

NAkuhakikishia miaka hiyo nilishuhudia mapambano makali kati yetu na wamasai na tukafanikishia kumyang'anya ROHO mmasai mmoja na tulikua tunajisifu sana kama tumeua kasimba fulani.
 
Date::9/23/2008
Makamu mwenyekiti CCM aomba nguvu ya dola kudhibiti upinzani
Frederick Katulanda, Tarime
Mwananchi

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Mskekwa, amesema atawasiliana na Rais Jakaya Kikwete ili amwagize Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Mstaafu Isaac Machibya, aruhusu nguvu zaidi ya dola itumike kuwadhibiti wanachama wa Chama cha Demokrasia (Chadema), aliyodai kuwa wanafanya fujo.

Akizungumza jana wakati wa kumnadi mgombe udiwani wa CCM Tarime mjini, Peter Zacharia, Msekwa, alisema atamweleza Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM amwamuru Kanali Machibya awaamuru polisi kutumia nguvu ya ziada katika kubilina na hali hiyo wakati huu wa kampeni za kuwania kiti cha ubunge wa Tarime.

"Wanatufanyia fujo, jana mfuasi wetu, Rubeni Marwa, alijeruhiwa kwa mawe na amekatika kidole na mwingine, Omari Nzungu, leo hii amemwagiwa pilipili machoni. Sasa hizi ni vurugu hatuwezi kuendela kuvumilia, nitamwambia Rais leo hii, hivyo yatakayo tokea shauri yenu," alisema Msekwa wakati akihutubia mkutano huo wa kampeni.

Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya siasa ambao wamezungumza na gazeti hili baada ya kauli hiyo ya Msekwa, walionya kuwa kama Rais atapokea taarifa hiyo na kuamuru Jeshi la Polisi kutumia nguvu, hali ya usalama Tarime inaweza kuchafuka zaidi.

Walisema eneo hilo linaweza kugeuka uwanja wa vita kutokana na msimamo wa wananchi wa wilaya Tarime ambao wamekuwa wakiishi kwa mapigano ya koo kwa kwa muda mrefu.

Dalili za kuwapo kwa vurugu, zilianza kuonekana tangu kuanza kwa kampeni hizo na hasa baada ya kuwasili kwa viongozi wa ngazi za juu wa CCM ambao walipkewa kwa kuzomewa wakati wanaingia mjini Tarime.

Hata hivyo vurugu ziliibuka zaidi mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya wafuasi wa Chadema kukerwa na vitendo vya viongozi wa CCM kuwakikejeli chma chao kwa kukiita kuwa ni cha watu wawili.

Hata hivyo, juzi jioni wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM ambapo kada mmoja wa chama hicho, alimwagiwa pilipili na kijana ambaye anayedaiwa kuwa mfuasi wa chadema, kulisababishwa na viongozi wa CCM kuanza kuishambulia chadema kwa maneno hivyo kuamsha hasira za wananchi hao ambao walianza kuzomea.

Vurugu zilizuka baada ya askari polisi kumshika kijana huyo na kutak kumpeleka kituoni ndipo wafuasi Chadema waliwasonga wakiwataka wamwachie mwenzo huku wakirusha mawe mpaka alipoachiwa.

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa CCM, Luteni Yusuph Makamba, aliwataka wananchi hao kutomchagua mgombea wa Chadema, kwa madai kuwa chama hicho hakina bajeti ya kuendeshea nchi, hivyo hawatapata maendeleo haraka.

Tangu kuanza kwa kampeni huizo kumekuwapo msuguano mkali kati ya wafuasi wa CCM na Chadema.
 
Acha uongo wewe poti, lini wajita wakapigana na wamasai? kwi kwi kwi
 
Mkamap,
Hapana. Enzi za Mwalimu alikuwa akipeleka FFU kule na kuzima wizi wa ng'ombe. There was law and order na Wakurya walijua mbele ya Nyerere hakuna mchezo. Hiyo ya Wamasai ni tofauti. Mimi nililenga wizi wa ng'ombe baina ya Wakurya kwa Wakurya wa koo mbalimbali.
 
Yameanza yale yaliyoripotiwa Pemba kabla jeshi na polisi hawajaitwa kutuliza amani. Tanzania ya Mkapa inaendelezwa na Kikwete kwa kasi na nguvu mpya
 
Hata mimi siungi mkono machafuko ya aina yoyote - yawe yanayosababishwa na polisi au wananchi wa Tarime. Lakini pia sishangilii habari ambazo hazina kichwa wala miguu kuwa Tarime "kuna fujo".

Kuna matumizi mengi sana ya neno ukweli, wewe kuleta habari za magazeti (ambayo wakati wa mazishi ya Wangwe yalitoa ramli kuwa Tarime kutawaka moto kwa machafuko kabla ya kupata aibu ya mwaka) haimaanishi kuwa wewe una ukweli.

Hali halisi ya mambo haisapoti kinachoandikwa na magazeti hapa ili kuweka sababu ya kujaza mamia ya polisi Tarime ili "kutuliza fujo".

Mimi sina haya ya kukushoot wewe (messenger muhimu sana kwa habari za machafuko ya Tarime) ili kumaliza story. Ninasisitiza kile nilichosisitiza wakati wa mazishi ya Wangwe kuwa wananchi wa Tarime sio majuha kama ambavyo TBC1 na magazeti ya Rostam Azizi yalivyotaka (likiwemo mtanzania????) watu waaamini.

Mwisho wa siku, magazeti yalionekana yanachochea habari za uongo na mimi nilikuwa vindicated kwa kuonyesha picha halisi ya Tarime hapa JF - Hakuna fujo wa vita iliyotokea Tarime.

Wewe nimekuuliza useme kama una hakika kuwa Tarime kuna vita au la. Na swali la nyongeza ni kuwa vita ilianza lini (just in case utasema kuwa Tarime kuna vita na machafuko zinazohitaji mamia ya polisi kuzimaliza).

Hapa ni hoja tu huku maswali na majibu yakitolewa accordingly. Umbea na habari za uchochezi zitakemewa mkuu (katika hili nakuhakikishia right now).

Kama unakumbukumbu, mimi niliwahi kuuliza hapa juu ya nini chanzo cha haya mapigano? Isaya Mwita akanipa somo ka kutosha na nilimshukuru kwa hili.

Ninachoandika sasa ni matokeo maelezo kutoka kwa wana Tarime na mimi mwenyewe kufuatilia.

Tarime kuna tatizo ingawaje wengine hamtaki kukubali. Siko hapa kushawishi watu ambao hamtaki kusikia yale yasio faa. Naona ungekuwa tayari kuyafukia chini ya carpet.

Siandiki kwasababu ni Tarime, soma maandiko yangu kuhusu ugomvi wa Kyela ambako mimi ndiko natoka.

Hakuna excuse yoyote kwenye watu wa wilaya moja kugeukana na kuanza kugombana whether ni kwa kushawishiwa na watu wengine au la. Kama mnashawishiwa na watu wengine tena toka mbali, basi ndio ujinga wenyewe ambao inatakiwa muuseme wazi na kuupiga vita badala ya kutafuta mchawi.

Soma tena maandishi ya Mwita juu ya hayo mapigano yameanza lini. Sasa kama wewe unasema hayapo, basi hayo yote yanayoandikwa ni kwa kuwazulia wana Tarime, why? Kwanini hawasingiziwi watu wa wilaya zingine.

Watu mnakataa hata ukweli, ndio maana nchi inazidi kuwa na wajinga wengi. Mwerevu hakatai tatizo lililopo na badala yake anachukua hatua kulitatua na sio kukaa pembeni akisubiri wengine waje wamtatulie.
 
Hakuna makosa yoyote kubandika huu ujumbe hapa. IGP hataweza kukataa kama mambo yatawekwa kweupe namna hii. Hii haina tofauti na wale ambao wanaandika ujumbe kwa Kikwete, Mbowe, Mtikila na viongozi wengine kupitia hii forum.

Hii forum inasomwa na watu wengi na vizuri ikajulikana kuwa IGP amejulishwa kinachoendelea Tarime.

Magabe Kibiti,
Nafikiri kuna walaakini hapa. Hivi JF ndio njia ya Chadema kuwasiliana na serikali? Anapoandika ndani ya JF mlalahoi mwingine yeyote inakuwa ni mawazo yake binafsi na sio kuwa anategemea aliyoandika yawafikie wahusika.

Lakini Mnyika anawakilisha chama cha siasa, kwa hiyo ni upuuzi kwake kuitumia JF, unless iwe ni miliki ya Chadema, katika kuwasilishia jumbe za chama chake serikalini.
 
Mkamap,
Hapana. Enzi za Mwalimu alikuwa akipeleka FFU kule na kuzima wizi wa ng'ombe. There was law and order na Wakurya walijua mbele ya Nyerere hakuna mchezo. Hiyo ya Wamasai ni tofauti. Mimi nililenga wizi wa ng'ombe baina ya Wakurya kwa Wakurya wa koo mbalimbali.

Mkuu Jasusi,

Mimi nimesikia mapigano ya kiukoo na kikabila Tarime tokea miaka ya Nyerere. Tena wakati huo tuna radio moja tu na control kubwa ya serikali. Labda uniambie RTD nao walikuwa wamenunuliwa RA, walikuwa wanatangaza propaganda.

Ila kusema wakati wa mwalimu hayo mapigano hayakuwepo ni uongo wa mchana, sorry nitarudia tena kusema ni uongo maana siamini mtu kama Jasusi unaweza kusema hayo mapigano hayakuwepo. Sio kweli hata wakati wa Nyerere yalikuwepo. Labda kilichotofauti ni wakati wa Nyerere polisi walikuwa wanaenda kushughulikia wakati sasa who cares? Kama baadhi ya wana Tarime wenyewe wanasema mapigano hayapo, hata CCM wanaweza kusema mapigano hayapo, kwanini wakahangaike kuyamaliza?

Miaka ya 80 watu tulikuwa secondary schools tena tukiwa active kwenye siasa na kusikiliza RTD kila siku. Sasa mtu unapokuja na uongo kama huo kwamba wakati wa Nyerere mapigano hayo hayakuwepo, ninajiuliza unataka kumdanganya nani?
 
Kama unakumbukumbu, mimi niliwahi kuuliza hapa juu ya nini chanzo cha haya mapigano? Isaya Mwita akanipa somo ka kutosha na nilimshukuru kwa hili.

Ninachoandika sasa ni matokeo maelezo kutoka kwa wana Tarime na mimi mwenyewe kufuatilia.

Sidhani kama kupata habari au maelezo toka kwa Isaya mwita pekee yake tu kunaweza kufanya ufikie hitimisho kwenye fikara na maandishi yako kuhusu Tarime.

Ongeza muda kwenye kujua mambo ya Tarime ikiwezekana kusikia toka kwa kina mwita wengine.

Tarime kuna tatizo ingawaje wengine hamtaki kukubali. Siko hapa kushawishi watu ambao hamtaki kusikia yale yasio faa. Naona ungekuwa tayari kuyafukia chini ya carpet.

Sidhani kama kuna yeyote ambaye ana sababu ya kufukia mambo kwenye carpet hapa. Nimekukumbusha kuwa wakati wa msiba wa Wangwe kuna news kibao ziliwekwa hapa kuwa Tarime itawaka moto na blah blah nyingi. Swali ni kuwa, je mapigano na machinjano yalitokea Tarime wakati huo kama ambavyo TBC1 na magazeti ya Rostam Azizi yalieneza Tanzania nzima?

Siandiki kwasababu ni Tarime, soma maandiko yangu kuhusu ugomvi wa Kyela ambako mimi ndiko natoka.

Hakuna excuse yoyote kwenye watu wa wilaya moja kugeukana na kuanza kugombana whether ni kwa kushawishiwa na watu wengine au la. Kama mnashawishiwa na watu wengine tena toka mbali, basi ndio ujinga wenyewe ambao inatakiwa muuseme wazi na kuupiga vita badala ya kutafuta mchawi.

Ukipata sehemu hata moja ambayo mimi natoa excuse kwa mapigano au nashabikia "haya mapigano" naomba uiweke hapa. Mimi napinga habari potofu zinazowekwa hapa na kwenye media nyumbani ili kuhalalisha mamia ya polisi walioletwa Tarime "kutuliza fujo"

Tuliokulia Tarime tumezoea kuwaona polisi kwa wingi sana kuanzia mwaka 1995 na kila baada ya miaka mitano (wakati wa uchaguzi) na sio wakati mwingine wowote. Hii ni moja ya sababu ya kukushawishi kukubali udaku na uzushi kuwa Tarime sasa hivi kuna "fujo na mauaji ya kutisha".

Soma tena maandishi ya Mwita juu ya hayo mapigano yameanza lini. Sasa kama wewe unasema hayapo, basi hayo yote yanayoandikwa ni kwa kuwazulia wana Tarime, why? Kwanini hawasingiziwi watu wa wilaya zingine.

Watu mnakataa hata ukweli, ndio maana nchi inazidi kuwa na wajinga wengi. Mwerevu hakatai tatizo lililopo na badala yake anachukua hatua kulitatua na sio kukaa pembeni akisubiri wengine waje wamtatulie.

Mimi nimezaliwa na kukulia Tarime, sihitaji kusoma maandishi ya Mwita ili kujua kinachotokea Tarime. Sina sababu ya kujua motive ya Mwita au yule mwandishi wa Tarime ambayo alitumiwa kuandika habari za kichochozi wakati wa msiba wa Wangwe na zikatumiwa na magazeti karibu yote Tanzania bila hata kufanyiwa editing.

Ninaeleza ukweli (na imethibitishwa hapa baada ya watu wa Tarime kutouana na kuchinjana) na kama ambavyo matukio ya Tarime yalionesha kuwa mimi nilieleza hali halisi ya Tarime ila vyombo vya habari vilileta uongo na uzushi wakati wa msiba wa Wangwe.
 
Magabe Kibiti,
Nafikiri kuna walaakini hapa. Hivi JF ndio njia ya Chadema kuwasiliana na serikali? Anapoandika ndani ya JF mlalahoi mwingine yeyote inakuwa ni mawazo yake binafsi na sio kuwa anategemea aliyoandika yawafikie wahusika.

Lakini Mnyika anawakilisha chama cha siasa, kwa hiyo ni upuuzi kwake kuitumia JF, unless iwe ni miliki ya Chadema, katika kuwasilishia jumbe za chama chake serikalini.

Hakuna makosa yoyote kuitumia JF au magazeti ya bongo. Ni kawaida kuwa na press conference kwenye matukio muhimu duniani na huu ni wakati murua kabisa wa kuitumia JF kufikisha ujumbe.

Media hutumika kusaidia habari iwe kwenye record za wengi zaidi. Pamoja na kuwasiliana na serikali na wahusika wote. Ni vizuri mambo yakawa kwenye record zote nchini (ikiwemo JF). Wewe kama una ugomvi na JF na Chadema (kama nilivyokusoma kwenye maandishi yako mengi hapa) unaweza kuendelea nao tu wakati mwingine. Kwa sasa habari ya kinachotokea Tarime ni muhimu kupata njia ya kuwafikia walengwa na wasomaji wengi zaidi.
 
Mkuu Jasusi,

Mimi nimesikia mapigano ya kiukoo na kikabila Tarime tokea miaka ya Nyerere. Tena wakati huo tuna radio moja tu na control kubwa ya serikali. Labda uniambie RTD nao walikuwa wamenunuliwa RA, walikuwa wanatangaza propaganda.

Ila kusema wakati wa mwalimu hayo mapigano hayakuwepo ni uongo wa mchana, sorry nitarudia tena kusema ni uongo maana siamini mtu kama Jasusi unaweza kusema hayo mapigano hayakuwepo. Sio kweli hata wakati wa Nyerere yalikuwepo. Labda kilichotofauti ni wakati wa Nyerere polisi walikuwa wanaenda kushughulikia wakati sasa who cares? Kama baadhi ya wana Tarime wenyewe wanasema mapigano hayapo, hata CCM wanaweza kusema mapigano hayapo, kwanini wakahangaike kuyamaliza?

Miaka ya 80 watu tulikuwa secondary schools tena tukiwa active kwenye siasa na kusikiliza RTD kila siku. Sasa mtu unapokuja na uongo kama huo kwamba wakati wa Nyerere mapigano hayo hayakuwepo, ninajiuliza unataka kumdanganya nani?

Umemiss point ya Jasusi kuhusu wakati wa mwalimu. Wakati wa mwalimu, kama kulikuwa na mapigano Tarime (ambayo muliyasikia kwenye RTD), basi polisi au FFU waliletwa haraka sana na wakayatuliza na sio "kuyaacha tu" yakaendelea mpaka wakati wa uchaguzi.
 
Popote pale Tanzania ambapo CCM huwa inabanwa kwenye uchaguzi hutokea fujo, tena fujo kubwa, na fujo zote hizi hufanywa na polisi kwa maelekezo ya CCM. CCM wataingiza hii nchi kwenye maafa. Kama hawapo tayari kwa ushindani wa kistaraabu wangefuta mfumo wa vyama vingi kulikoni kuendelea kuwadanganya watu.

Mkuu...

Nakubaliana na wewe kwa 100% kwa hili. Bado CCM haiko tayari kuwa na mfumo wa vyama vingi.Hata ukiangalia mifumo yetu ya polisi,usalama wa taifa,mahakama,jeshi, Broadcasting Corporations,radio, hata bunge lenyewe utaona kabisa kuwa bado kuna ndimi za chama tawala kukandamiza upinzani kwa namna yoyote ile.Bado tuna akina "Kingunge" wengi ambao kwao wapinzani ni kama rebels!! na siyo simply dissidents!! Wao wanataka kupaint a picture kuwa wapinzani ni majitu ya kupenda fujo!! kuuwa na kuleta vurugu!! na wao ndiyo watu wa amani na uzalendo halisi kwa nchi!!
Sasa tujiulize tu swali moja kuwa wao je ndio wenye mapenzi ya kweli na nchi yetu????
 
Acha uongo wewe poti, lini wajita wakapigana na wamasai? kwi kwi kwi

WEWE kama ni mkweli nasi mnafiki poti na mpenda kukubali ukweli
waambie hadhira kinaga ubaga
Mapigano ya namna hiyo yameenza lini sema ukweli wako.

Choko choko za wanchari na wanchori zimeaanz alini?

Hahaha Wajita hawapigani na wamasai kwani ni akina nani wanapigana na wamasai na kwasababu zipi?
 
mambo yalivyo:

1222150687_ffuweb.jpg

Hivi kati ya mabloga wetu wote hakuna aliyekwenda Tarime?
 
Umemiss point ya Jasusi kuhusu wakati wa mwalimu. Wakati wa mwalimu, kama kulikuwa na mapigano Tarime (ambayo muliyasikia kwenye RTD), basi polisi au FFU waliletwa haraka sana na wakayatuliza na sio "kuyaacha tu" yakaendelea mpaka wakati wa uchaguzi.

Poti
wewe ndio una miss point ya mtanzania

ya kwamba kwanini mapigano yawepo?? Na utahubiri vipi demokrasia kwa wanakijiji wakati wewe ndani mwako kila siku mnachomana visu wewe na mkeo na watoto wenu??

Tujifunze kuukubali ukweli .
Niemkuulizeni mbona kwenye maandamano ya amani hua kumejazana askari ??ulishawahi kuhoji hilo?

yeyote anayelata vurugu huko home lazima police wa deal naye perpendicularly na aadhibiwe vigorously.
 
Akizungumza jana wakati wa kumnadi mgombe udiwani wa CCM Tarime mjini, Peter Zacharia, Msekwa, alisema atamweleza Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM amwamuru Kanali Machibya awaamuru polisi kutumia nguvu ya ziada katika kubilina na hali hiyo wakati huu wa kampeni za kuwania kiti cha ubunge wa Tarime.

Msekwa na CCM wamefilisika sana. Wakati wa uchaguzi huko Kiteto tuliambiwa kuwa watu kadhaa wa upinzani walijeruhiwa lakini Msekwa huyu hakuomba amri za matumizi ya nguvu ya dola. Kumbe kweli mtu huyu hajui utawala wa kidemokrasi, anategemea kutumia nguvu tu ili kufanikisha mambo yake; ni heri kabisa alinyang'anywa uspika.
 
WEWE kama ni mkweli nasi mnafiki poti na mpenda kukubali ukweli
waambie hadhira kinaga ubaga
Mapigano ya namna hiyo yameenza lini sema ukweli wako.

Choko choko za wanchari na wanchori zimeaanz alini?

Hahaha Wajita hawapigani na wamasai kwani ni akina nani wanapigana na wamasai na kwasababu zipi?

Wanchori ni kina nani tena?

Kwi kwi kwi, poti, wajita watapigana na wamasai kwa ajili ya nini? pamba au samaki?

Back to the issue, mimi ndiye nilimuuliza mtanzania swali la mapigano yameanza lini. Kama hana jibu anaweza kusema tu.
 
Umemiss point ya Jasusi kuhusu wakati wa mwalimu. Wakati wa mwalimu, kama kulikuwa na mapigano Tarime (ambayo muliyasikia kwenye RTD), basi polisi au FFU waliletwa haraka sana na wakayatuliza na sio "kuyaacha tu" yakaendelea mpaka wakati wa uchaguzi.

Magabe,

Ulichoandika ndicho hata mimi nimeandika hapo juu kwamba labda tofauti ni kwamba wakati wa Mwalimu, polisi walikuwa wanatumwa mara moja kwenda kutuliza wakati sasa hakuna anayejali.

Mtu akisema hivyo nitamwelewa lakini sio kusema wakati wa Mwalimu mapigano hayakuweko eti kulikuwa na wizi wa ng'ombe tu. Jamani tuwe wakweli vinginevyo wote tunajiingiza kwenye propaganda za akina RA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom