HeheheheMtikila atakuwa alikwisha waandaa watu wa first-aid. He must have anticipated this reaction, and perhaps expected the worse
Sipati picha kama dhahma hii ingemkuta Dr Slaa au Zitto nadhani wanamgambo wa Chadema hapa JF wangekuwa wananoa mapanga yao. Ama kweli mkuki mtam kwa nguruwe...
Ushahidi upi unataka wakati ripoti ya ukaguzi na ya tume ya Mwakyembe ziko wazi? Ni wajibu wa vyombo husika kuwapeleka mahakamani wahusika. Dr. Slaa hajasema waitwe Scotland yard kuchunguza maana ushahidi tayari uko wazi.
Hivi huyu mchungaji Mtikila kweli ni mtu mwenye akili timamu ?. Japo siungi mkono vurugu za uchaguzi au vurugu zozote, lakini kwa mawazo yangu, huyu mchungaji ni mtu aliyechanganyikiwa kwa kiasi fulani. Naomba wana JF mnielewe sina maana kuwa ni mwenda wazimu bali ni extremist fundamentalistl. Anajenga hoja ambazo kwa mtu wa kawaida atangundua ni fikra za kusadikika.
Maneno yake ni uchochezi wa wazi, polisi hawakumdhibiti kwa sababu wapinzani wakigombani ni kwa advantage ya CCM.
Sasa si wampeleke mahakamani? Msimamo wangu juu ya Wangwe niliutoa siku ile ile anakufa kwamba ile ni ajali. Kama kuna mtu anachochea vurugu au anasema uwongo basi polisi au hao waliotuhumiwa waende mahakamani. Sheria ndivyo inavyosema na wala sio kupiga watu.
Vurugu zote zinaanzia na mambo madogo kwa kuwatumia hao vijana wasio na kazi mitaani, mwisho wake ni nchi nzima kuangamia. Lazima tulaani vurugu zozote zile.
Hapa sasa wewe unaleta siasa za kuku na mayai nani alianza! Unajua ukitaka wananchi waheshimu sheria inabidi kwanza Serikali ya CCM (I mean CCM) waheshimu sheria. What do you expect kwenda kushitaki Mtikila wakati unaona kabisa huko mahakamani ni mbali na sheria zetu ni kupoteza muda na fedha! Wake up; CCM and the executive government have a problem, and this will cost this nation. Believe me nchi hii Rais hadi mtu wa chini hawaheshimu sheria, ndiyo maana unaona haya yanatokea.
Mtanzania ukitaka nidhamu iwepo kwanza anza juu ndiyo uwaseme hao wa-chini, wake-up!
Yule mchungaji matata anayeitwa Mtikila, hivi pundwe amepelekwa hospitali kulazwa na kushonwa nyuzi baada ya kupigwa mawe na wananchi wenye hasira. Mtikila alipata dhahama hiyo baada ya kuhutubia kuwa Mbowe na CHADEMA yake ndio waliomuua Chacha Wangwe.
.......ndiyohiyo
Magabe,
Humu mtandaoni tupo watu wa taaluma mbalimbali na uelewa wetu wa mambo pia ni tofauti. Gold Cyadination ni process inayoeleweka vizuri sana pamoja na madhara yake. Na pia CN haichukui muda kuleta madhara ya kiafya kwa mtu. K.m. maji kiasi ya kijiko cha chai yenye 2% ya CN inaweza ikaondoa roho ya mtu.
Sasa kama kweli ushahidi mkubwa upo wa matumizi mabaya ya CN na kumwagwa kwenye vyanzo vya maji, basi ulete ili tujenge hoja ya kuwaadhibu hao wachimbaji. Lakini kama hakuna, basi tuachane na porojo za mitaani. Kuamini au kutoamini 'system', ni position ya kuchukua kulingana na hoja, lakini tukumbuke pia kuwa, ni rahisi sana kujenga uzushi.
mimi nafikiri tunakuza maneno
Polisi hawakudhibiti nini jamani? kama angepondwa pondwa mawe hapo sawa .Lakini jamaa amevizia Mtikila kageuka upande mwingine kampa la kichwa hii ni ishara ya kuwa mtu huyu kutumwa.
Kama angepandwa ghadhabu wakamshambulia hapo sawa,lakini mtu huyu kamvizia .
Pole sana mzee wetu Mtikila, mzee wa "kulipua mabomu". Hiyo ni ajali ya bomu kumlipukia mlipuaji. Uwe mwangalifu wakati mwingine....
Lakini kwanini akina SLaa na wengineo wanaotajwa na Mtikila kuwa ndio waliopanga mauaji ya Wangwe hawachukui hatua za kisheria?Na hapa by "hatua za kisheria" simaanishi kwenda kushtaki polisi bali kumpeleka mahakamani moja kwa moja?Slaa na wenzake walipotoa list of shame,watajwa walitishia kwenda mahakamani na hawakwenda,na hivyo kututhibitishia kwamba tuhuma zote dhidi yao zilikuwa za kweli.Wakati mwingine kukaa kimya unapotuhumiwa kunaweza kumpa jeuri mtoa tuhuma kuendelea kumwaga tuhuma zaidi.Unadhani leo Mtikila angediriki kuongea hayo iwapo akina Slaa wangechukua hatu mara baada ya ile press conference ya kuwatuhumu na mauaji ya Wangwe?Kipigo alichopata kinaweza kuwa solution ya muda mfupi tu lakini ukweli ni kwamba huyu mtu alipaswa apandishwe kizimbani kuthibitisha tuhuma zake.
Mzee Mwanakijiji,
I hope unaelewa siasa. Kama unaelewa basi utajua siasa si mahakamani.
Leo FIFA wamewaadhibu Croatia kwa chants za Monkey dhidi ya mchezaji wa UK, kwanini wasiwaajibishe hao waliokuwa wanatoa hayo maneno ya kashfa badala ya kuiadhibu nchi? Chama cha siasa kinakuwa judged sio kwa matendo ya viongozi wake tu bali hata matendo ya washabiki wao.
.
Basi hizi ni siasa za kitoto I may say. Pamoja na kuwa Mtikila anaweza kutofautiana nao CHADEMA sioni sababu ya wao kufurahia yeye kupigwa mawe.
Shame on their bones (whomever celebrates Mtikila's stoning).
🙁
Basi hizi ni siasa za kitoto I may say. Pamoja na kuwa Mtikila anaweza kutofautiana nao CHADEMA sioni sababu ya wao kufurahia yeye kupigwa mawe.
Shame on their bones (whomever celebrates Mtikila's stoning).
🙁
of course huwezi kupata kwa sababu unaangalia suala hili kwa mwanga wa itikadi za chama badala ya kuona uhalifu uliotendeka na kuukataa. Ukishavuka huo mtazamo wa chama utaona kuwa uhalifu usizoelewe kukubalika, au hata kufafanuliwa bali ni lazima ushughulikiwe.
Mtikila hakustahili kipigo hicho na kama alivyosema na mimi niliashiria hapo juu ni kuwa Polisi wanawajibika moja kwa moja hasa kama alitoa taarifa za kuwa kuna mipango ya kitu kama hicho. Pamoja na hayo kila mtu awajibishwe kwa maneno yake na vitendo vyake, mtu akinitukania mama yangu kuna level ya matusi ambayo naweza kumuambia "bwana, mweke mama yangu pembeni" akiendelea nikimshindilia ngumi na kumvunja meno nitakuwa nimekosea; lakini atakuwa amejitakia kwa sababu nilishamwambia asinitukanie mama yangu.
Mambo ya kuchezea vionjo vya watu au hisia zao ni mabaya sana and should not be taken for granted. Tunaona jinsi gani Rwanda the flames of hatred were fueled by maneno ya kichochezi na kuita watu "cockroaches" n.k Tumeyaona maneno yakitumika kuwasha moto wa kisasi Iraq, Palestina, Israeli na hata katika historia ya Marekani during the civil rights movement.
Kama huoni uzito wa matumizi ya maneno na nguvu ya "spoken word' sijui itakutaje. Get over your politics na uone kuwa siasa za vitisho, uchochezi, hazina nafasi. Lazima watu warudi kwenye "hoja hujibiwa kwa hoja".
But, of course, huwezi kufanya hivyo kwa sababu kwako ni siasa na siasa tu.
Kusema mtu amemuua mwingine ni kosa la jinai. Mwenye wajibu wa kufungua kesi ni jamhuri. Sio Mbowe, Mengi, Slaa, Mnyika wala Zitto. Hivyo, polisi wamkamate Mtikila.
HIYO SIO MARA YA KWANZA KWA YEYE KUTOA TUHUMA KAMA HIZO HUYO KICHWA CHAKE KIMEPIGWA SANA SASA AMESHACHOKA HANA UWEZO WA KUFIKIRIA KAMA BINADAMU WA KAWAIDA , APELEKWE AKAPIMWE AKILI KWANZA
2. Kusema kwamba asishushwe jukwaani apelekwe mahakamani nayo ni kituko kwa kuwa akishtakiwa leo kesi itaisha mwaka 2009 wakati uchaguzi wa Tarime ni Oktoba 12 mwaka 2008.
UNA UHAKINA NA UNAYOSEMA ? HATA IKIISHA MWAKA 3000 SI USHAHIDI BADO HAUJAKAMILISHWA ?
Huyu ndiye Mtikila, aliyefungwa jela kwa kusema CCM wamemuua Kolimba na aliyeshtakiwa kwa kuita maiti ya Nyerere kuwa ni MZOGA
HUKO JELA WALIMGONGA SANA KICHWA CHAKE KAMA MORGAN WA ZIMBABWE HANA AKILI SAWA HUYU TUSIHANGAIKE NAE