Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Mwanakijiji,

Huyu nzi wa KLHnews akirudi usisahau kutuhabarisha.
 
Mtanzania,
Ni kweli hata yule mke wa pili anamtambua Marium lakini haiwezi kuhalalisha kwamba anatambuliwa na familia ya Wangwe...Binafsi kama Dr. Slaa anatakiwa kuomba msamaha basi tuanze na familia ya Wangwe wanatakiwa kuomba msamaha kisha tuone kama atasimama...

Mkuu hili swala linapikwa tu, iweje huyu Marium baada ya yote yaleyokwisha tokea leo aje na habari hii mpya ya Arobaini.. I mean kuna kitu gani muhimu sana kuwafanya viongozi wa Chadema wahudhurie Arobaini nyumbani kwake!..I mean what is the deal na hiyo arobaini hasa ikiwa tunaona nyumba za marehemu Dodoma, Mwanza, Tarime na Dar.
kwa nini tusiwalaumu familia kwa kuweka hizi arobaini nyumba mbili.. Je, kama viongozi wa Chadema wangekwenda Dar wakaacha kwenda Tarime mngesema nini?..
Jamani huyu mwanamke na wote wanaompandisha chati wana lao jambo...

Kwanza hiyo arobaini si inafanyiwa pale marehemu alipozikwa? Mimi ningetegemea wafanyie Tarime.

Tatizo sasa kila watu wanajifanya wanafanya arobaini huku hawajui hata utamaduni wa hiyo arobaini.

Ila tu kwenye masuala ya familia za watu, ni muhimu kuwaachia wenye familia. Kama kweli Dr. Slaa kasema hamtambui huyo mwanamke kama mke wa Wangwe, hapo huenda hasira imechukua nafasi ya busara. Kwa mawazo yangu hakutakiwa kusema hivyo.
 
Stevin Wasira aka Tyson anawake 5 watoto Lukuki unashangaa nini mkuu!! watu wanafata jadi...King Mswati nadhani ni balaaa

Wote hao ni kundi moja tu na je kweli dunia hii ya credit crunch unaweza kutunza wake wote hao na watoto wote kwa usawa?

Huyo Mswati si kama Mugabe tu, watu wake wanakufa kwa ukimwi yeye kila mwaka anaoa mke mwingine.

Jadi zingine hazifai kabisa kwa nchi maskini kama TZ. Mnaotaka endeleeni nazo, ili msianze kutuibia ili kulinda hizo jadi zilizopitwa na wakati.
 
Mkandara,

Mbona hata yule mke mwingine aliyehojiwa ni kama anamtambua huyu mama?

Kwa mila za Kiafrika kama prof. Wangwe ambaye nafikiri ndiye mkuu wa hiyo familia anamtambua, basi huyo anatambuliwa na ukoo. Sio lazima hao wanawake wengine wamkubali maana wanashindania bwana.

Ila Wangwe naye, karne ya 21 na wake watatu? Ndio maana tunaendelea kuwa maskini. Wabunge ndio walitakiwa kuongoza mabadiliko kwa kupinga mambo yanayotukwamisha. Sasa watoto wote hao, nani atawasaidia na kuwaendeleza?

Mkuu Mtanzania, nitakupa kura yangu kule Kyela! ..... kula tano kwanza 🙂
 
Mkandara,

Mbona hata yule mke mwingine aliyehojiwa ni kama anamtambua huyu mama?

Kwa mila za Kiafrika kama prof. Wangwe ambaye nafikiri ndiye mkuu wa hiyo familia anamtambua, basi huyo anatambuliwa na ukoo. Sio lazima hao wanawake wengine wamkubali maana wanashindania bwana.

Ila Wangwe naye, karne ya 21 na wake watatu? Ndio maana tunaendelea kuwa maskini. Wabunge ndio walitakiwa kuongoza mabadiliko kwa kupinga mambo yanayotukwamisha. Sasa watoto wote hao, nani atawasaidia na kuwaendeleza?

Kwa kweli mnapotosha alichokisema Dr Slaa, kwa aliyesikiliza TBC1 tafadhali atuwekee hapa. Maana wengine tukiweka tutaonekana tunamtetea tu kipenzi chetu Dr Slaa.

Halafu Prof Wangwe sio msimamizi wa mirathi ya Chacha Wangwe, ni kimbelembele chake tu kinamtuma kuwa msemaji wa familia. Na mtaona kwenye arobaini hata msemaji hakuwa yeye.

Asha
 
Dada Asha,

Kuwa mkuu wa familia ni tofauti na kuwa msimamizi wa mirathi. Sijui sehemu zingine lakini kule kwetu sisi, mkuu wa familia ndio anaamua mambo yote yanayohusiana na misiba, of course anashauriana na wengine pia.

Haya mambo ya sio mama mmoja au baba mmoja hayana maana kabisa. Ukoo ni mkubwa kuliko mtu mmoja mmoja. mkianza kutenga watu hata kwenye koo sijui mtaishia wapi.

Hivi huko Zanzibar inaelekea mnabaguana sana kwi kwi kwi!!
 
Wazanzibar sisi sio kama wachagga. Msimamizi wa mirathi lazima awe mtu wa karibu. Prof Wangwe anajilazimisha kuwa kiranja wa familia. Halafu mbona hawatetei wake wengine wa marehemu, kila siku Mariam, Mariam, Mariam. Kuna nini kati yao? Halafu si alitangaza kutaka kugombea ubunge Tarime kupitia CCM? Nini kilimuogopesha? Au kwa sababu wakati wa msiba walimwambia wewe wa Dar es salaam rudi ulipotoka tuachie wa Tarime?

Asha
 
CCM: Ruksa kutumia kifo cha Wangwe kisiasa

2008-09-30 11:36:47
Na Simon Mhina

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni `ruksa` ndugu wa Marehemu Chacha Wangwe kutumia jukwaa la kampeni za Chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Tarime kuzungumzia hisia zao juu ya mazingira ya kifo cha ndugu yao.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Pius Msekwa alisema ndugu hao wana haki kuzungumzia kifo hicho kwenye jukwaa la CCM kwani hizo ndizo haki za binadamu.

Akifafanua, mwanasiasa huyo alisema ndugu hao ukiwaondolea jukwaa la siasa, hawana sehemu nyingine ya kusema, kutoa dukuduku zao na kuonyesha hisia zao.

Msekwa ametoa kauli hiyo akijibu malalamiko ya viongozi wa Chadema kwamba baadhi ya vyama vimekigeuza kifo cha Wangwe kuwa mtaji wa kisiasa katika uchaguzi huo.

``Jamani nyie hamfahamu haki za binadamu, wale wana madukuduku yao, lakini wamekosa mahali pa kusemea, wanapopanda kwenye majukwaa yetu wanaona hiyo ni sehemu muafaka, ruksa hatuwezi kuwazuia,`` alisema.

Hata hivyo, Msekwa alisema wanaolalamikia kifo cha Wangwe sio CCM, bali ndugu zake.

Alisisitiza kwamba nchi yetu imetoa uhuru wa kujieleza kwa kila mwananchi, ili mradi asivunje sheria, hivyo wanachokifanya ndugu wa Wangwe ni sahihi.

``Kwa mfano juzi nimesikia mjane wa marehemu yeye akitumia jukwaa la vyombo vya habari kutoa hisia zake mbona hakunyimwa? Kwa hiyo na sisi hatuwezi kuwanyima fursa hiyo kama wanataka,``alisema.

Alipoulizwa kama haoni suala hilo ni sawa na uchochezi, Msekwa alisema mtu kudai kwamba haelewi mazingira ya kifo cha marehemu wake kilivyotokea sio uchochezi.

``Tutaendelea kuwakaribisha ndugu wa Wangwe kwenye mikutano yetu na hatuwezi kuwapangia cha kuzungumza,``alisema.

Alisema wameamua kufanya hivyo, kwa vile ndugu wa marehemu wamejirizisha kwamba kifo hicho kilijaa utata.

Pia alisema malalamiko kama hayo hayakuanzia kwenye jukwaa la CCM, bali kwa kaka wa Marehemu huyo Profesa Wangwe.

Kuhusu mwenendo wa kampeni, Msekwa alisema hakuna vitisho vyovyote vinavyotolewa na Polisi na hao wanaodai kuna askari `wamemwagwa` hawaelewi mambo.

Alisema vikosi vya askari vilivyomwagwa ni kwa ajili ya kuwalinda wananchi na mali zao na kuwa amini dhidi ya wezi wa ng`ombe.

``Unajua huku kuna wezi wa Ng`ombe na mapigano ya koo, hivyo lazima polisi wawe wengi,``alisema.

Alipoulizwa kama Polisi wamemtuma atoe msimamo huo, Msekwa alisema tataribu za Polisi ziko wazi, hawawezi kuletwa sehemu kwa nia ya kuvuruga, bali kulinda amani.
Alisema raia wema hawana sababu yoyote ya kuogopa Polisi.

SOURCE: Nipashe
 
Polisi wakiri aliyekamatwa ofisi za Chadema ni askari wao
Na Kizitto Noya

JESHI la Polisi limesema askari aliyekamatwa wilayani Tarime akijaribu kununua kadi 20 za uanachama wa Chadema, alikuwa kazini.

Kiongozi wa Kikosi cha Operesheni Maalum ya jeshi hilo jimboni Tarime, Venance Tossi aliliambia gazeti hili jana kuwa askari huyo ni wa kikosi chake ambaye alikuwa katika "kazi maalum" ya kikachero.

"Huyu ni askari wetu wa kikundi maalum cha intelijensia yaani ukachero aliyekuwa kazini. Sasa huwezi kuwatambua polisi wote na ndio maana alikamatwa," alisema Kamanda Tossi bila kusema aina ya kazi aliyokuwa akifanya askari huyo.

Alisema mawazo yaliyojengeka kwamba askari huyo alilenga kufanya hujuma katika uchaguzi huo sio sahihi kwani alikuwa kazini na kukamatwa kwake ni ajali ya uwajibikaji.

"Ni vema nikwambie ukweli ili msiandike uongo. Huku tuna vikosi vingi sana ambavyo vinafanya kazi tofauti wengine wako kwenye uniform (sare) na wengine wanavaa kiraia. Huyo ni askari wetu, alikuwa kazini," alisema.

Kabla ya taarifa ya kamanda Tossi, kaimu mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini, DCI, Kamishina Peter Kivuyo alisema polisi itatumia kanuni na taratibu zake kumwadhibu askari huyo ikithibitika kuwa alifanya hivyo kinyume na maelekezo ya kazi.

Alisema ni mapema mno kuzungumzia suala hilo sasa kwani ofisi yake haijapata taarifa za kiutendaji kutoka Tarime, lakini alisisitiza kuwa ikithibitika alifanya hivyo nje ya maelekezo ya kazi, askari huyo tashughulikiwa kwa taratibu za kijeshi.

"Ni mapema mno kuzungumzia suala hilo sasa kwa kuwa bado hatuna hakika na tukio lenyewe, lakini ikithibitika kwamba alifanya hivyo nje ya maelekezo ya kazi, polisi itamchukulia hatua kwa mujibu wa taratibu na kanuni za kazi zilizopitishwa kisheria," alisema Kivuyo.

Ufafanuzi alioutoa Kamanda Tossi, ambaye juzi aligoma kuzungumzia suala hilo, umethibitisha madai ya Chadema kuwa kijana huyo ni muajiriwa wa Jeshi la Polisi.

Kijana huyo, ambaye anadaiwa kutokea Arusha, alikamatwa baada ya kubanwa na walinzi wa Chadema wakati alipoenda kujaribu kununua kadi 20 za uanachama.

Kijana huyo, Emmanuel Zacharia, ni mmoja wa polisi 400 waliomwagwa wilayani Tarime kwa ajili ya oparesheni maalum ya kidemokrasia na kuzuia mapigano baina ya koo.

Mara baada ya kufika ofisi za Chadema, watu waliokuwepo eneo hilo "hawakuwa na amani" naye na katika mahojiano walimuona akibabaika na ndipo walipomuweka chini ya ulinzi na kumpekua. Katika upekuzi huo walimkuta na barua ya polisi inayomtambulisha benki kuwa apewe huduma anayotaka.

Kukamatwa kwake kulitokea siku moja baada ya mwanafunzi wa kidato cha tatu kukamatwa kwenye ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) akisaka mteja wa kununua shahada za kupigia kura.
 
Mchungaji Mtikila nusura kupigwa mawe tena Tarime
Fredrick Katulanda na Mussa Juma, Tarime

MVUA za mawe zimeendelea kumsakama mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party, (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, baada ya kunusurika kupigwa mawe wakati akiendelea na staili yake ya kampeni ya 'kuirushia madongo' Chadema akidai kuwa inahusika na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo la Tarime, Chacha Wangwe.

Tukio hilo limekuja siku chache baada ya mchungaji huyo wa kanisa la uamsho kujeruhiwa kisogoni kwa jiwe lililorushwa na mtu mmoja wakati alipotoa tuhuma hizo kwenye mkutano wake wa kampeni mjini Tarime, ambako uchaguzi utafanyika Oktoba 12 kuchagua mbunge na diwania.

Jana nusura adha hiyo impate tena wakati akihutubia mkutano wa kampeni za chama chake katika eneo la Buhemba majira ya saa 10:00 jioni.

Tukio hilo lilitokea baada ya Mtikila kumwaga kauli zilizowakera baadhi ya waliohudhuria mkutano huo.

Wakati mchungaji huyo akimwaga tuhuma hizo, mtu mmoja aliamua kurusha mawe, lakini kabla hajarusha mawe aliwahiwa na mlinzi wa Mtikila aliyemkamata na kumkabidhi kwa polisi na mkutano ukaendelea.

Jana, kama kawaida yake aliendelea kushusha tuhuma nzito kwa Chadema na kwa baadhi ya wafanyabiashara maarufu nchini akiwatuhumu kutumia ukabila kumuondoa Wangwe.

Mtikila, ambaye ni maarufu kwa kutoa tuhuma nzito, aliwahi kutoa tuhuma hizo kwa Chadema mapema mwezi huu, akihusisha kifo cha mbunge huyo wa jimbo la Tarime na mgongano wa kikabila ndani ya chama hicho na kumuhusisha mfanyabiashara mmoja maarufu.

Mchungaji huyo alikuwa ameanza kueleza kifo cha Wangwe ambaye alifariki kwenye ajali ya gari ndogo wakati akisafiri kutoka Dodoma kuelekea Dar es salaam kuhudhuria mazishi ya mfanyabiashara Bhoke Munamka.

Wakati huo huo wa kampeni za uchaguzi kugombea ubunge jimbo la Tarime wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika eneo la Kemakorere alikozikwa mbunge wa chama hicho jana ulidorora baada ya mvua kali kunyesha.

Mkutano huo ambao ulianza majira ya saa 10: 00 jioni lakini ulihudhuriwa na watu wachache waliostahimili mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha kijijini humo.

Hata hivyo pamoja na mvua hiyo kunyesha mgombea wa Chadema Charles Mwera, alihutubia wanachama wachache waliomudu kusimama kwenye mvua hiyo kijijini hapo.

Akizungumza katika kampeni hizo Mwera aliomba wanakijiji hao kumchagua ili aweze kuendeleza mazuri yaliyokuwa yakifanywa na marehemu Chacha Wangwe, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo aliyefariki kwa ajali ya gari Julai mwaka huu.

Alisema iwapo wanakijiji hao watampigia kura na hatimaye akafanikiwa kuwa mbunge, atahakikisha kwamba elimu kwa watoto wa Tarime inatolewa bure ili iweze kuwanufaisha wananchi hao ambao wengi wao ni masikini.

Aliitumia fursa hiyo kukanusha tuhuma kuwa Chadema inahusika na kifo cha aliyekuwa Wangwe, na kwamba wanaotoa shutuma hizo ni wale ambao hawaitakii mema Tarime na wana ajenda zao binafsi.

Alilitaka Jeshi la Polisi nchini limkamate mwenyekiti wa chama cha DP, Mch. Christopher Mtikila kwa madai kuwa anasambaza kauli za uchochezi ambazo zinalenga kusababisha maafa jimboni humo.

Source: Zote mbili MWANANCHI
 
It must be the only card they think they are holding now. Pathetic!
 
hii ndio season ya Mtikila kumaliza njaa zake,sasa kishavuta vipesa vya CCM kazi sasa ni kupiga domo Chadema wamemwua Wangwe.....kweli hili lunatic ni la kupuuza tuu,maana hata kulipeleka court unaweza kuonekana na wewe mwehu tuu!
 
Hivi watu kama hawa, wamefikaje hata kushika madaraka makubwa ya nchi? Haitendei haki kabisa familia ya Wangwe. Inaelekea utu haupo kabisa sasa kwa wanasiasa.
 
Mtanzania,
That is a good question.I thought he was retiring in 2005 and bring some young blood in the system lakini kumbe!
 
....hivi hili lizee linastaafu lini,kwani lilichoiba hakitoshi?
 
Unategemea nini kutoka kwenye chama kilicho kumbatia mafisadi? Hao CCM ni mufilisi kabisa wanatuharibia nchi tu.
 
CCM: Ruksa kutumia kifo cha Wangwe kisiasa

2008-09-30 11:36:47
Na Simon Mhina

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni `ruksa` ndugu wa Marehemu Chacha Wangwe kutumia jukwaa la kampeni za Chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Tarime kuzungumzia hisia zao juu ya mazingira ya kifo cha ndugu yao.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Pius Msekwa alisema ndugu hao wana haki kuzungumzia kifo hicho kwenye jukwaa la CCM kwani hizo ndizo haki za binadamu.

Akifafanua, mwanasiasa huyo alisema ndugu hao ukiwaondolea jukwaa la siasa, hawana sehemu nyingine ya kusema, kutoa dukuduku zao na kuonyesha hisia zao.

Msekwa ametoa kauli hiyo akijibu malalamiko ya viongozi wa Chadema kwamba baadhi ya vyama vimekigeuza kifo cha Wangwe kuwa mtaji wa kisiasa katika uchaguzi huo.

``Jamani nyie hamfahamu haki za binadamu, wale wana madukuduku yao, lakini wamekosa mahali pa kusemea, wanapopanda kwenye majukwaa yetu wanaona hiyo ni sehemu muafaka, ruksa hatuwezi kuwazuia,`` alisema.

Hata hivyo, Msekwa alisema wanaolalamikia kifo cha Wangwe sio CCM, bali ndugu zake.

Alisisitiza kwamba nchi yetu imetoa uhuru wa kujieleza kwa kila mwananchi, ili mradi asivunje sheria, hivyo wanachokifanya ndugu wa Wangwe ni sahihi.

``Kwa mfano juzi nimesikia mjane wa marehemu yeye akitumia jukwaa la vyombo vya habari kutoa hisia zake mbona hakunyimwa? Kwa hiyo na sisi hatuwezi kuwanyima fursa hiyo kama wanataka,``alisema.

Alipoulizwa kama haoni suala hilo ni sawa na uchochezi, Msekwa alisema mtu kudai kwamba haelewi mazingira ya kifo cha marehemu wake kilivyotokea sio uchochezi.

``Tutaendelea kuwakaribisha ndugu wa Wangwe kwenye mikutano yetu na hatuwezi kuwapangia cha kuzungumza,``alisema.

Alisema wameamua kufanya hivyo, kwa vile ndugu wa marehemu wamejirizisha kwamba kifo hicho kilijaa utata.

Pia alisema malalamiko kama hayo hayakuanzia kwenye jukwaa la CCM, bali kwa kaka wa Marehemu huyo Profesa Wangwe.

Kuhusu mwenendo wa kampeni, Msekwa alisema hakuna vitisho vyovyote vinavyotolewa na Polisi na hao wanaodai kuna askari `wamemwagwa` hawaelewi mambo.

Alisema vikosi vya askari vilivyomwagwa ni kwa ajili ya kuwalinda wananchi na mali zao na kuwa amini dhidi ya wezi wa ng`ombe.

``Unajua huku kuna wezi wa Ng`ombe na mapigano ya koo, hivyo lazima polisi wawe wengi,``alisema.

Alipoulizwa kama Polisi wamemtuma atoe msimamo huo, Msekwa alisema tataribu za Polisi ziko wazi, hawawezi kuletwa sehemu kwa nia ya kuvuruga, bali kulinda amani.
Alisema raia wema hawana sababu yoyote ya kuogopa Polisi.

SOURCE: Nipashe

An idiot called Msekwa! Kwake yeye wanaosema sio CCM wakati anajua kabisa wanapanda majukwaani kusema ni Keba Wangwe kiongozi mwandamizi wa CCM, Profesa Wangwe Mjumbe wa NEC CCM na Mariam Wangwe kada wa CCM aliyeolewa na mbunge wa CHADEMA. Hivi bado wanatuaminisha kwamba hapa kuna ufamilia tu hakuna UCCM hapo! Huyu Keba aliyemfunga jela Chacha na Prof Wangwe aliyemtenga Chacha kwa kumuita muhuni na mpinzani leo ndio familia ambayo inapewa 'hisani' kutumia jukwaa la CCM kufikisha kilio chao! Ama kweli, ukistaajabu ya Makamba utaona ya Msekwa.

Naona umeamua kujinukuu...
 
Koba,]
Mimi nilidhani polisi wamemtahadharisha aache kuhubiri mambo ya kifo cha Wangwe, au?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom