Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
First Lady,
Twende hivyo hivyo tutafika tu... hushangai vifo vya Tabora kuna thread 3 lakini kwa kuwa muasisi ni Bwana mkubwa inabidi iwe hivyo tu...
![]()
Mbwa ambaye alivalishwa fulana ya CCM yenye picha ya mgombea ubunge wa chama hicho akiwa mitaani huko Tarime kabla ya kuawa na mmliki wake kutiwa mbaroni Alhamisi.
Damu yamwagika Tarime
Makubo Haruni, Tarime
Daily News; Saturday,October 04, 2008 @00:01
Watu wawili wafuasi wa CCM na Chadema wamekufa kwa kukatana kwa panga na kisu baada ya kutofautiana kimtazamo kuhusu ushabiki kwa vyama vyao juzi usiku. Kamanda wa Polisi Mkoani Mara, Liberatus Barlow, amewataja waliouana kuwa ni Mwita Marwa (25) na Manga Mesere (22), wote wakazi wa Kijiji cha Mangucha Kata ya Nyanungu.
Barlow alisema kwamba tukio hilo lilitokea juzi saa 12 jioni wakati marehemu hao walipokuwa wakinywa ulevini na kuanza kutoleana matusi yaliyosababisha Mesere kumjeruhi shingo Marwa ambaye kabla hajakata roho alimchoma Mesere kisu tumboni na kusababisha utumbo kumwagika.
Barlow aliongeza kuwa kutokana na vifo hivyo hakuna aliyekamatwa kwa sababu mahasimu hao waliuana baada ya kuchokozana wao wenyewe. Alisema Polisi itafanya uchunguzi na kuweka jalada hilo katika kumbukumbu. Hata hivyo, amewaonya wanasiasa waache siasa za mabishano na kumwaga damu ikiwa ni pamoja na kufikia hatua ya kuuana.
Wakati mauaji hayo yakitokea, juzi pia kulitokea kituko mjini hapa kwa mbwa kuvalishwa fulana ya CCM ya rangi ya kijani ambayo ilikuwa na picha ya mgombea ubunge wake Ryoba Kangoye. Tukio hilo lilitokea saa moja kasorobo usiku kwa mbwa huyo kufika eneo la Stendi bila kuhofu kelele za watu na kwenda kwa mmiliki wake, Robi Ikwabe, aliyekuwa akiuza vyombo vya ndani karibu na Kituo Kidogo cha Polisi.
Akizungumzia tukio hilo,Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba alikielezea kitendo hicho kuwa ni cha kihuni na kinaonyesha baadhi ya vyama vya siasa vinavyojimaliza. Alieleza kuwa CCM ina nguo, bendera na kadi nyingi za vyama vingine lakini haiwezi kuthubutu kuwavalisha mbwa au kuzichoma moto kadi hizo.
Kutokana na tukio hilo polisi wamewatia mbaroni, mama mmiliki wa mbwa na vijana wawili ambao wametajwa na Kamanda wa Polisi, Barlow kuwa ni Chacha Ikwabe,na Chacha Kitumbo ambao wanadaiwa kuhusika kumvalisha mbwa huyo fulana ya CCM. Baada ya kukamatwa kwa watu hao, mgombea ubunge kupitia Chadema, Charles Mwera na wa udiwani wa Tarime Mjini wa Chama hicho, John Heche, wametaka Polisi wawaachie mara moja.
Hii kali ya mwaka...
Kwanza walevi hao waligeuka kuwa wafuasi wa chadema na ccm na baadae wakawa wanasiasa kwa mujibu wa mwandishi na Kamanda Rwambow.
Pia nimeshangazwa sana na hatua ya Katibu mkuu wa ccm Bw Makamba kuwadharau mbwa kiasi hicho.
Hawa wazee wapumzike sasa....Hawajui kuna haki za wanyama nowadays?
Haki za watoto na wanawake zenyewe bado wanasuasua..Ama kweli wako waaay behind.
Habari hii bado pia imenichanganya kiana na ni muhimu kwa wananchi wa Tarime kuelewa kuwa watalishwa kila kitu this time around...
Mbwa/Mwenye Mbwa kukamatwa kwasababu eti ana nguo zenye rangi yenye kufanana na bendera ya chama cha Mavituz ni UNAZI.
Huku sasa ni kutapatapa...Yani badala ya sera ni ushabiki kama michezo?
Hivi mbona ni vituko?
Hii kwanza ni zaidi ya michezo na sasa ni kama Baath Party tu..No different..Hawa viongozi wa sasa wa ccm waachie madaraka mara moja na wawapishe vijana..
Yani kama ukiwafanyia wananchi yale wanayostahili kufanyiwa kuna hata haja ya polisi kuwakamata?
Si wananchi wenyewe watawafukuzia mbali?
Ama kweli Siku ya kufa nyani...
Kila unaposoma mambo ya Tarime unagundua jinsi nchi yetu na watu wake walivyo wajinga wa kutupwa.
Hivi kweli ingelikuwa kama huku West, Tambwe angepata wapi hata nguvu ya kusimama jukwaani na kusema hayo anayoyasema sasa? Waandishi wangemtolea hotuba zake za huko nyuma alipokuwa upinzani na hapo ndio ungelikuwa mwisho wake.
Hivi mtu unaweza kuzua jambo kubwa kama hili la kusema viongozi wa CHADEMA watakamatwa, bila ushahidi wowote na vyombo vya habari vikaandika?
Kumbe mambo yanayotokea hapa JF ni refection sahihi ya Tanzania na wananchi wake walipofikia.
Kwa Tanzania tunahitaji mabadiliko makubwa sana katika fikra za watu. Looh! jitihada zote za Nyerere inaelekea tumerudi hatua kumi nyuma, inasikitisha sana!
Kama hizi ndizo siasa, kweli tuna safari ndefu sana.