Hold on a minute; riots na vitu kama hivyo siyo suala la watu wa Tarime tu. Vinatokea sehemu nyingi duniani na ndio maana tunakuwa na Polisi.
a. Mtu anayevunja sheria ni mhalifu. Period hakuna udhuru wa Chama wala siasa katika hilo. Kama hawa watu wamempiga mawe hakuna cha kudai ni wana Chadema au wana CCM; hawa ni wahalifu na sheria ichukue mkondo wake.
b. Kama Mtikila alikuwa anaeneza habari hizo na kudai kwa uthabiti kuwa x,y,z wamemuua Wangwe na kueneza habari hizo ili kupanda chuki miongoni mwa wananchi au kuchezea hisia zao hilo linaweza kuwa kwenye uhuru wa maoni. Lakini tukijiuliza kama angesema Makamba, Kikwete na Msekwa wamemuua Mbatia mnafikiri kweli Polisi wangeacha asambaze habari hizo au angetiwa pingu kwa "uchochezi"?
Sasa kama habari hii kuwa "Wananchi walipandwa na hasira na kuwaomba polisi wamkamate kwa kufanya uchochezi lakini polisi wakamuacha aendelee kusema na kugawa makaratasi yenye maneno yake kuwa Mbowe, Mengi, Ndesa, Slaa, Mnyika na Zitto ndio waliopanga na kumuua Chacha Wangwe kwa kutuma vijana wamchome Kisu na baadaye kumpiga na nyundo. Hapo ndipo wananchi wakamgeukia na kumpiga mawe" Ni kweli, tunajiuliza sasa Polisi waliomwagwa huko ni wa nini?
c. NI kutokuwa makini kuwawajibisha CHadema au mtu mwingine yeyote kwa vitendo vya watu wenye akili na utashi wao. Kila mtu lazima ajifunze kubebeshwa mzigo wake yeye mwenyewe. Kwanini mzigo huu wa watu kupiga watu wengine mawe wabebeshwe Chadema au CCM for that matter? Kwanini wasibebeshwe wahalifu wenyewe na kuwajibishwa.
Kama aliyechochea watu hao hasira kwa maneno yake ni Mtikila kwanini Mtikila asiwajibishwe kwa kuchochea hasira za watu namna hiyo kwa maneno ya kichochezi?
Kama Polisi walikuwepo na waliona uchochezi unaodaiwa kufanywa na Mtikila kwanini wao wenyewe wasiwajibishwe kwa hilo. Kama watadai ni uhuru wa maoni, hebu mtu athubutu huko Tarime aanza kusambaza vipeperushi kuwa CCM, Kikwete na Makamba walipanga njama za kumuua Wangwe wakaajiri wauaji kutoka Afrika ya Kusini ambao walistage accidenti na mmoja wa watu waliosimimamia operesheni hiyo ni Mbunge maarufu wa Chama hicho akishirikiana na Kamishna mmoja wa Polisi. Na ya kuwa yule daktari mpya wa Mkoa wa Dodoma aliletwa pale kwa ajili ya kuficha ushahidi kwani ilikuwa ni siku chache tu tangu afike Dodoma ndiyo kifo cha Wangwe kilitokea. Mtu huyo aeneze uvumi huu kwa kugawa makatarasi kwenye kampeni na muone kama Msekwa na Jeshi zima la Polisi halitashuka Tarime.
Tusiwe na haraka ya kuhukumu watu wengine kwa makosa ya wengine. Kila mtu abebeshwe mzigo wake yeye mwenyewe.
On the other hand, kwanini watu hawa wa wafanye kitu kana kwamba wanamtetea Mbowe na Chadema huko Tarime?