Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,193
- Thread starter
- #1,041
Mkuu,inawezekana aliyemvalisha mbwa huyo alikua na nia nzuri tu labda uanzi kwa CCM ulikua umezidi.Kaazi kwa waliomuua.Nadhani akili haikushiriki ktk maamuzi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tarime: Mbwa avaa fulana ya CCM,auawa, mmiliki akamatwa
Kampeni hizo, licha ya kutawaliwa na kashfa na maneno makali kama zilivyo kampeni nyingine za kisiasa, zimekuwa na matukio mengine mengi yakiwemo ya kutunguana kwa mawe, majaribio yasiyofanikiwa ya biashara ya shahada za kupigia kura, kuchoma fulana za vyama na kupigwa mawe kwa gari la kampeni.
''Hizi ndizo siasa za wenzetu, sisi tunawaachia wananchi, maana hata sisi tunaweza kufanya hivyo kama tukiamua, lakini tutaonekana wote wendawazimu ndiyo maana nasema nawaachia wananchi wao ndiyo watakaoamua,'' alieleza Makamba.
Alisema ingawa nao wanazo bendera nyingi ambazo zimesalimishwa na wafuasi wengi wa Chadema, hawatathubutu kufanya hivyo.
Send this article
Tarime: Ni utata mtupu!
2008-10-03 19:22:43
Na Emmanuel Lengwa, Jijini
Licha ya jitihada za Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kuwa hali ya amani na utulivu inaendelea kuwepo wakati wa Kampeni za kuwanadi wagombea wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa Mbunge katika Jimbo la Tarime, hali bado imeendelea kuwa tata kutokana na kuongezeka kwa matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani ambapo jana, mama mmoja na wanawe wawili wanadaiwa kupigwa na kumwagiwa pilipili kwenye nyuso zao.
Inadaiwa kuwa mama huyo na wanawe wamepata kipigo na kupakwa pilipili baada ya kuhusishwa na dhihaka ya kitendo cha mbwa mmoja kuonekana mtaani akiwa amevishwa nguo zenye bendera ya chama kimoja cha siasa.
Imedaiwa kuwa tukio hilo limetokea jana , mishale ya saa 9:00 mchana.
Ikadaiwa na mmoja wa mashuhuda kuwa baada ya mbwa huyo kuonekana mitaani, watu wanaodhaniwa kuwa ni makomandoo wa chama kinachohasimiana na kile ambacho bendera yake imevishwa mbwa, wakamkamata mama mwenye mbwa huyo na wanawe kabla ya kuwapeleka porini na kuwasulubu kwa kipigo na kisha kuwasiliba nyuso zao kwa pilipili.
``Kabla ya kuwapiga, mama huyo na wanawe walivuliwa nguo na kumwagiwa pilipili ... inasikitisha sana,`` akasema mmoja wa mashuhuda. Hata hivyo, kiongozi mmoja wa kampeni wa CHADEMA, Bw. Msafiri Mtemelwa, amesema mama huyo na wanawe ni wafuasi wa chama chao na kwamba waliomtendea unyama huo ni watu wanaodhaniwa kuwa ni wa CCM.
Akasema Bw. Mtemelwa kuwa cha kushangaza, baada ya wao kutoa taarifa polisi, mama huyo na wanawe wakafuatwa huko waliko na kushikiliwa polisi badala ya wahusika wa tukio hilo kusakwa.
``Hivi sasa, tupo hapa Polisi tunashughulikia hatma ya mama huyu na wanawe... maana tunashangaa kuwa sisi ndio tuliotoa taarifa zake polisi ili asaidiwe, lakini badala yake yeye na wanae ndio wamekamatwa.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Liberatus Barow amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo la mbwa kuvishwa sare za CCM.
Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi, Kamanda Barow amesema amepata taafa za tukio hilo na kuwa yuko safarini kutoka Musoma mjini kwenda Tarime kulishughulikia.
``Taarifa ya tukio hilo nimezipata, lakini sina maelezo zaidi na hivi sasa niko njiani kwenda huko kulishughulikia,`` akasema Kamanda Barow.
Aidha Kamanda Barow ameiambia Alasiri kuwa tayari Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini,DCI, Robert Manumba, amewasili mkoani Mara ili kusimamia hali ya usalama.
Akasema pamoja na mambo mengine, DIC Manumba anakwenda kusimamia upelelezi wa sakata la usambazi wa waraka wa uchochezi unaodaiwa kusambazwa na Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila.
Katika hatua nyingine, baadhi ya viongozi wamekuwa wakilalamikia vitendo vya vurugu jimboni humo na kueleza kuwa havifai kwani ni vya hatari.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, CCM, Yusufu Makamba amelalamikia vitendo hivyo, vikiwemo vile vya kuzomewa kwa wagombea na pia viongozi wa chama chake wakati wa mikutano ya kampeni.
Amesema Makamba kuwa vitendo vya kuzomewa kwa viongozi vinaashiria vurugu ambazo zinaungwa mkono na wapinzani wao wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia, CHADEMA.
Hata hivyo alipoulizwa kuwa matukio hayo yanaathiri kwa kiasi gani mbio za chama chake za kulinasa jimbo hilo, Makamba alijibu kwa kifupi: ``Sina cha kusema. ``
Aidha, wakati Katibu huyo wa CCM akimwaga chozi dhidi ya hali ya vurugu ambayo amedai kuwa si njema kwani inazorotesha hali ya amani na utulivu, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe ambaye alikuwa pia jimboni humo, anadaiwa kuwa hadi sasa yuko nje ya nchi.
Imedaiwa kuwa Bw. Zitto yuko nchini Rwanda kwa shughuli za kikazi, kwani ana nyadhifa nyingi zinazomfanya awe akihitajika katika maeneo tofautitofauti.
Akizungumzia jambo hilo, Mwanasheria wa Chama hicho ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CHADEMA, Bi. Halima Mdee, amesema safari za Zitto haziwezi kuhusishwa moja kwa moja na yale yanayojiri kwenye kampeni za uchaguzi.
Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Bi. Halima amesema Zitto ni kijana jasiri na kuwa hawezi kukimbia kauli ya Mkuu wa wilaya ambaye anajua wazi kuwa hana ubavu wa kuamuru kukamatwa kwake.
``Binafsi namjua Zitto kuwa ni jasiri, ingekuwa ni kukimbia angekimbia wakati ule aliposimamishwa bungeni, lakini nimjuavyo hawezi kukimbia kauli ya mkuu wa wilaya,``akasema Bi. Mdee.
Akasema kilio cha muda mrefu cha vyama vya upinzani kuwa watendaji wanatumia madaraka yao vibaya kwa manufaa ya vyama vyao au wao binafsi kimedhihirika kupitia agizo la mkuu huyo wa wilaya.
``Kwa muda mrefu tumekuwa na kilio chetu juu ya watendaji wa Serikali, Mkuu wa wilaya pale anamuwakilisha rais, lakini inaonyesha kuwa hawezi kutenganisha majukumu yake na siasa, sasa anatumia rungu lake kutaka kumuonea kila anayeona anahatarisha maslahi ya chama chake,`` akadai Bi. Mdee.
SOURCE: Alasiri
My take: wakuu huu ni unyama uliokithiri,hivi kumfanyia mwanamke unyama wa aina hii utavumilika kweli? Hapana sasa inabidi wananchi wamtetee huyo mama wakamtoe kwa nguvu huko polisi maanke kama polisi walishindwa kumkamata mhalifu insteady wakamkamata victim,basi hata wananchi wakivamia kituo cha polisi jeshi hilo litakua limejitakia.Hizi sheria mwitu dawa yake ni civil disobedience full stop!
wakuu,
Hivi aliyeua mbwani nani? Ni polisi au wafuasi wa chama fulani? Liwe liwalo,wanaharakati wa haki za wanyama inabidi kulaani vikali kitendo hicho cha kikatili.
Ina maana mnyama alikua kosa gani mpaka watu wakurupuke kumuua? Kwa hiyo mnyama kauawa kisiasa? It is very disgusting kuona watu waliopewa akili wanakurupuka na kumuua mnyama aliyetumika kisiasa as if huyo mnyama alijivika hayo magwanda peke yake.
Tarime: Mbwa avaa fulana ya CCM,auawa, mmiliki akamatwa
Mbwa ambaye alivalishwa fulana ya CCM yenye picha ya mgombea ubunge wa chama hicho akiwa mitaani huko Tarime kabla ya kuawa na mmliki wake kutiwa mbaroni Alhamisi.
Frederick Katulanda na Mussa Juma, Tarime
KAMPENI za uchaguzi wa ubunge na udiwani wilayani Tarime zimezidi kuchukua sura tofauti baada ya watu wasiojulikana kumvalisha mbwa fulana yenye picha ya mgombea wa ubunge wa CCM, Christopher Kangoye na kurandaranda naye katika mitaa ya mji wa Tarime.
Kampeni hizo, licha ya kutawaliwa na kashfa na maneno makali kama zilivyo kampeni nyingine za kisiasa, zimekuwa na matukio mengine mengi yakiwemo ya kutunguana kwa mawe, majaribio yasiyofanikiwa ya biashara ya shahada za kupigia kura, kuchoma fulana za vyama na kupigwa mawe kwa gari la kampeni.
Lakini jana matukio hayo yalipanua wigo wake kutoka kwa binadamu aliyejaliwa akili za kujua mema na mabaya hadi kwa hayawani wa kufugwa.
Mbwa aliyekuwa amevishwa fulana ya rangi za kijani na njano yenye picha ya mgombea wa CCM, alionekana kuanzia majira ya saa 1:00 jioni akikatiza mitaa mbalimbali akiwa ndani ya nguo hizo zinazovaliwa na wafuasi wa CCM kumnadi mgombea wao kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Oktoba 12.
Haikueleweka mbwa huyo alivishwa fulana hiyo na watu gani, lakini polisi imemkamata mmiliki wa mbwa huyo, Robhi Ikwabe ili asaidie upelelezi wa kumnasa mtu aliyehusika na tukio hilo.
Kamanda wa polisi mkoani Mara, Liberatus Barlow alisema hadi sasa jeshi lake linawashikilia watu watatu ambao wanasadikiwa kuwa walionekana wakiwa wamemshikilia mbwa huyo na kupita naye mitaani kabla ya kumwachia aendelee na safari zake.
Ingawa haijabainika waliohusika walikuwa na nia gani, inasemekana kuwa watu walioshuhudia tukio la mbwa huyo, ambaye baadaye alikimbilia kwa mmiliki wake aliye eneo la kituo cha mabasi jirani na kituo kidogo cha polisi, huenda ni wafuasi wa Chadema kutokana na kudaiwa kuwa walikuwa wakionyesha ishara ya vidole ambayo ni alama ya chama hicho.
Katibu mkuu wa CCM, Yusufu Makamba alieleza kusikitisha na hali hiyo na kusema akiwa kama kiongozi mwenye uvumilivu suala hilo anawaachia maamuzi, ambao alisema ni wananchi watakaopiga kura kuchagua viongozi wao.
Alisema kuwa vurugu zinazoendela zinadhihirisha uhuni na kusema CCM ni chama cha wastaarabu, hivyo wanawaachia wananchi.
''Hizi ndizo siasa za wenzetu, sisi tunawaachia wananchi, maana hata sisi tunaweza kufanya hivyo kama tukiamua, lakini tutaonekana wote wendawazimu ndiyo maana nasema nawaachia wananchi wao ndiyo watakaoamua,'' alieleza Makamba.
Alisema ingawa nao wanazo bendera nyingi ambazo zimesalimishwa na wafuasi wengi wa Chadema, hawatathubutu kufanya hivyo.
Naye mgombea ubunge wa Chadema katika jimbo la Tarime, Charles Mwera aliwafukuza polisi katika msafara wake wa kampeni na kuwataka waende kukomesha mapigano ya koo badala ya kutumia fedha za umma kumfuata kwenye mikutano yake.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji Masanga juzi, Mwera alisema katika msafara wake hahitaji kundi la askari na magari kama ilivyo sasa kwani kama kuna umuhimu wa kuwa na askari angependa askari wasiozidi wawili.
''Mimi sina shida na askari najua mnatumia mamilioni ya fedha kutufuata, lakini kuna kazi za muhimu za kufanya kuzuia mapigano ya koo na kulinda amani maeneo mbalimbali nchini na sio sasa askari wote kujazana Tarime na badala yake kuwa kero,'' alisema Mwera.
Alisema yeye kama mwenyekiti wa halmashauri ni mkazi wa Tarime na hivyo haoni umuhimu wa kulindwa kwani yupo nyumbani kwake na mikutano yao haina matatizo kutokana na wananchi kufurahia sera za Chadema badala ya kashfa na uchochezi wa vyama vingine.
Akizungumzia migogoro ya kikabila katika wilaya hiyo, alisema kama akichaguliwa atahakikisha inamalizwa kwa mazungumzo na kujiepusha na kufanya kazi kwa misingi ya ukabila.
''Matatizo yenu ya mapigano tutayashughulikia kwa mazungumzo, matatizo ya wizi wa mifugo nayo yatashughulikiwa kwa umakini ili kuhakikisha wilaya hii inakuwa shwari wakati wote,'' alisema Mwera.
Naye, katibu mwenezi wa Chadema, Erasto Tumbo aliwataka wakazi wa Tarime kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kumpigia kura mgombea wa chama hicho bila hofu na kwamba hakuna ambaye anaiba kura zao kama wanavyodhania.
''Ukimaliza kupiga kura kaa mita 100 mbele ya kituo hadi matangazo ya matokeo yatakapobandikwa na wakimaliza sote twende halmashauri kusubiri kutangaziwa mshindi wetu kwani hakuna kulala siku hiyo hadi kieleweke,'' alisema Tumbo

Mbwa ana kosa gani?
Waliomuua mbwa na mbwa mwenyewe nani katenda kosa la jinai?
Hao wanaharakati ni wa Mbwa tu ama vipi? mbona sijasikia wanahakati wa mbuzi,ng'ombe,kondoo wanapochinjwa.Hii inanikumbusha kama sikosei ni mbeya ambapo mbwa alihukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupewa jina la binadamu.
Shallow arguinment as usual,kwa hiyo CCM mmechinja mbwa?
Hii inanikumbusha kama sikosei ni mbeya ambapo mbwa alihukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupewa jina la binadamu.
Sio jina la binadamu mkuu, aliitwa Immigration
Kwani mbwa haliwi??