Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Mtikila atakuwa alikwisha waandaa watu wa first-aid. He must have anticipated this reaction, and perhaps expected the worse
Hehehehe

Leo nimejikuta nacheka tu... This reminds me mswahili...

Yangu mimi macho!
 
Katika wapinzani niliokuwa nawaona makini na wana msimamo Mtikila alikuwa mmojawao, lakini siku hizi anaonekana buree sana, yaani kama pesa ndio zinaweka watu wazima hivii, yaani waonekane kama msichana ma**** ambaye anafanya vitu kutokana na hela alizopewa haya mambo ya aibu. Pole mzee
 
Sipati picha kama dhahma hii ingemkuta Dr Slaa au Zitto nadhani wanamgambo wa Chadema hapa JF wangekuwa wananoa mapanga yao. Ama kweli mkuki mtam kwa nguruwe...

Vipi hilo jiwe lingempata mgombea wa CCM? Hilo balaa ambalo Tossi angezusha huko, usiombe! Unakumbuka Venance Tossi alikuwa kamanda (CO) wa FFU mkoa wa Dar? Unakumbuka alifanya nini wakati wanachama wa CUF walipoandamana baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 pale Dar? Yaani ilikuwa unyama zaidi ya unyama, au wenyewe wanaita "undava", zile picha za video ukiziona utadhani watu wako Iraq au Kosovo, alitembeza kipigo cha "kufa mtu". Akina Jenerali Ulimwengu walipigia sana kelele hiyo kitu pamoja na kina Hellen Kijo-Bisimba na Prof Haroub Othman, kupinga jinsi waandamanaji walivyokuwa wanaburuzwa kubondwa marungu ya kisogoni na kuvunjwa miguu, lakini Mkapa akawapelekea jibu la kuwashangaza zaidi: akampandisha Venance Tossi cheo! Tangu hapo Tossi ni mwendo wa kupaa tu katika madaraka huko polisi, na anakumbuka vizuri sana matukio yanayompatia cheo!

Kwa kweli kuhusu demokrasia kwetu bado kabisa! Lakini tutafika tu, ni kuwa mambo hayajaiva kiasi cha kutosha, siku watu wakifikia "threshold" mapinduzi yatakuja yenyewe. Ni kama mimba, ikifikia muda wake wa kupata uchungu lazima mtoto azaliwe, hawezi kubakia humo milele.
 
Ushahidi upi unataka wakati ripoti ya ukaguzi na ya tume ya Mwakyembe ziko wazi? Ni wajibu wa vyombo husika kuwapeleka mahakamani wahusika. Dr. Slaa hajasema waitwe Scotland yard kuchunguza maana ushahidi tayari uko wazi.


Sikuelewi
Kwanini unaona kila mara linapofika suala la DR SLAA unaona ni mhimu vyombo husika vitekeleze wajibu wake.Lakini hapo hapo unamtaka Mtikila aende mahakamani?? sioni hoja.

Kwanini usione pia Mtikila katoa tuhuma zake hivyo ni wajibu wa vyombo husika na watuhumiwa kutumia haki yao kisheria ? Ama hiyo halipi?

Sielewi unamaanisha nini.
DR SLAA alipotoa tuhuma hao KIJANI walikuja kuchunguza tuhuma hizo wakati Slaa tayari ameshatangaza watuhumiwa.

Mtikila akiita scotland yard na akiwataja watuhumiwa ni kosa .Kazi sana hapa
 
Hivi huyu mchungaji Mtikila kweli ni mtu mwenye akili timamu ?. Japo siungi mkono vurugu za uchaguzi au vurugu zozote, lakini kwa mawazo yangu, huyu mchungaji ni mtu aliyechanganyikiwa kwa kiasi fulani. Naomba wana JF mnielewe sina maana kuwa ni mwenda wazimu bali ni extremist fundamentalistl. Anajenga hoja ambazo kwa mtu wa kawaida atangundua ni fikra za kusadikika.

Maneno yake ni uchochezi wa wazi, polisi hawakumdhibiti kwa sababu wapinzani wakigombani ni kwa advantage ya CCM.
 
Hivi huyu mchungaji Mtikila kweli ni mtu mwenye akili timamu ?. Japo siungi mkono vurugu za uchaguzi au vurugu zozote, lakini kwa mawazo yangu, huyu mchungaji ni mtu aliyechanganyikiwa kwa kiasi fulani. Naomba wana JF mnielewe sina maana kuwa ni mwenda wazimu bali ni extremist fundamentalistl. Anajenga hoja ambazo kwa mtu wa kawaida atangundua ni fikra za kusadikika.

Maneno yake ni uchochezi wa wazi, polisi hawakumdhibiti kwa sababu wapinzani wakigombani ni kwa advantage ya CCM.

mimi nafikiri tunakuza maneno
Polisi hawakudhibiti nini jamani? kama angepondwa pondwa mawe hapo sawa .Lakini jamaa amevizia Mtikila kageuka upande mwingine kampa la kichwa hii ni ishara ya kuwa mtu huyu kutumwa.

Kama angepandwa ghadhabu wakamshambulia hapo sawa,lakini mtu huyu kamvizia .
 
Sasa si wampeleke mahakamani? Msimamo wangu juu ya Wangwe niliutoa siku ile ile anakufa kwamba ile ni ajali. Kama kuna mtu anachochea vurugu au anasema uwongo basi polisi au hao waliotuhumiwa waende mahakamani. Sheria ndivyo inavyosema na wala sio kupiga watu.

Vurugu zote zinaanzia na mambo madogo kwa kuwatumia hao vijana wasio na kazi mitaani, mwisho wake ni nchi nzima kuangamia. Lazima tulaani vurugu zozote zile.

Hapa sasa wewe unaleta siasa za kuku na mayai nani alianza! Unajua ukitaka wananchi waheshimu sheria inabidi kwanza Serikali ya CCM (I mean CCM) waheshimu sheria. What do you expect kwenda kushitaki Mtikila wakati unaona kabisa huko mahakamani ni mbali na sheria zetu ni kupoteza muda na fedha! Wake up; CCM and the executive government have a problem, and this will cost this nation. Believe me nchi hii Rais hadi mtu wa chini hawaheshimu sheria, ndiyo maana unaona haya yanatokea.

Mtanzania ukitaka nidhamu iwepo kwanza anza juu ndiyo uwaseme hao wa-chini, wake-up!
 
Hapa sasa wewe unaleta siasa za kuku na mayai nani alianza! Unajua ukitaka wananchi waheshimu sheria inabidi kwanza Serikali ya CCM (I mean CCM) waheshimu sheria. What do you expect kwenda kushitaki Mtikila wakati unaona kabisa huko mahakamani ni mbali na sheria zetu ni kupoteza muda na fedha! Wake up; CCM and the executive government have a problem, and this will cost this nation. Believe me nchi hii Rais hadi mtu wa chini hawaheshimu sheria, ndiyo maana unaona haya yanatokea.

Mtanzania ukitaka nidhamu iwepo kwanza anza juu ndiyo uwaseme hao wa-chini, wake-up!

Nakumbuka ya Zimbabwe juzi juzi tu. Tarime naona kama kuna watu wanafanya mazoezi ya Agenda 21 yaani kazi kubwa mbele yetu mwaka 2010. Wana JF maneno haya tutakumbushana wakati mwafaka. HALI SI NZURI
 
Yule mchungaji matata anayeitwa Mtikila, hivi pundwe amepelekwa hospitali kulazwa na kushonwa nyuzi baada ya kupigwa mawe na wananchi wenye hasira. Mtikila alipata dhahama hiyo baada ya kuhutubia kuwa Mbowe na CHADEMA yake ndio waliomuua Chacha Wangwe.

.......ndiyohiyo

Mambo mengine ni common sense tu, yaani Mtikila amekula hela za Rostam, leo anawahutubia wananchi wa Tarime na kuwaambia kua ni Chadema ndio wamemuua Wangwe, halafu eti tulitegemea wananchi wamsikilze bila majibu?

Hata mimi nisingeamini kuwa hiyo ni Tarime ninayoisikia kila siku, Mtikila kwa nini anasema maneno haya sasa wakati wa uchaguzi? Kwa nini hakuyasema kabla ya uchaguzi?

Wananchi wa Tarime ni lini waliwahi kulala usingizi kama majimbo mengine?
 
Magabe,
Humu mtandaoni tupo watu wa taaluma mbalimbali na uelewa wetu wa mambo pia ni tofauti. Gold Cyadination ni process inayoeleweka vizuri sana pamoja na madhara yake. Na pia CN haichukui muda kuleta madhara ya kiafya kwa mtu. K.m. maji kiasi ya kijiko cha chai yenye 2% ya CN inaweza ikaondoa roho ya mtu.

Nafurahi sasa umeanza kuongelea issue muhimu za Tarime na sio mambo ya sidiria, mihogo na Mtikila kama ulivyokuwa umeanza kuyaleta hapa. Nilijua taaluma za wana JF ndiyo maana muda wote nimesisitiza kuongelea issue za muhimu kama hizi.

Sasa kama kweli ushahidi mkubwa upo wa matumizi mabaya ya CN na kumwagwa kwenye vyanzo vya maji, basi ulete ili tujenge hoja ya kuwaadhibu hao wachimbaji. Lakini kama hakuna, basi tuachane na porojo za mitaani. Kuamini au kutoamini 'system', ni position ya kuchukua kulingana na hoja, lakini tukumbuke pia kuwa, ni rahisi sana kujenga uzushi.

Okay,

Sasa tunaanza kazi (wakati pia nikisubiria ueleze rules of engagement na aina ya ushahidi unaoutaka - wa picha, kitaalamu, namba ya vifo na magonjwa, au maneno yangu against ya makampuni ya madini):

Hapo zamani za kale - kabla ya ukoloni, wazee (chacha, marwa, na bhoke) wa kimila wenye ushawishi mkubwa kabisa kwa jamii yao (ya kikurya) walikaa kikao ili kuamua hatima ya jamii yao. Kikao hicho ambacho kilichukua masaa matatu kilifikia maamuzi yafuatayo:

.....itaendelea
 
mimi nafikiri tunakuza maneno
Polisi hawakudhibiti nini jamani? kama angepondwa pondwa mawe hapo sawa .Lakini jamaa amevizia Mtikila kageuka upande mwingine kampa la kichwa hii ni ishara ya kuwa mtu huyu kutumwa.

Kama angepandwa ghadhabu wakamshambulia hapo sawa,lakini mtu huyu kamvizia .

Kwi kwi kwi,

poti, inawezekana huyo jamaa aliyemvizia mtikila na kumpiga na jiwe ni mmoja wa polisi waliojazana Tarime, nani ajuaye?!
 
Pole sana mzee wetu Mtikila, mzee wa "kulipua mabomu". Hiyo ni ajali ya bomu kumlipukia mlipuaji. Uwe mwangalifu wakati mwingine....

Hapo umenigusa sana mkuu!!!Inanikumbusha ule wimbo wa mvuvi kina.Mzowea kuvua samaki kwenye madimbwi akienda baharini lazima atazama.Mtikila aliweza kujenga jina lake kwa kuwapaka watu wenye tuhuma zaidi ya alizokuwa akizitaja,na hivyo watuhumiwa hao kuhofia kum-bana zaidi wakijua yatatokea makubwa zaidi.This time,amekosea mahesabu yake.Anataka kulipa mamilioni ya Rostam kwa njia ambazo zinamgharimu zaidi ya hilo deni.Pengine atajifunza this time.
 
Mtikala kwenda Tarime, kupanda jukwaan na kuropoka hayo maneno inaashiria anataka fujo itokee anataka watu wapigane na anataka mchafuko hapo tarime.ther z no option anatakiwa apigwe na hao ccm wakileta fujo mara kumi ndo 2tajua kabisa katumwa,
huwez ongea ujinga kama ule nyumban kwa mbunge ambaye hata watu hawajamsahau
hongo hizo na hapa Tanzania lazima watu wafe ndo ujinga wa CCM uishe.
 
Lakini kwanini akina SLaa na wengineo wanaotajwa na Mtikila kuwa ndio waliopanga mauaji ya Wangwe hawachukui hatua za kisheria?Na hapa by "hatua za kisheria" simaanishi kwenda kushtaki polisi bali kumpeleka mahakamani moja kwa moja?Slaa na wenzake walipotoa list of shame,watajwa walitishia kwenda mahakamani na hawakwenda,na hivyo kututhibitishia kwamba tuhuma zote dhidi yao zilikuwa za kweli.Wakati mwingine kukaa kimya unapotuhumiwa kunaweza kumpa jeuri mtoa tuhuma kuendelea kumwaga tuhuma zaidi.Unadhani leo Mtikila angediriki kuongea hayo iwapo akina Slaa wangechukua hatu mara baada ya ile press conference ya kuwatuhumu na mauaji ya Wangwe?Kipigo alichopata kinaweza kuwa solution ya muda mfupi tu lakini ukweli ni kwamba huyu mtu alipaswa apandishwe kizimbani kuthibitisha tuhuma zake.
 
Lakini kwanini akina SLaa na wengineo wanaotajwa na Mtikila kuwa ndio waliopanga mauaji ya Wangwe hawachukui hatua za kisheria?Na hapa by "hatua za kisheria" simaanishi kwenda kushtaki polisi bali kumpeleka mahakamani moja kwa moja?Slaa na wenzake walipotoa list of shame,watajwa walitishia kwenda mahakamani na hawakwenda,na hivyo kututhibitishia kwamba tuhuma zote dhidi yao zilikuwa za kweli.Wakati mwingine kukaa kimya unapotuhumiwa kunaweza kumpa jeuri mtoa tuhuma kuendelea kumwaga tuhuma zaidi.Unadhani leo Mtikila angediriki kuongea hayo iwapo akina Slaa wangechukua hatu mara baada ya ile press conference ya kuwatuhumu na mauaji ya Wangwe?Kipigo alichopata kinaweza kuwa solution ya muda mfupi tu lakini ukweli ni kwamba huyu mtu alipaswa apandishwe kizimbani kuthibitisha tuhuma zake.

Watanzania wengi wana mawazo kama haya ambayo ni potofu!

Si kila tuhuma inabidi uzijibu, utazijibu ngapi kama watu hawakupendi au kama kuna political games? wakati mwingine ukikaa kimya unaonekana kuwa uko matured.

Yaani kama Mtikila mzalendo anatakiwa aende polisi akashtaki kuwa CHADEMA wamemuua wangwe. Mbona ameshastaki kesi nyingi sana, tena kubwa na akashinda, kwa nini uite wanahabari useme vitu hivyo?

Waberoya
 
Mzee Mwanakijiji,

I hope unaelewa siasa. Kama unaelewa basi utajua siasa si mahakamani.

Leo FIFA wamewaadhibu Croatia kwa chants za Monkey dhidi ya mchezaji wa UK, kwanini wasiwaajibishe hao waliokuwa wanatoa hayo maneno ya kashfa badala ya kuiadhibu nchi? Chama cha siasa kinakuwa judged sio kwa matendo ya viongozi wake tu bali hata matendo ya washabiki wao.

.

Kuna mifano mingine haiwezi kuapply kama FIFA

Au ndio ule mchezo wa kumfukza au kumfokea mke wako pindi mtoto wenu wa kike anapopata ujauzito kabla ya ndoa?

Hivi katika wale wote walioko gerezani hawana makundi yao kama, makanisa, misikiti, vyama, familia,koo, makabila, n.k kwa hiyo wote hao makundi yao walaumiwe? where is personal accountability?

Basi hizi ni siasa za kitoto I may say. Pamoja na kuwa Mtikila anaweza kutofautiana nao CHADEMA sioni sababu ya wao kufurahia yeye kupigwa mawe.

Shame on their bones (whomever celebrates Mtikila's stoning).

🙁

Wewe nawe naona umefurahia unapretend kama vile unamwonea huruma Mtikila, hakuna kumuonea huruma mnafiki malipo yake NAONA YANAWAHI KULIKO NILIVYOTARAJIA.Yule jamaa aliyempiga jiwe anashabaha sana nampa hongera popote pale alipo!

waberoya
 
Basi hizi ni siasa za kitoto I may say. Pamoja na kuwa Mtikila anaweza kutofautiana nao CHADEMA sioni sababu ya wao kufurahia yeye kupigwa mawe.

Shame on their bones (whomever celebrates Mtikila's stoning).

🙁

Wakati naelekea kujenga....... niliposikia habari hizi dala dala nzima walichekelea. Hapa inamaanisha nini?
 
of course huwezi kupata kwa sababu unaangalia suala hili kwa mwanga wa itikadi za chama badala ya kuona uhalifu uliotendeka na kuukataa. Ukishavuka huo mtazamo wa chama utaona kuwa uhalifu usizoelewe kukubalika, au hata kufafanuliwa bali ni lazima ushughulikiwe.

Mtikila hakustahili kipigo hicho na kama alivyosema na mimi niliashiria hapo juu ni kuwa Polisi wanawajibika moja kwa moja hasa kama alitoa taarifa za kuwa kuna mipango ya kitu kama hicho. Pamoja na hayo kila mtu awajibishwe kwa maneno yake na vitendo vyake, mtu akinitukania mama yangu kuna level ya matusi ambayo naweza kumuambia "bwana, mweke mama yangu pembeni" akiendelea nikimshindilia ngumi na kumvunja meno nitakuwa nimekosea; lakini atakuwa amejitakia kwa sababu nilishamwambia asinitukanie mama yangu.

Mambo ya kuchezea vionjo vya watu au hisia zao ni mabaya sana and should not be taken for granted. Tunaona jinsi gani Rwanda the flames of hatred were fueled by maneno ya kichochezi na kuita watu "cockroaches" n.k Tumeyaona maneno yakitumika kuwasha moto wa kisasi Iraq, Palestina, Israeli na hata katika historia ya Marekani during the civil rights movement.

Kama huoni uzito wa matumizi ya maneno na nguvu ya "spoken word' sijui itakutaje. Get over your politics na uone kuwa siasa za vitisho, uchochezi, hazina nafasi. Lazima watu warudi kwenye "hoja hujibiwa kwa hoja".

But, of course, huwezi kufanya hivyo kwa sababu kwako ni siasa na siasa tu.


M. M

Umejaribu sana kuelimisha kuhusu hili. Naamini wapo watu wanaokuelewa. Kuna wengine wishes zao nikuona kuwa CCM au CHADEMA ndio zinafagiliwa ili hatimae wafurahi kuliko kuangalia tunakoelekea na tulipotokea in a big picture. Wakati nasikiliza tuhuma za Mtikila niliwaambia jamaa zangu kuwa kama polisi hawatamkamata na kumhoji halafu wamuachie basi somalia, kongo (DRC) inakaribia. Leo kuna mmoja wao amenitext kuniambia uliamaanisha nini?

i will always stick on COMMON INTEREST.......

Asanteni sana
 
Kusema mtu amemuua mwingine ni kosa la jinai. Mwenye wajibu wa kufungua kesi ni jamhuri. Sio Mbowe, Mengi, Slaa, Mnyika wala Zitto. Hivyo, polisi wamkamate Mtikila.
HIYO SIO MARA YA KWANZA KWA YEYE KUTOA TUHUMA KAMA HIZO HUYO KICHWA CHAKE KIMEPIGWA SANA SASA AMESHACHOKA HANA UWEZO WA KUFIKIRIA KAMA BINADAMU WA KAWAIDA , APELEKWE AKAPIMWE AKILI KWANZA

2. Kusema kwamba asishushwe jukwaani apelekwe mahakamani nayo ni kituko kwa kuwa akishtakiwa leo kesi itaisha mwaka 2009 wakati uchaguzi wa Tarime ni Oktoba 12 mwaka 2008.
UNA UHAKINA NA UNAYOSEMA ? HATA IKIISHA MWAKA 3000 SI USHAHIDI BADO HAUJAKAMILISHWA ?

Huyu ndiye Mtikila, aliyefungwa jela kwa kusema CCM wamemuua Kolimba na aliyeshtakiwa kwa kuita maiti ya Nyerere kuwa ni MZOGA

HUKO JELA WALIMGONGA SANA KICHWA CHAKE KAMA MORGAN WA ZIMBABWE HANA AKILI SAWA HUYU TUSIHANGAIKE NAE

Hivi yule Mwehu aliyeua wenzake pale muhimbili hospitali kwa nini hakuachiwa huru na kupewa zawadi ya pipi jamani?

Kama mtikila ni hayawani, kwanini watu insane wanaruhusiwa kuwa viongozi wa vyama vya siasa na kugombea? Sheria za nchi si zinakataza?

Mwanakijiji, anzisha kampeni jamani Mtikila apimwe akili.

Alipofanya press dsm kabla ya kwenda alitangaza kuwa anakwenda kusema wazi jinsi Mbowe na Mengi walivyomuua Wangwe. Polisi wakamuangalia tu akifanya kosa la jinai.

Akaenda Tarime toka kampeni zimeanza yeye ni kuzunguka na pikipiki huku akisambaza vikaratasi vyake vya uchochezi tena akilindwa na magari ya FFU.

Sasa kama kuna wimbi la wizi, halafu polisi badala ya kukamata wezi wanawalinda wezi hao. Unategema raia wataheshimu utawala wa sheria?

Unajua kwanini Darisalama kuna wimbi la mob justice? When the rule of law is abondoned, when the laws of the rulers prevail, people raise up with no rules or laws. They believe in themselves.

Namuombea apone haraka jamani, huu ni mwezi mtukufu

Asha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom