of course huwezi kupata kwa sababu unaangalia suala hili kwa mwanga wa itikadi za chama badala ya kuona uhalifu uliotendeka na kuukataa. Ukishavuka huo mtazamo wa chama utaona kuwa uhalifu usizoelewe kukubalika, au hata kufafanuliwa bali ni lazima ushughulikiwe.
Mtikila hakustahili kipigo hicho na kama alivyosema na mimi niliashiria hapo juu ni kuwa Polisi wanawajibika moja kwa moja hasa kama alitoa taarifa za kuwa kuna mipango ya kitu kama hicho. Pamoja na hayo kila mtu awajibishwe kwa maneno yake na vitendo vyake, mtu akinitukania mama yangu kuna level ya matusi ambayo naweza kumuambia "bwana, mweke mama yangu pembeni" akiendelea nikimshindilia ngumi na kumvunja meno nitakuwa nimekosea; lakini atakuwa amejitakia kwa sababu nilishamwambia asinitukanie mama yangu.
Mambo ya kuchezea vionjo vya watu au hisia zao ni mabaya sana and should not be taken for granted. Tunaona jinsi gani Rwanda the flames of hatred were fueled by maneno ya kichochezi na kuita watu "cockroaches" n.k Tumeyaona maneno yakitumika kuwasha moto wa kisasi Iraq, Palestina, Israeli na hata katika historia ya Marekani during the civil rights movement.
Kama huoni uzito wa matumizi ya maneno na nguvu ya "spoken word' sijui itakutaje. Get over your politics na uone kuwa siasa za vitisho, uchochezi, hazina nafasi. Lazima watu warudi kwenye "hoja hujibiwa kwa hoja".
But, of course, huwezi kufanya hivyo kwa sababu kwako ni siasa na siasa tu.