Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Tume imeshapinga kupiga kampeni kwa kutumia kifo cha Wangwe
 

Katika majuha waliojaa huko CCM, masatu ndio kiranja. CCM hii inayojali fedha tu, haitaishiwa majuha wa aina hii, labda ibadilike na kuongozwa na ideology kama enzi ya Nyerere.
 
I would like to afford MP Zitto the benefit of the doubt and a chance to put his story straight to the people through JF.

The story rings rather politically motivated.
 
wakuu Abi-Tchaz,Invincible na nyambala,heshima kwenu,
 
I would like to afford MP Zitto the benefit of doubt and a chance to put his story straight to the people through JF.

The story rings rather politically motivated.


you are right buddy!
 
Hivi watu kama hawa, wamefikaje hata kushika madaraka makubwa ya nchi? Haitendei haki kabisa familia ya Wangwe. Inaelekea utu haupo kabisa sasa kwa wanasiasa.



Mkuu,

angalao sasa uko kwenye mstari.kwi kwi kwi.Ila pokea tano kwa kwa swali lako neutral1
 
Tume imeshapinga kupiga kampeni kwa kutumia kifo cha Wangwe


sasa ina maana Mtikila atafanya nini Tarime? Maanke hata akieneza injili haaaminiki tena,maanke bado hata huko kwenye ibada waumini watamtandika mawe.Kaazi kweli kweli.
 
Apewe pole kijana kabwe kazi ndio imeanza hapo yeye sio wa kwanza na hatokuwa wamwisho kwani amekuwa tishio kwa CCM na watafanya wawezalo katika nguvu zao zote na kuhakikisha anaondoka katika safu aliyokuwapo jihadhari kutoka sasa kunamanenoulishawahi kuambiwa kama miezi michache hivi huko nyuma nayarejea (chunga wewe CCM ndio yenye dola)nakutakia kila la kheri katika kuipigania nchi yetu hii
 
Ila wasilete ujinga wao,wakitaka kulitumbukiza taifa katika janga kubwa na wajaribu kuleta uonevu waone
 

Mtanzania
Kuongezea huyo Emmanuel Kulangwa,hakosi kwenye misafara ya majuu na Rais
 
Katika majuha waliojaa huko CCM, masatu ndio kiranja. CCM hii inayojali fedha tu, haitaishiwa majuha wa aina hii, labda ibadilike na kuongozwa na ideology kama enzi ya Nyerere.

Tawire mkuu mwerevu wewe na Chadema yako.....
 
Jamani, lililoandika ni Alasiri, si tunalifahamu vizuri gazeti hili. People should not be carried away
 
[Source Tanzania Daima]

DC: Zitto akamatwe




na Kulwa Karedia



KAMPENI za uchaguzi mdogo kuwania ubunge wa Jimbo la Tarime, jana zilichukua sura mpya, baada ya serikali kuingilia kati.

Serikali wilayani hapa imeagiza kukamatwa watu kumi, akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, kwa madai ya kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani katika kampeni zinazoendelea.

Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Stanley Kolimba, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mwenendo wa kampeni za uchaguzi zinazoendelea katika jimbo hilo.

“Tangu kuanza kwa kampeni hapa Tarime kumekuwepo na malalamiko mengi yanayotolewa na vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huu... sasa serikali imelazimika kuagiza vyombo vya dola kuwakamata wanaohusishwa na tuhuma hizi, akiwemo Zitto Kabwe,” alisema Kolimba.

Kolimba alibainisha kuwa, Zitto ni mmoja wa watu wanaotafutwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kina, kwa madai kuwa alihusika kuwashawishi wafuasi wa CHADEMA kufanya vurugu mara baada ya mkutano uliofanyika juzi katika viwanja vya Shule ya Msingi ya Nyamisangura.

Alisema katika mkutano huo, Zitto alihamasisha wafuasi wa CHADEMA kuchoma moto bendera, fulana na vitu mbalimbali vyenye nembo za Chama Cha Mapinduzi (CCM), jambo ambalo limezua malalamiko mengi kutoka kwa viongozi wa chama hicho tawala.

Alisema kwa kitendo hicho, mbunge huyo amevunja sheria na kanuni za uchaguzi, jambo ambalo kamwe haliwezi kuvumiliwa, kwani linaweza kusababisha hali ya uvunjifu wa amani na mshikamano uliopo.

“Jumapili iliyopita, Zitto akihutubia kwenye mkutano wa hadhara, Shule ya Msingi Nyamisangura, alikuwa mmoja wa watu waliochangia mno kuchomwa kwa nguo za CCM na kusababisha hali hiyo ambayo imelalamikiwa na vyama vinavyoshiriki uchaguzi huu, kikiwemo CCM,” alisema Kolimba.

Tayari watu kadhaa wameshakamatwa, na Kolimba alisema kati ya watu waliokamatwa, wengi wao wanatoka Kijiji cha Goroma, ambako mmoja wao anasakwa na polisi kwa tuhuma za kumvua mtu nguo na kumwacha uchi.

Alisema matukio mengine ambayo sasa yanaonekana kusababisha uvunjifu wa amani ni pamoja na wafuasi wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi kushusha bendera za vyama vingine na kupandisha za kwao.

Katika hatua nyingine, DC huyo alisema wamegundua mpango ulioandaliwa na baadhi ya vyama ambavyo hakuwa tayari kuvitaja, kuandaa vijana kutoka katika Wilaya ya Kurya nchini Kenya kuja kupiga kura Oktoba 12.

“Tumeagiza vyombo vyetu vya dola kushughulikia suala hili haraka iwezekanavyo,” alisema Kolimba.

Alisema kutokana na hali hiyo, wamewasiliana na viongozi wa Wilaya ya Kurya, kuona kama kweli kuna mpango huo wa kuleta vijana, jambo ambalo alisema kwa mujibu wa sheria haliruhusiwi na kwamba watakaobainika, watakamatwa mara moja.

Alitoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa kuacha kutumia lugha za uchochezi kwa vile kufanya hivyo kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Naye Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Tarime, Taitus Kagenzi, ameiomba serikali kuongeza idadi ya askari wilayani humu, ili kukabiliana na hali ya vurugu katika kampeni hizo, kwa madai kuwa askari waliopo hawatoshelezi mahitaji. Alisema askari wengi wanahitajika hasa Oktoba 12, ambayo ni siku ya kupiga kura.

Alisema idadi ya askari waliopo kwa sasa ni 423, wakiwemo maofisa mbalimbali, ambao kamwe hawawezi kusimamia shughuli ndogo ndogo, zinazotakiwa kusimamiwa na askari wa vyeo vya chini.


Msimamizi huyo alitumia nafasi hiyo kukanusha uvumi ulioenea mjini hapa kwamba anajiandaa kumtangaza mgombea wa CCM kabla ya kupata matokeo ya kura zote.

“Napenda kutumia nafasi hii kuwahakikisha wananchi wa Tarime kuwa, sitatangaza mgombea yeyote kwa shinikizo, kwani hakuna sheria inayoruhusu kufanya hivyo... mimi nitamtangaza yule tu aliyepata kura nyingi baada ya kura kuhesabiwa,” alisema Kagenzi.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, jana alinusurika tena kupondwa jiwe, wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Buhemba, mjini hapa.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Mtikila kuendelea kutoa kauli za uchochezi kuhusiana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, kwamba aliuawa na si ajali kama inavyodaiwa.

Baada ya kusikia kauli hizo, kijana mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alikuwa na jiwe tayari kumlenga Mchungaji Mtikila, lakini mmoja wa walinzi wa mchungaji huyo, aliwahi na kumkamata kabla hajadhibitiwa na polisi.

Naye Salehe Mohamed, anaripoti kuwa Jeshi la Polisi, limeongeza posho kwa askari wake waliopo Tarime.

Hali hiyo ina lengo la kuwaondolea vishawishi vya kutumiwa vibaya na vyama vya siasa kama ilivyodaiwa juzi, ambapo inadaiwa askari mmoja alikamatwa akitaka kununua kadi za CHADEMA.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Abdallah Mssika, alisema jana kuwa wamepokea taarifa za kukamatwa askari huyo, lakini ni mapema mno kuzungumzia kabla ya kufanyika kwa uchunguzi.

“Suala kuwa wananunua na kuziuza kadi za CHADEMA kwa sababu ya ukata wa fedha sikubaliani nalo, kwani tumeshaongeza posho kwa askari, naomba mnipe muda niweze kufuatilia kwa ukaribu zaidi,” alisema Mssika.

Kwa upande wake CCM, nayo imetoa kauli ya kuwashutumu viongozi wa CHADEMA ikidai kuwa ni wahuni, na hawajaonyesha nia ya kuimarisha umoja wa taifa na kuendeleza amani na utulivu katika kampeni za uchaguzi mdogo, zinazoendelea mjini Tarime.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Saalam na Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM, ofisi ndogo ya makao makuu, ilibainisha kuwa kauli na vitendo vya baadhi ya viongozi wa CHADEMA zinaashiria nia yao hiyo.

Taarifa hiyo ilisema kitendo cha Zitto kuwaongoza wafuasi wao kuchoma fulana zenye picha ya mgombea ubunge Tarime kwa tiketi ya CCM katika mkutano wa kampeni, kinaonyesha dhahiri uhuni na uvunjaji wa sheria.

“Tunajua hizo ni mbinu za uchochezi na fujo zilizoandaliwa na CHADEMA ili kuipaka matope CCM, jambo ambalo ni la uongo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, CCM imedai kuwa kijana Mahemba Daudi, aliyekamatwa juzi katika ofisi za CCM kwa kuuza shahada za kupigia kura, alipandikizwa na CHADEMA na CCM iligundua mtego huo na viongozi wa wilaya walitoa maelekezo yaliyosababisha kijana huyo kukamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi.

Edward Kinabo, naye anaripoti kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeshindwa kutoa msimamo wake dhidi ya vyama vinavyodaiwa kutumia kifo cha Wangwe kama mtaji wa kisiasa wa kujipatia ushindi katika uchaguzi huo, kwa kuihusisha CHADEMA na kifo hicho.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Lewis Makame, alisema jana kuwa, tume yake haina ushahidi juu ya kifo hicho kutumiwa vibaya na taarifa ya msimamizi wa uchaguzi jimboni Tarime haijaeleza kuwepo kwa hali hiyo.

Alisema yanayosemwa kuhusu kifo cha Wangwe yamekuwa yakiandikwa na vyombo vya habari na tume yake haiwezi kuzichukulia taarifa hizo kuwa ni za kweli hadi hapo zitakapothibitishwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo.

Hata hivyo alisema, iwapo mtu atatumia kifo hicho kukashifu wengine, hilo litakuwa kosa, kwa kuwa ni kinyume cha maadili ya uchaguzi, lakini kama mtu atakizungumzia tu kifo hicho katika kampeni, hapo hakuna kosa.


Akiunga mkono kauli hiyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Rajab Kiravu, alisema si kila kinachosemwa kuhusu kifo cha Wangwe, kina ubaya, kwani katika hali ya kawaida ni rahisi kwa kifo hicho kutajwa kwenye kampeni hizo, kwani ndicho kilichosababisha kuitishwa kwa uchaguzi huo.

“Kwa mfano, mtu anaweza kusema kwenye kampeni kuwa uchaguzi huu unafanyika kwa sababu ya kifo cha Chacha Wangwe. Sasa mtu akisema hivyo …hiyo ni kawaida tu… si kashfa,” alisema Kiravu.

Kuhusu vurugu zinazoendelea, Jaji Makame alisema NEC imesikitishwa na taarifa za kuwepo kwa matukio yanayoashiria uvunjaji wa amani katika kampeni za uchaguzi huo.

Alisema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa sheria na endapo wanaohusika watabainika, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Aliviasa vyama vya siasa na wagombea wanaoshiriki katika uchaguzi huo kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maadili ya uchaguzi.

Aidha, aliwasihi wananchi wa Tarime kushiriki katika kampeni kwa kusikiliza kwa utulivu sera za vyama vyote na kuepuka kujihusisha na vitendo vinavyoweza kuleta uvunjaji wa amani.

Tangu kuanza kwa kampeni wiki mbili zilizopita, kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya vurugu na uvunjaji wa amani miongoni mwa wafuasi wa vyama vinne vya siasa; CCM, CHADEMA, NCCR MAGEUZI na DP, vilivyosimamisha wagombea wao katika uchaguzi huo.
 
Hivi kuchoma moto takataka ni kusababisha vurugu??? Halafu mbona wakina Rostam, Lowassa, Jeetu Patel, Chenge na wengineo polisi mmekuwa bubu kuwakamata?? Wameiba pesa wakatengeneza tshirt wananchi wa Tarime wakazikataa. Wamewashtukia kwamba mnawadharau. Hizo pesa zilikuwa za kwao kwa ajili ya maendeleo na sio mitumba.
 
Zitto ni mtu makini sana katika kufanya mambo yake, sidhani kama alishiriki kuchoma bendera ya Chama cha Mafisadi au kuhamasisha kitendo hicho. Viongozi aka mafisadi wa chama cha mafisadi wanafahamu fika umaarufu mkubwa walioupata Zitto na Dr Slaa kaitika mapambano dhidi ya mafisadi. Hivyo CCM watawabambambikia chochote kile ili kuwapunguzia umaarufu wao au hata kuwafunga. Naona juhudi za kuwanyamazisha zinazofanywa dhidi yao na chama chao ni sawa kabisa na juhudi za fisadi Mugabe alias dikteta katika kumnyamazisha Tsavangarai na MDC. Mashtaka dhidi ya Zitto yanaweza kufikishwa mahakamani haraka sana wakati mashtaka dhidi ya mafisadi wa EPA, Meremeta, Kiwira, Richmond n.k. yanajaribu kumalizwa kimya kimya. Ni matumaini yangu Watanzania tutaliona hili. Kigumu chama cha mafisadi! Kigumu.
 
Of course kama ni kweli kachoma hizo T-shirts za CCM ni makosa.

Katika kitu ambacho kinaimaliza Afrika sasa ni vurugu za kisiasa. I hope wanasiasa wetu
wataelewa umuhimu wa kulinda amani.

Inaelekea sasa Tarime kuna tension kubwa sana. Naona tume ya uchaguzi na serikali wanashindwa kutimiza wajibu wao. Kama sheria zipo lazima zitumike kwa makali yote tena bila kuangalia sura ya mkosaji.

Inasikitisha sana kwa watu maskini kuamua kukumbatia vurugu badala ya amani.

Huyo Kolimba badala ya kushinda kwenye kuongea na vyombo vya habari inatakiwa achukue hatua zote zinazotakiwa kukomesha vurugu za kisiasa. Kama tumeshindwa kuheshimu demokrasia basi afadhali irudisheni nchi kwenye chama kimoja. Kuna haja gani ya kufanya uchaguzi huku watu wanajua wataiba au watatumia vurugu kupata hizo kura?
 

Hivi hao Ma-DC, mapolisi na tume ya uchaguzi mbona hawakuagiza wele mabaradhuli wa KITETO wakamatwe? Watueleze kwanza wamefikia wapi kuhusu haya ya Kiteto:

Ushiriki wa Jeshi la Polisi

Jeshi la polisi lilikuwa mihimili muhimu sana kwa ushindi wa CCM Kiteto. Polisi wa Kiteto walifanya kazi pamoja na CCM kuidhibiti CHADEMA kwa kutumia mabavu na kila aina ya mizengwe kwa faida ya CCM. Matukio ya uvunjifu wa amani yalifanywa mbele ya polisi na hata tulifipokisha malalamiko rasmi polisi, polisi walihofu kuchukua hatua stahiki na pale walipoona aibu walijitahidi kuwabembeleza viongozi wa CCM badala ya kuchukua hatua kama chombo cha dola. Kwa mfano;

Maafisa wa Uhamiaji walimzuia uwanja wa ndege Dodoma fundi wa helikopta yetu kwa zaidi ya saa mawili bila kumweleza sababu za msingi.



CCM kwa kuwatumia makomandoo wake walivamia mkutano wa Kijungu na kuwapiga raia na kuwajeruhi mbele ya polisi lakini polisi hawakuchukua hatua zozote hata baada ya vyombo vya habari kuripoti unyama huo.

Kata ya Matui polisi walielezwa kuwa waziri wa viwanda na biashara alikuwa akiendesha zoezi la kununua shahada za kura lakini hawakukubali kwenda kuzuia zoezi hilo.


Nimeitoa hapa: Tamko la Uchaguzi wa Kiteto
 
Kwanza polisi walikua wapi muda huo? wakileta uonevu tu,sisi na wao.to hell with them!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…