Mtanzania,
Ni kweli hata yule mke wa pili anamtambua Marium lakini haiwezi kuhalalisha kwamba anatambuliwa na familia ya Wangwe...Binafsi kama Dr. Slaa anatakiwa kuomba msamaha basi tuanze na familia ya Wangwe wanatakiwa kuomba msamaha kisha tuone kama atasimama...
Mkuu hili swala linapikwa tu, iweje huyu Marium baada ya yote yaleyokwisha tokea leo aje na habari hii mpya ya Arobaini.. I mean kuna kitu gani muhimu sana kuwafanya viongozi wa Chadema wahudhurie Arobaini nyumbani kwake!..I mean what is the deal na hiyo arobaini hasa ikiwa tunaona nyumba za marehemu Dodoma, Mwanza, Tarime na Dar.
kwa nini tusiwalaumu familia kwa kuweka hizi arobaini nyumba mbili.. Je, kama viongozi wa Chadema wangekwenda Dar wakaacha kwenda Tarime mngesema nini?..
Jamani huyu mwanamke na wote wanaompandisha chati wana lao jambo...
Stevin Wasira aka Tyson anawake 5 watoto Lukuki unashangaa nini mkuu!! watu wanafata jadi...King Mswati nadhani ni balaaa
Mkandara,
Mbona hata yule mke mwingine aliyehojiwa ni kama anamtambua huyu mama?
Kwa mila za Kiafrika kama prof. Wangwe ambaye nafikiri ndiye mkuu wa hiyo familia anamtambua, basi huyo anatambuliwa na ukoo. Sio lazima hao wanawake wengine wamkubali maana wanashindania bwana.
Ila Wangwe naye, karne ya 21 na wake watatu? Ndio maana tunaendelea kuwa maskini. Wabunge ndio walitakiwa kuongoza mabadiliko kwa kupinga mambo yanayotukwamisha. Sasa watoto wote hao, nani atawasaidia na kuwaendeleza?
Mkandara,
Mbona hata yule mke mwingine aliyehojiwa ni kama anamtambua huyu mama?
Kwa mila za Kiafrika kama prof. Wangwe ambaye nafikiri ndiye mkuu wa hiyo familia anamtambua, basi huyo anatambuliwa na ukoo. Sio lazima hao wanawake wengine wamkubali maana wanashindania bwana.
Ila Wangwe naye, karne ya 21 na wake watatu? Ndio maana tunaendelea kuwa maskini. Wabunge ndio walitakiwa kuongoza mabadiliko kwa kupinga mambo yanayotukwamisha. Sasa watoto wote hao, nani atawasaidia na kuwaendeleza?
Kwa kweli mnapotosha alichokisema Dr Slaa, kwa aliyesikiliza TBC1 tafadhali atuwekee hapa. Maana wengine tukiweka tutaonekana tunamtetea tu kipenzi chetu Dr Slaa.
Halafu Prof Wangwe sio msimamizi wa mirathi ya Chacha Wangwe, ni kimbelembele chake tu kinamtuma kuwa msemaji wa familia. Na mtaona kwenye arobaini hata msemaji hakuwa yeye.
Asha
Dada Asha,
Kuwa mkuu wa familia ni tofauti na kuwa msimamizi wa mirathi. Sijui sehemu zingine lakini kule kwetu sisi, mkuu wa familia ndio anaamua mambo yote yanayohusiana na misiba, of course anashauriana na wengine pia.
Haya mambo ya sio mama mmoja au baba mmoja hayana maana kabisa. Ukoo ni mkubwa kuliko mtu mmoja mmoja. mkianza kutenga watu hata kwenye koo sijui mtaishia wapi.
Hivi huko Zanzibar inaelekea mnabaguana sana kwi kwi kwi!!
CCM: Ruksa kutumia kifo cha Wangwe kisiasa
2008-09-30 11:36:47
Na Simon Mhina
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni `ruksa` ndugu wa Marehemu Chacha Wangwe kutumia jukwaa la kampeni za Chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Tarime kuzungumzia hisia zao juu ya mazingira ya kifo cha ndugu yao.
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Pius Msekwa alisema ndugu hao wana haki kuzungumzia kifo hicho kwenye jukwaa la CCM kwani hizo ndizo haki za binadamu.
Akifafanua, mwanasiasa huyo alisema ndugu hao ukiwaondolea jukwaa la siasa, hawana sehemu nyingine ya kusema, kutoa dukuduku zao na kuonyesha hisia zao.
Msekwa ametoa kauli hiyo akijibu malalamiko ya viongozi wa Chadema kwamba baadhi ya vyama vimekigeuza kifo cha Wangwe kuwa mtaji wa kisiasa katika uchaguzi huo.
``Jamani nyie hamfahamu haki za binadamu, wale wana madukuduku yao, lakini wamekosa mahali pa kusemea, wanapopanda kwenye majukwaa yetu wanaona hiyo ni sehemu muafaka, ruksa hatuwezi kuwazuia,`` alisema.
Hata hivyo, Msekwa alisema wanaolalamikia kifo cha Wangwe sio CCM, bali ndugu zake.
Alisisitiza kwamba nchi yetu imetoa uhuru wa kujieleza kwa kila mwananchi, ili mradi asivunje sheria, hivyo wanachokifanya ndugu wa Wangwe ni sahihi.
``Kwa mfano juzi nimesikia mjane wa marehemu yeye akitumia jukwaa la vyombo vya habari kutoa hisia zake mbona hakunyimwa? Kwa hiyo na sisi hatuwezi kuwanyima fursa hiyo kama wanataka,``alisema.
Alipoulizwa kama haoni suala hilo ni sawa na uchochezi, Msekwa alisema mtu kudai kwamba haelewi mazingira ya kifo cha marehemu wake kilivyotokea sio uchochezi.
``Tutaendelea kuwakaribisha ndugu wa Wangwe kwenye mikutano yetu na hatuwezi kuwapangia cha kuzungumza,``alisema.
Alisema wameamua kufanya hivyo, kwa vile ndugu wa marehemu wamejirizisha kwamba kifo hicho kilijaa utata.
Pia alisema malalamiko kama hayo hayakuanzia kwenye jukwaa la CCM, bali kwa kaka wa Marehemu huyo Profesa Wangwe.
Kuhusu mwenendo wa kampeni, Msekwa alisema hakuna vitisho vyovyote vinavyotolewa na Polisi na hao wanaodai kuna askari `wamemwagwa` hawaelewi mambo.
Alisema vikosi vya askari vilivyomwagwa ni kwa ajili ya kuwalinda wananchi na mali zao na kuwa amini dhidi ya wezi wa ng`ombe.
``Unajua huku kuna wezi wa Ng`ombe na mapigano ya koo, hivyo lazima polisi wawe wengi,``alisema.
Alipoulizwa kama Polisi wamemtuma atoe msimamo huo, Msekwa alisema tataribu za Polisi ziko wazi, hawawezi kuletwa sehemu kwa nia ya kuvuruga, bali kulinda amani.
Alisema raia wema hawana sababu yoyote ya kuogopa Polisi.
SOURCE: Nipashe
Naona umeamua kujinukuu...An idiot called Msekwa! Kwake yeye wanaosema sio CCM wakati anajua kabisa wanapanda majukwaani kusema ni Keba Wangwe kiongozi mwandamizi wa CCM, Profesa Wangwe Mjumbe wa NEC CCM na Mariam Wangwe kada wa CCM aliyeolewa na mbunge wa CHADEMA. Hivi bado wanatuaminisha kwamba hapa kuna ufamilia tu hakuna UCCM hapo! Huyu Keba aliyemfunga jela Chacha na Prof Wangwe aliyemtenga Chacha kwa kumuita muhuni na mpinzani leo ndio familia ambayo inapewa 'hisani' kutumia jukwaa la CCM kufikisha kilio chao! Ama kweli, ukistaajabu ya Makamba utaona ya Msekwa.
Asha
Naona umeamua kujinukuu...