Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.


Mkamap
Very well said .hapa umeacha unazi umesema ukweli .Lakini wa kulaumiwa zaidi ni Serikali ya CCM na si wana Tarime.Wana Tarime wanalishwa sumu.Hata baada ya Uchaguzi kutakuwa na maafa na they will never heal na maneno yako Mkamp yatakumbwa .
 
The beginning of the end for Zitto Kabwe... very sad indeed...

What do u mean!?

Hizo ni propaganda tu za wana CCM, kama kawaida wana side step ishu za hoja na kuingiza mambo tofauti.

Alasiri pia kuna wakati wanakuwa na habazri kama za kwenye Kiu na Ijumaa...I dont belive this story
 
Mhn, na zile kadi za vyama vya upinzani ambazo CCM hudai zimerudishwa kwao, huzipeleka wapi vile? Mbona hawakuitiwa polisi wawakamate? Kamba imekatikia pembamba leo.
 
Hivi nakumbuka kuna wale jamaa waliochoma bendera ya CCM kule Iringa na walikuwa wana CCM vile vile... or what happened to them

Na tena sasa ile bendera ndiyo hasa ilikuwa mali ya CCM na si kama hizi nguo walizo pewa.Hivi nguo hizi zinazo liliwa huko wamepewa zikizeeka watadaiwa ?
 
Date::9/30/2008
Polisi wakiri aliyekamatwa ofisi za Chadema ni askari wao
Na Kizitto Noya
 
Mjue; mpaka sasa kwa watz kuna vita; vita ya roho na mwili ndani ya mtu huyo huyo mwenye vita; mwili unasema chukua malia ya CCM ufaidike maana ni ya bure haina account popote tena nia ya kifisadi hakuna atakayeuliza; roho inakataa kuwa hiyo ni dhambi; ufisadi ni dhambi mbaya; nenda Chama makini taifa liokoke; hapa ndipo tulipo; waliochoma T-shirt hata Kolimba naona hajui sheria kabisa; Bendera ya ccm ni mali binafsi; inamilikiwa na mtu binafsi yaani CCM ( no STG/STJ/SU etc) si mali ya umma; wanagawa bure kama njugu hiyo mali isiyo na mmiliki ( ya kifisadi) na mwananchi analazimishwa tu kuipokea kwa umaskini; sasa akigundua kuwa umaskini ukinunuliwa ndio unazidi hapo haihitaji tena bali atachoma/tupa/gawa. Na hiyo si dhambi; wala haiko ktk sheria; na Kolimba hasomi tu yaani nina wasi wasi na hawa watu sijui wanapataje vyeo bila integrity yoyote ya kulinda maslahi ya umma. NIko hapo tu kwa leo
 


Madilu asante sana sana sana.
 
Hii inaweza kuwa na maana kubwa sana, ambayo usipotumia kichwa na kukipa kazi kichwa chako hutaelewa na kuona kama huu uliofanyika ni uhuni.



MAUMIVU YA KICHWA HUANZA POLEPOLE
 

Vurugu za hapa na pale hata kigoma zinatokea. Ninachokataa mimi ni assertions za viongozi wa ngazi za juu wa CCM [Makamba, Msekwa] kuwa Tarime [hivi sasa] kuna mapigano ya kikabila na koo kila kata/tarafa unayotua/zunguka. Huu ni uongo wa kutupwa. Vurugu hata Dar zipo [mara ngapi tunasikia wanafunzi wa UDSM wamefanya vurugu?] Tofautisha vurugu na MAPIGANO?
Think of it! Kama kweli mapigano yapo [kama hao wajingawajinga wa CCM na waandishi uchwara wanavyotaka tuamini], kwanini kampeni za uchaguzi zinaendelea? Kwanini serikali haichua hatua za kuhakikisha kuwa mapigano hayo yanasimamishwa mara moja? P'se, give me a break!
 

I'll repeat again. Kuna tofauti kubwa sana kati ya vurugu na mapigano. Ninachojaribu ku-debunk hapa ni uongo wa viongozi wa CCM ngazi ya taifa ambao pia umechotwa na vyombo vya habari kuwa: Tarime hivi sasa kuna mapigano makali ya kikabila/koo yanayoendelea kwa kila kata/tarafa wilayani humo. This is not true. Vurugu za hapa na pale za ushabiki wa kisisa[kutupiana mawe, kuzomeana] yes, zipo. Na hizi huwa zipo/zinajitokeza sehemu zote hata huko Marekani kwenyewe vurugu kama hizi hutokea once in a while.

Kuhusu Mtikila, what did you expect? Yaani, uli-expect kuwa atapeleka ujingaujinga wake huko Tarime anaowafanyia magabacholi na wazaramo kila siku alafu arudi bila nundu? Acha kunichekesha mkuu!
 



Gustanza-The
Umesema kama vile uko hapa tarime na sisi.Umejuaje mkuu ?Yaani akina Msekwa bwana .
 

Gustanza_The

Kuna kitu hapa sikuelewi. Kwanza, niseme najua kwamba Journalism ya Tanzania simply sucks, aggravating and nauseating. They are the weakest of all professionals in the history labor specialization.

Lakini, hapa nashindwa kuona walichokosea katika ku cover Tarime, hususan mfano wako wa wao kuandika kwamba watu wamekamatwa kwa kuzomea CCM. Umeeleza kwamba hawa media wanaibeba CCM. Lakini mimi nadhani aliyeandika kwamba watu wanakamatwa kwa kuzomea CCM inawezekana kabisa anataka kuonyesha CCM ilivyokuwa draconian and weakly kiasa kwamba wanakamata hata watu wanaowazomea. Wakati, kama ulivyosema, hata Malkia anazomewa. Yani, muandishi wa Alasiri yuko upande wako hapa. Hilo ni dongo kwa CCM, nadhani.

Sijaona katika mfano wako the press ilipoharibu.
 
Gustanza_The

Kuna kitu hapa sikuelewi. Kwanza, niseme najua kwamba Journalism ya Tanzania simply sucks, aggravating and nauseating. They are the weakest of all professionals in the history labor specialization.

The master of extremes and hyperboles; no middle ground, no grey just black or white! Even that is not just simply black but it has to be "blacker than anything ever recorded in human history"!
 
Kwa kukiri huko kwa polisi, nadhani sasa CHADEMA wanaweza kulishitaki Jeshi la Polisi kwa tukio hili, na huko mahakamani wanaweza kuamriwa wataje kwa uhakika ni kitu gani hasa walikuwa wamemtuma huyo askari wao, na wajitetee kama huko si kuzuia ama kudunisha mchakato mzima wa uchaguzi. Na kwa namna nyingine wametoa kigezo cha kupinga ushindi wa uchaguzi huu hasa kama chama kinachotumikiwa na jeshi hilo la polisi kitashinda. Ninavyoona hawa watu wa Tarime hawatakuwa na mbunge hadi uchaguzi wa 2010.
 

Mkuu, soma article yote [Alasiri] utaona outright bias iliyomo ndani ya hiyo article. Kukamatwa kwa watu wanne huko Nyamongo kwa sababu tu eti wamezomea vingozi wa CCM, ilikuwa ni spin/attempt ya Alasiri kujaribu kupumbaza umma kuwa, kweli kuna ushahidi wa viongozi wa CCM kufanyiwa fujo huko Tarime...

P.S. niko busy kidogo sasa hivi, ila nitapost the entire article hapo baadaye.
 
kulikoni hata kuhamisha mashambulizi yake toka CCM na kwenda CHADEMA?

Mtikila aahidi kuendelea kuishambulia Chadema
Frederick Katulanda, Tarime
Mwananchi

MWENYEKITI wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila amesema ataendelea kusambaza nyaraka zinazohusu kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo la Tarime, Chacha Wangwe na hatima ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwa haogopi kukamatwa na polisi.

Kauli hiyo ya kiongozi huyo machachari imekuja baada ya kamanda wa polisi mkoa wa Mara, Liberatus Barlow kusema mapema wiki hii kuwa jeshi lake litamkamata mchungaji huyo wa kanisa la Wokovu Kamili na kumchukulia hatua za kisheria kwa kuendelea kusambaza waraka unaoihusisha Chadma na kifo cha Wangwe, akieleza kuwa waraka huo ni wa uchochezi.

Lakini pia Mch. Mtikila ameeleza hayo siku moja baada kunusurika kupigwa jiwe wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni, tukio hilo likitokea siku chache baada ya kiongozi huyo kutunguliwa na jiwe kwenye mkutano mwingine baada ya kuituhumu Chadema kumuua mbunge huyo wa Tarime.

Shambulio la kwanza lilisababisha Mtikila akimbizwe hospitalini na kushonwa nyuzi saba baada ya jiwe alilorushiwa kumchana kisogoni.

Lakini jana, 'mtumishi huyo wa Mungu' alionekana kutoyumbishwa na kauli hiyo ya DCI wala matukio yanayotokea kwenye wilaya ambayo mapigano baina ya koo hulipuka mara kwa mara.

"Nitaendelea kusambaza nyaraka hizi hadi nifikie lengo langu la kusambaza nakala milioni moja kwa watu wasiopungua milioni 10," Mtikila aliwaambia waandishi wa habari jana.

Mtikila, ambaye aliwahi kutumikia kifungo cha mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kusema kuwa viongozi wa CCM walimuua katibu wa zamani wa CCM, Horace Kolimba, alisema haogopi kukamatwa na polisi kwa kuwa tayari ameshakamatwa mara kadhaa na kushitakiwa.

Kiongozi huyo wa DP alimtaka Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba kutopoteza muda wake kwa kuunda tume kwenda Tarime kumchunguza yeye (Mtikila) kama anaendelea na kusambaza waraka huo kwa kuwa ni wazi kwamba hatakoma.

"Hakuna atakayenizuia kusambaza waraka huu, na sasa ninasambaza waraka mwingine, huu unaoeleza 'Taarifa ya DP na Mwisho wa Chadema' ambao nitasambaza nyumba kwa nyumba kwa kutoa nakala za kutosha, nitasambaza mikoa yote pamoja na hapa Tarime," alieleza Mtikila, ambaye pia ni kiongozi wa taasisi ya Liberty Desk, ambayo shughuli zake hivi sasa zimefifia.

Akizungumzia uzoefu wake wa mapambano na vyombo vya dola, Mtikila alisema ameshawahi kukamatwa mara 29 tofauti na kuwekwa ndani ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kesi za aina mbalimbali, kitu kinachomfanya asiogope kukamatwa tena kwa kuwa polisi hawana jipya.

Mtikila alisema ameamua kutoa kauli hiyo baada ya kuamini kuwa polisi wana mpango wa kumziba mdomo katika kampeni zake na yeye hatakubali na badala yake ataendelea kusambaza waraka huo.

"Imefika mahali tunafungwa mdomo tusizungumze mambo ya nchi yetu," alisema. "Wamekufa akina Sokoine kwa ajali nilizungumza, amekufa Horrace Kolimba pia nilizungumza na kupiga kelele kwa vile tuliamini wameuawa. Naomba DCI atambue kuwa mimi ni mtu mwenye msimamo nitaendelea kueleza."

Alifafanua kuwa namna pekee ya itakayomzuia asiendelee kusambaza waraka huo ni wahusika kutoa waraka mbadala utakaoeleza sababu za kifo cha Wangwe vinginevyo, ataendelea kuusambaza waraka huo hadi jamii ijue ukweli.

"Sasa ninasaka fedha zaidi ili niweze kuongeza nakala ambazo pia nitasambaza tena," alisisitiza.

Kamanda huyo alisema tayari ofisi ya DCI imeunda tume ambayo itaenda wilayani Tarime kwa ajili ya kumchunguza Mtikila kwa kitendo chake cha kusambaza waraka huo unaoeleza kuwa ana ushahidi unaojitosheleza kwamba CHADEMA ilimuua Wangwe.

Katika kampeni zake Mchungaji Mtikila amemtaka Spika wa Bunge, Samwel Sitta kutopuuza ombi la mke mdogo wa marehemu Wangwe, Mariam Wangwe, ambaye aliomba Bunge kuunda tume kuchunguza kifo cha mume wake.

Alisema kama Bunge liliunda tume kuchunguza mambo mengine, halina budi pia kuunda tume ya kuchunguza kifo cha Wangwe kwa vile ni mwakilishi wa wananchi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…