Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Mwananchi
My Take:
Usiharakishe kuhukumu na kubebesha watu lawama.
MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila jana alidai kuwa waliomjeruhi juzi ni wanachama wa Chadema, lakini jana kada mmoja wa CCM na wanachama wanne wa DP walifikishwa mahakamani kwa kosa la kumshambulia mwanaiasa huyo matata.
Mtikila, ambaye anasifika kwa kutoa tuhuma nzito dhidi ya mtu yeyote bila ya woga, alitunguliwa kichwani na jiwe wakati akitoa tuhuma kuwa Chadema inahusika katika mauaji ya mbunge wa zamani wa Tarime, Chacha Wangwe, wakati akihutubia mkutano wa hadhara. Shambulizi hilo lilisababisha Mtikila kukimbizwa hospitalini ambako alishondwa nyuzi saba kichwani.
Akizungumza na waandishi wa habari hotelini jana Mtikila alisema baada ya kupatiwa matibabu na kwenda kituo cha polisi alikuta watu tofauti wamekamatwa kuhusika na shambulio hilo baada ya kubaini kuwa wengi wao ni wafuasi wa chama chake.
''Kama nilivyoeleza jana, hawa polisi wanataka kuvuruga kesi yangu kwa lengo la kuilinda Chadema," alisema Mtikila. "Walionipiga mawe si hao waliokamatwa. Ninawajua, mmoja sawa, lakini wengine sio. Wamekamata wanachama wangu na sasa wanataka kunifanya kuamini kuwa wanachama wangu wamehusika.''
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Oparesheni Maalum, Venance Tossi watu waliohusika na kufanya shambulio hilo la mawe katika mkutano huo ni Musa Petro (4, Afidhi Stanislaus, Mwita Chacha, Mwita Kyaongo pamoja na Selema William.
Kuhusu madai ya Mtikila kuwa waliokamatwa si wale waliohusika na shambulio hilo, Kamanda Tossi alisema anachoamini yeye ni kuwa waliokamatwa ndio waliohusika na tukio hilo.
''Wamekamatwa jana katika eneo la tukio, na leo wamefikishwa mahakamani, sasa kama waliokamatwa sio wenyewe hilo ni suala lake Mtikila,'' alieleza na kisha akakata simu.
Habari zaidi zimeeleza kuwa Musa Petro, ambaye ni mmoja wa watu waliokamatwa, ametambuliaka kuwa ni balozi wa nyumba kumi wa CCM na kwamba wengine waliobaki ni wanachama wa DP inayoongozwa na mchungaji huyo wa kanisa la ufufuo.
Watu watano wanaosadikiwa kumshambulia Mchungaji Mtikila wamefikishwa mahakamani jana katika kesi namba TAR /IR/ 3419 /08.
Wakati watu watano wakifikishwa kortini kwa tuhuma za kumshambulia Mtikila, wananchi wameelezea kipigo hicho kuwa ni fundisho kwa wanasiasa ambao wameshindwa kunadi sera za vyama vyao na badala yake kuchochea mgawanyiko kwa kutumia kifo cha aliyekuwa mbunge wao Chacha Wangwe.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wananchi waliozungumza na Mwananchi walisema kuwa sababu iliyomfanya Mtikila apigwe na jiwe na kujeruhiwa kichwani ni sawa na ile iliyomfanya Dk. Sengondo Mvungi wa chama cha NCCR-Mageuzi kushambuliwa.
Mmoja wa wakazi wa mji wa Tarime, Ambrosi Wantaigwa alisema kuzungumza suala la kifo katika ajenda ya uchaguzi kumekuwa kukiwaumiza wananchi wa Tarime na hivyo kuwataka wanasiasa kuepuka jambo hilo.
''Hili ni jambo linaloumiza sana kama serikali ilishatangaza awali kuwa ni ajali, familia haikuridhika nayo ikaitisha watalaam wake na kufanya uchunguzi na kudhihirika kuwa ni ajali, unawezaje kusimama jukwaani kututangazia mambo kama hayo. Kama unadhani unao ushahidi, jukwaa si mahala pake, peleka polisi,'' alieleza.
Naye Mchungaji Nicodemas alisema kuwa Mtikila akiwa mchungaji mwenzake alitenda kosa ambalo kimantiki linapingana na maandiko matakatifu, kwa vile kwa kauli zake zinapanda mbegu za chuki na uchochezi.
''Kabla ya kutamka hayo alipaswa kujiuliza kwanza mara mbili, kwa sababu wananchi wa Tarime bado wana uchungu wa kifo cha mbunge wao ambaye walimpenda sana.Ukishindwa kutofautisha jambo, kama biblia inavyoeleza kuwa kila jambo kwa wakati wake, basi hayo ndiyo matokeo yake,'' alieleza mchungaji huyo.
My Take:
Usiharakishe kuhukumu na kubebesha watu lawama.