Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.

Mtanzania
Mmiliki wa gazeti la majira ni Richard Nyaulawa. Natumaini unamfahamu.

Kama wewe ni msomaji mzuri wa hili gazeti mpaka miaka hii, mmmhhhh! Inakuwa sawa na mtu anayedai kuwa msomaji mzuri wa gazeti la Rai. Rai na Majira yote yamebakwa na mafisadi wa CCM na kubakia majina tu.

Kama mhariri wa Rai (aliyepita?) bwana Balile anaonekana ni mganga njaa, huyo ni cha mtoto kwa mhariri wa Majira, by the name of Kulangwa (if not mistaken).

Mimi binafsi nilikuwa msomaji mzuri wa Rai na Majira miaka ya mwanzo ya tisini na kati kati. No more. Sorry kwa kuwatoa nje ya mada husika.
 

People's power at work! Safi sana wananchi wa Tarime,hakuna kulala mpaka kieleweke.

Revolution Forever!
 



Ushauri wangu kwa Dr. Slaa ni kuwa, taifa linakutegemea sana labda kuliko kiongozi mwingine yeyote wa upinzani. Kwa hiyo ningekushauri tena na tena, kama chama, wewe binafsi, Mbowe n.k, mmekosea jambo, ni vema usiliongelee kama huna majibu uliyofikiria kwa busara, maana kinyume na hivyo, unapofungua kinywa unazidisha kuboronga na kuharibu hadhi yako.
 
Mkuu,

Dr.Slaa ni kiongozi ambae hana tabia au mazoea ya kukimbia matatizo kama walivyo viongozi wengine ndani ya CCM.Yeye ni mtu wa kutoa maelezo ili kuweka fact straight,jambo ambalo ni msamiati kwa viongozi wengi wa CCM
 

Invicible,

Asante, kwa kweli nilikuwa sijui nani anamiliki hilo gazeti. Labda kwasababu mimi sijali sana mmiliki au mwandishi labda kama kuna matatizo. Naangalia kinachoandikwa. Hata RAI niliacha kusoma kabla hata ya kujua limeuzwa, nilifikiri waandishi tu wameshusha kiwango.

Mimi magazeti ninayosoma ni Majira, Mwananchi na mwanahalisi kwa Jumatano. Ya Kiingereza thisday, the citizen, daily news na Guardian. Najua mmiliki wa daily news na guardian. Nahisi thisday ni la Mengi. Sijui nani wenye mwananchi na Mwanahalisi na pia nilikuwa sijui Majira ya nani. Labda tunatofautiana, mimi sijali kabisa mmiliki ni nani, hata editors wa hayo magazeti siwajui japo nayasoma kila siku. Niko more interested kwenye contents za hayo magazeti kuliko kwenye nani anandika.

Richard Nyaulawa namfahamu kiasi japo sio sana, si ni yule mbunge wa Mbeya vijijini? Kabla ya 2005 aliwahi pata zawadi ya Mwana Mbeya bora. Sijui alifanya nini mpaka kupata hiyo zawadi. Baada ya hapo ameingia bungeni sijawahi kumsikia tena bungeni na hata kwenye siasa za Mbeya, nafikiri anatajwa mara chache sana. Nilikuwa najua huko nyuma alikuwa Business Times.

Kitu ambacho nina uhakika nacho, hata kama gazeti ni la fisadi mimi nitasoma tu ili mradi contents zake ziwe zinafaa. Kama ni propaganda basi huko sitakaa mara nyingi. Ni sawa na Tanzania Daima, kama ni jambo ambalo sio la siasa, mimi nasoma maana wana waandishi wazuri lakini kwenye siasa hapana. Nilikuwa nasoma huko nyuma Mtanzania, lakini nao sasa nimeacha maana contents zao zimeshuka kiwango. Nilianza kusoma RaiaMwema lakini kadri muda unavyoenda naona kama uchunguzi wao sio makini. Mwanahalisi wana kura yangu kwa gazeti za Jumatano.

Watu wengine tumesoma hata vitabu vya Manazi, je nakubaliana nao? Hapana, ukitaka kuelemika lazima usome maandiko hata ya watu ambao hukubaliani nao. Kuna cheap propaganda, hizo ndio hazifai hata kusoma maana ndani yake huwezi kujifunza kitu.
 

Spinning at work....
 
Hivi Mariamu alihidhuria mazishi ya Wangwe kule Kemakorere?
 

Haya! We unaamini maneno ya MNEC wa CCM Profesa Wangwe kumuita Dr Slaa muongo, MNEC ambaye alisema haridhiki kuwa marehemu alikufa kwa ajali; mpaka post mortem nyingine, ikafanyika ya pili Prof Wangwe, Zitto na Mariam Wangwe wote wakishuhudia kwa macho yao. Wote wakatoka wameridhika kuwa ni ajali halafu mara baada ya kuzika MNEC huyo huyo na Mariam huyo huyo wanaibuka wakisema kuwa haikuwa ajali wanataka uchunguzi wa tatu! Hapo sinafanyika siasa za UCCM tu na jimbo la Tarime, we hushangai kwa nini wake wengine wa marehemu wanakuja Dar es salaam kuchukua watoto wao toka kwa huyo mwanamke?

Hebu niambie we Kubwa JINGA JINGA dr Slaa kakosea nini kati ya aliyoyasema yote? Nionyeshe japo moja tu!

Asha
 
Hivi Mariamu alihidhuria mazishi ya Wangwe kule Kemakorere?

Alihudhuria. Lakini nasikia wake wawili walikataa asishiriki, mpaka wazee waliposuluhisha. Ndio maana arobaini zikawa mbili, ya Dar e salaam ya Mariam na Wangwe ambaye si baba mmoja na mama mmmoja na marehemu. Ni mandugu tu katika ukoo. Halafu kukawa na arobaini nyingine huko kemakorere ya wake wakubwa za marehemu na ndugu zake wa karibu zaidi. CHADEMA wakashiriki kwa karibu zaidi arobaini kule Tarime, arobaini ya Dar es salaam wakawatuma wabunge wao wa viti maalum kwa kuwa chama kilikuwa katika kikao cha kamati kuu.

Asha
 

Asante kwa kufafanua. Nilitaka kushangaa sana, maana kama familia wanamtambua na ndiye alikuwa anakaa na watoto wote wa marehemu, ingelikuwa kitu cha ajabu kutoenda kwao kumzika bwanake.

Msiba hata koo zingine watu wanafanyia sehemu mbalimbali ila kwenye mazishi wote lazima wawepo labda kama kuna sababu kubwa sana.
 


Familia ya Dar es salaam ambayo sio tumbo moja na marehemu ndio inamtambua. Familia ya Tarime ambayo ni tumbo moja na marehemu haimtambui. Ameanza kukaa na watoto tisa baada ya marehemu kufariki hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari. Sio kabla, sasa tujiulize ni kwanini amewachukua watoto sasa hivi?

Asha
 
Asha Abdala,

Unasema kwa uhakika maanake nilivyosikia mimi tofauti kabisa....
Kifupi ni kwamba Marium hatambuliwi na ujio wake ungezua matatizo makubwa. Nakuomba kitu kimoja unifahamishe kama unajua, inakuwaje wake wengine wote wanatambuliwa na familia ya marehemu isipokuwa huyu kuna tatizo gani ikiwa Marehemu alikuwa na wake wengi.
 

Mkandara,

Mbona hata yule mke mwingine aliyehojiwa ni kama anamtambua huyu mama?

Kwa mila za Kiafrika kama prof. Wangwe ambaye nafikiri ndiye mkuu wa hiyo familia anamtambua, basi huyo anatambuliwa na ukoo. Sio lazima hao wanawake wengine wamkubali maana wanashindania bwana.

Ila Wangwe naye, karne ya 21 na wake watatu? Ndio maana tunaendelea kuwa maskini. Wabunge ndio walitakiwa kuongoza mabadiliko kwa kupinga mambo yanayotukwamisha. Sasa watoto wote hao, nani atawasaidia na kuwaendeleza?
 

Stevin Wasira aka Tyson anawake 5 watoto Lukuki unashangaa nini mkuu!! watu wanafata jadi...King Mswati nadhani ni balaaa
 
very good question........it deserve a good answer. maana tunashidwa kuelewa issue ni mapungufu ya media au ni swala la siasa chafu za vyama huko tarime?? au issue ni rushwa kwa wandishi! what is the point....?tusaidiane ili twende sawa

You'd have to say that, overall, it's all of the above.

1.Kwamba, hizi ni siasa chafu za CCM kutaka kuvuruga amani Tarime kwa ku-inject suala la mapigano ya kikabila/koo baina ya wanatarime ili mradi tu washinde uchaguzi.

2:Kwamba, hili ni suala la uandishi mbovu wa habari. Habari nyingi zinazoandikwa kuhusu Tarime, ukichunguza kwa makini, waandishi wake ni "toka Jijini". Toka Jijini? Plus, utakuta suala la uharifu limetendeka serengeti [ambayo ni wilaya/jimbo tofauti], ama Shirati, lakini headlines zinasomeka "Risasi zavuma Tarime...," "Tarime hakukaliki..." C,mon, people! Hamuoni kuwa hizi ni njama za kutaka kuipaka Tarime matope?

3:kwamba, CCM haikubaliki Tarime. So, kitu wanachojaribu kufanya sasa hivi ni ku-create narratives kwamba kuna mapigano ya kikabila/koo ili wakishindwa, wakate rufaa mahakani na kutengua matokeo ya uchaguzi.

4:Wanatumia trick kuwa kuna mapigano ya kikabila/koo [ambayo hayapo], ili kushinikiza serikali imwage askari wengi mitaani/vijijini/tarafani, ambao, in turn, watatumiwa na CCM ku-intimidate wapiga kura na kusababisha wengi wakate tamaa ya kupiga kura. Maana sasa hivi ukisema anything kuhusu CCM, wewe ni mchochea vurugu, hivyo unakamatwa na kuswekwa ndani. The real question then remain: where's the freedom of speech?

5:Wanatumia visingizio vote hivyo ili waibe kura kirahisi: Nitakupeni mfano hapa: Mwaka 1995 na 2000, NCCR-MAGEUZI walishinda chaguzi zote mbili lakini CCM kama kawaida yao wakaiba kura. Then, ilipofika mwaka 2005, wananchi wa Tarime wakawa wameshtukia diri. Wakaamua kuwa watapiga kura, then wakishamaliza, watakaa vituo mpaka kura zote zitakapohesabiwa na matoke yametangazwa. CCM hawakupata fursa ya kuiba kura mwaka 2005. Matokeo yake: Marehemu Wangwe (CHADEMA) akaibuka mshindi. So now, CCM wanachotaka kufanya ni kujenga hizi narratives za "mapigano" ili wananchi wakitaka kudhibiti kura zisiibiwe kama walivyofanya mwaka 2005, CCM waseme, "ah! ona, wanataka kuvamia vitu vya kura..., wanataka kufanya fujo hawa...," then FFU waitwe, kisha wananchi watawanywe kwa nguvu, then kura ziibiwe kirahisi. It's that simple people. Kama mnataka kuendelea kubisha, bisheni tu...

So ujumbe wangu kwa wale wote mnaojifanya kuwa hamjui njama za CCM, at some point, you need to come to your sense and realize that this is a dirty game ambayo CCM kwa kushirikiana na vyombo vya habari wana-attempt kufanya ili kuhakikisha kuwa wanachukua jimbo la Tarime. Na kwa wale tuliobahatika kuishi Tarime, hili tunalifahamu na tunachojaribu kuwaeleza hapa ni kweli tupu.

P.S. simnajua wananchi vijijini wanavyoogopa askari?
 
Yote yanatokea Tarime; vurugu, mapigano, uchochezi, kupakaziana, uandishi wa kupotosha. Kuna yanayotokea kwa bahati mbaya na kuna yanayotokea kwa kupangwa kama sehemu ya kampeni za kisiasa.
Kama kupigana hawa ndugu wamekuwa wakipigana kwa muda mrefu, hakuna sababu yoyote itakayowafanya wawe wameacha kupigana hivi sasa. Kwenye kampeni za kisiasa, kunakuwa na kila aina ya kupakaziana ili kutafuta milage kwa wapiga kura.
Ni juu ya anayesikia na kusoma kupima na kuamua akiamini nini
 
Katika kuzungumzia suala la Tarime tusije kuficha vichwa vyetu kwenye mchanga kama Mbuni. Kwamba kukana kabisa na kwa uhakika kuwa hakuna vurugu kwenye baadhi ya sehemu au kwenye mikutano fulani ni kukana ukweli. Kwamba mambo ni "shwari" ni kujilaghai. Vinginevyo mtu ataelezea vipi nundu ya Mtikila? itaelezewa vipi kifo cha mtu aliyepigwa risasi?

Upande mwingine pia bado ni kweli habari za Tarime sijui kama zinaripotiwa kwa ukweli wote maana katika mapambano kama haya ya kisiasa mhanga wa kwanza kabisa ni ukweli. Uamuzi wa mtu mzima ni kupima kila unachosoma na kusikia na kuamua wewe mwenyewe ni kipi kinakaribiana na ukweli zaidi. Ndio maana sisi wengine tumelilia picha za huko Tarime na ukiondoa picha ya makarandinga yaliyopaki na kipigo cha Mtikila na huyo bwana aliyekamatwa akiuza shahada hakuna ushahidi wowote wa vurugu kubwa, machafuko makubwa, n.k Zaidi tunavyosikia ni vijembe vya kisiasa na kushutumiana.

Kukosekana kwa ushahidi huo wa picha n.k hakumaanishi kuwa hali ni shwari; lakini kwa kadiri mambo yanavyokwenda tutaweza kupata habari za ndani kabisa kwani KLHN imeshapeleka 'nzi" wake huko Tarime maana haya ya kusubiri kusimuliwa na kuambiwa wakati mwingine yanaua ukweli wenyewe.
 



Mkuu,

Ila sasa hapo ni suala la mada nyingine.Ili tuanze kuwachambua wabunge woore wenye wake wengi na wenye mahawara ili tuchambue kiini cha umaskini wetu.Kama tu ni lazima sana
 
Mtanzania,
Ni kweli hata yule mke wa pili anamtambua Marium lakini haiwezi kuhalalisha kwamba anatambuliwa na familia ya Wangwe...Binafsi kama Dr. Slaa anatakiwa kuomba msamaha basi tuanze na familia ya Wangwe wanatakiwa kuomba msamaha kisha tuone kama atasimama...

Mkuu hili swala linapikwa tu, iweje huyu Marium baada ya yote yaleyokwisha tokea leo aje na habari hii mpya ya Arobaini.. I mean kuna kitu gani muhimu sana kuwafanya viongozi wa Chadema wahudhurie Arobaini nyumbani kwake!..I mean what is the deal na hiyo arobaini hasa ikiwa tunaona nyumba za marehemu Dodoma, Mwanza, Tarime na Dar.
kwa nini tusiwalaumu familia kwa kuweka hizi arobaini nyumba mbili.. Je, kama viongozi wa Chadema wangekwenda Dar wakaacha kwenda Tarime mngesema nini?..
Jamani huyu mwanamke na wote wanaompandisha chati wana lao jambo...
 
Mkuu Mkandara,

Maneno makuu hayoo.I salute you bro
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…