very good question........it deserve a good answer. maana tunashidwa kuelewa issue ni mapungufu ya media au ni swala la siasa chafu za vyama huko tarime?? au issue ni rushwa kwa wandishi! what is the point....?tusaidiane ili twende sawa
You'd have to say that, overall, it's all of the above.
1.Kwamba, hizi ni siasa chafu za CCM kutaka kuvuruga amani Tarime kwa ku-inject suala la mapigano ya kikabila/koo baina ya wanatarime ili mradi tu washinde uchaguzi.
2:Kwamba, hili ni suala la uandishi mbovu wa habari. Habari nyingi zinazoandikwa kuhusu Tarime, ukichunguza kwa makini, waandishi wake ni "toka Jijini". Toka Jijini? Plus, utakuta suala la uharifu limetendeka serengeti [ambayo ni wilaya/jimbo tofauti], ama Shirati, lakini headlines zinasomeka "Risasi zavuma Tarime...," "Tarime hakukaliki..." C,mon, people! Hamuoni kuwa hizi ni njama za kutaka kuipaka Tarime matope?
3:kwamba, CCM haikubaliki Tarime. So, kitu wanachojaribu kufanya sasa hivi ni ku-create narratives kwamba kuna mapigano ya kikabila/koo ili wakishindwa, wakate rufaa mahakani na kutengua matokeo ya uchaguzi.
4:Wanatumia trick kuwa kuna mapigano ya kikabila/koo [ambayo hayapo], ili kushinikiza serikali imwage askari wengi mitaani/vijijini/tarafani, ambao, in turn, watatumiwa na CCM ku-intimidate wapiga kura na kusababisha wengi wakate tamaa ya kupiga kura. Maana sasa hivi ukisema anything kuhusu CCM, wewe ni mchochea vurugu, hivyo unakamatwa na kuswekwa ndani. The real question then remain: where's the freedom of speech?
5:Wanatumia visingizio vote hivyo ili waibe kura kirahisi: Nitakupeni mfano hapa: Mwaka 1995 na 2000, NCCR-MAGEUZI walishinda chaguzi zote mbili lakini CCM kama kawaida yao wakaiba kura. Then, ilipofika mwaka 2005, wananchi wa Tarime wakawa wameshtukia diri. Wakaamua kuwa watapiga kura, then wakishamaliza, watakaa vituo mpaka kura zote zitakapohesabiwa na matoke yametangazwa. CCM hawakupata fursa ya kuiba kura mwaka 2005.
Matokeo yake: Marehemu Wangwe (CHADEMA) akaibuka mshindi. So now, CCM wanachotaka kufanya ni kujenga hizi narratives za "mapigano" ili wananchi wakitaka kudhibiti kura zisiibiwe kama walivyofanya mwaka 2005, CCM waseme, "ah! ona, wanataka kuvamia vitu vya kura..., wanataka kufanya fujo hawa...," then FFU waitwe, kisha wananchi watawanywe kwa nguvu, then kura ziibiwe kirahisi. It's that simple people. Kama mnataka kuendelea kubisha, bisheni tu...
So ujumbe wangu kwa wale wote mnaojifanya kuwa hamjui njama za CCM, at some point, you need to come to your sense and realize that this is a dirty game ambayo CCM kwa kushirikiana na vyombo vya habari wana-attempt kufanya ili kuhakikisha kuwa wanachukua jimbo la Tarime. Na kwa wale tuliobahatika kuishi Tarime, hili tunalifahamu na tunachojaribu kuwaeleza hapa ni kweli tupu.
P.S. simnajua wananchi vijijini wanavyoogopa askari?