Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Jamani hii kazi kwelikweli mbwa anavishwa Jezi si mchezo!TARIME kweli nimewakubali
 
First Lady,

Twende hivyo hivyo tutafika tu... hushangai vifo vya Tabora kuna thread 3 lakini kwa kuwa muasisi ni Bwana mkubwa inabidi iwe hivyo tu...

Aboh kumbe MKjj ni Bwana mkubwa sikulijua hilo!ila tutafika tu
 
Damu yamwagika Tarime
Makubo Haruni, Tarime
Daily News; Saturday,October 04, 2008 @00:01

Watu wawili wafuasi wa CCM na Chadema wamekufa kwa kukatana kwa panga na kisu baada ya kutofautiana kimtazamo kuhusu ushabiki kwa vyama vyao juzi usiku. Kamanda wa Polisi Mkoani Mara, Liberatus Barlow, amewataja waliouana kuwa ni Mwita Marwa (25) na Manga Mesere (22), wote wakazi wa Kijiji cha Mangucha Kata ya Nyanungu.

Barlow alisema kwamba tukio hilo lilitokea juzi saa 12 jioni wakati marehemu hao walipokuwa wakinywa ulevini na kuanza kutoleana matusi yaliyosababisha Mesere kumjeruhi shingo Marwa ambaye kabla hajakata roho alimchoma Mesere kisu tumboni na kusababisha utumbo kumwagika.

Barlow aliongeza kuwa kutokana na vifo hivyo hakuna aliyekamatwa kwa sababu mahasimu hao waliuana baada ya kuchokozana wao wenyewe. Alisema Polisi itafanya uchunguzi na kuweka jalada hilo katika kumbukumbu. Hata hivyo, amewaonya wanasiasa waache siasa za mabishano na kumwaga damu ikiwa ni pamoja na kufikia hatua ya kuuana.

Wakati mauaji hayo yakitokea, juzi pia kulitokea kituko mjini hapa kwa mbwa kuvalishwa fulana ya CCM ya rangi ya kijani ambayo ilikuwa na picha ya mgombea ubunge wake Ryoba Kangoye. Tukio hilo lilitokea saa moja kasorobo usiku kwa mbwa huyo kufika eneo la Stendi bila kuhofu kelele za watu na kwenda kwa mmiliki wake, Robi Ikwabe, aliyekuwa akiuza vyombo vya ndani karibu na Kituo Kidogo cha Polisi.

Akizungumzia tukio hilo,Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba alikielezea kitendo hicho kuwa ni cha kihuni na kinaonyesha baadhi ya vyama vya siasa vinavyojimaliza. Alieleza kuwa CCM ina nguo, bendera na kadi nyingi za vyama vingine lakini haiwezi kuthubutu kuwavalisha mbwa au kuzichoma moto kadi hizo.

Kutokana na tukio hilo polisi wamewatia mbaroni, mama mmiliki wa mbwa na vijana wawili ambao wametajwa na Kamanda wa Polisi, Barlow kuwa ni Chacha Ikwabe,na Chacha Kitumbo ambao wanadaiwa kuhusika kumvalisha mbwa huyo fulana ya CCM. Baada ya kukamatwa kwa watu hao, mgombea ubunge kupitia Chadema, Charles Mwera na wa udiwani wa Tarime Mjini wa Chama hicho, John Heche, wametaka Polisi wawaachie mara moja.
 
mbwatarime.jpg

Mbwa ambaye alivalishwa fulana ya CCM yenye picha ya mgombea ubunge wa chama hicho akiwa mitaani huko Tarime kabla ya kuawa na mmliki wake kutiwa mbaroni Alhamisi.
 
Hawa Polisi nao wamezidi kuchukulia mambo for granted! Yaani wamesikia tu kwamba watu wameuana wenyewe wakaridhika? Ati hakuna uchunguzi zaidi? Hakuna walioshindwa kuzuia uhalifu? Hakuna walioshindwa au kuzembea kushughulikia majeruhi? Wamechomana visu wamekufa, imetoka? Liberati umesoma bwana hebu jitahidi kidogo kuonesha kuwa elimu inakusaidia!
 
Tarime: Mbwa avaa fulana ya CCM,auawa, mmiliki akamatwa

Mbwa ambaye alivalishwa fulana ya CCM yenye picha ya mgombea ubunge wa chama hicho akiwa mitaani huko Tarime kabla ya kuawa na mmliki wake kutiwa mbaroni Alhamisi.
Frederick Katulanda na Mussa Juma, Tarime

KAMPENI za uchaguzi wa ubunge na udiwani wilayani Tarime zimezidi kuchukua sura tofauti baada ya watu wasiojulikana kumvalisha mbwa fulana yenye picha ya mgombea wa ubunge wa CCM, Christopher Kangoye na kurandaranda naye katika mitaa ya mji wa Tarime.

Kampeni hizo, licha ya kutawaliwa na kashfa na maneno makali kama zilivyo kampeni nyingine za kisiasa, zimekuwa na matukio mengine mengi yakiwemo ya kutunguana kwa mawe, majaribio yasiyofanikiwa ya biashara ya shahada za kupigia kura, kuchoma fulana za vyama na kupigwa mawe kwa gari la kampeni.

Lakini jana matukio hayo yalipanua wigo wake kutoka kwa binadamu aliyejaliwa akili za kujua mema na mabaya hadi kwa hayawani wa kufugwa.

Mbwa aliyekuwa amevishwa fulana ya rangi za kijani na njano yenye picha ya mgombea wa CCM, alionekana kuanzia majira ya saa 1:00 jioni akikatiza mitaa mbalimbali akiwa ndani ya nguo hizo zinazovaliwa na wafuasi wa CCM kumnadi mgombea wao kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Oktoba 12.

Haikueleweka mbwa huyo alivishwa fulana hiyo na watu gani, lakini polisi imemkamata mmiliki wa mbwa huyo, Robhi Ikwabe ili asaidie upelelezi wa kumnasa mtu aliyehusika na tukio hilo.

Kamanda wa polisi mkoani Mara, Liberatus Barlow alisema hadi sasa jeshi lake linawashikilia watu watatu ambao wanasadikiwa kuwa walionekana wakiwa wamemshikilia mbwa huyo na kupita naye mitaani kabla ya kumwachia aendelee na safari zake.

Ingawa haijabainika waliohusika walikuwa na nia gani, inasemekana kuwa watu walioshuhudia tukio la mbwa huyo, ambaye baadaye alikimbilia kwa mmiliki wake aliye eneo la kituo cha mabasi jirani na kituo kidogo cha polisi, huenda ni wafuasi wa Chadema kutokana na kudaiwa kuwa walikuwa wakionyesha ishara ya vidole ambayo ni alama ya chama hicho.

Katibu mkuu wa CCM, Yusufu Makamba alieleza kusikitisha na hali hiyo na kusema akiwa kama kiongozi mwenye uvumilivu suala hilo anawaachia maamuzi, ambao alisema ni wananchi watakaopiga kura kuchagua viongozi wao.

Alisema kuwa vurugu zinazoendela zinadhihirisha uhuni na kusema CCM ni chama cha wastaarabu, hivyo wanawaachia wananchi.

''Hizi ndizo siasa za wenzetu, sisi tunawaachia wananchi, maana hata sisi tunaweza kufanya hivyo kama tukiamua, lakini tutaonekana wote wendawazimu ndiyo maana nasema nawaachia wananchi wao ndiyo watakaoamua,'' alieleza Makamba.

Alisema ingawa nao wanazo bendera nyingi ambazo zimesalimishwa na wafuasi wengi wa Chadema, hawatathubutu kufanya hivyo.

Naye mgombea ubunge wa Chadema katika jimbo la Tarime, Charles Mwera aliwafukuza polisi katika msafara wake wa kampeni na kuwataka waende kukomesha mapigano ya koo badala ya kutumia fedha za umma kumfuata kwenye mikutano yake.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji Masanga juzi, Mwera alisema katika msafara wake hahitaji kundi la askari na magari kama ilivyo sasa kwani kama kuna umuhimu wa kuwa na askari angependa askari wasiozidi wawili.

''Mimi sina shida na askari najua mnatumia mamilioni ya fedha kutufuata, lakini kuna kazi za muhimu za kufanya kuzuia mapigano ya koo na kulinda amani maeneo mbalimbali nchini na sio sasa askari wote kujazana Tarime na badala yake kuwa kero,'' alisema Mwera.

Alisema yeye kama mwenyekiti wa halmashauri ni mkazi wa Tarime na hivyo haoni umuhimu wa kulindwa kwani yupo nyumbani kwake na mikutano yao haina matatizo kutokana na wananchi kufurahia sera za Chadema badala ya kashfa na uchochezi wa vyama vingine.

Akizungumzia migogoro ya kikabila katika wilaya hiyo, alisema kama akichaguliwa atahakikisha inamalizwa kwa mazungumzo na kujiepusha na kufanya kazi kwa misingi ya ukabila.

''Matatizo yenu ya mapigano tutayashughulikia kwa mazungumzo, matatizo ya wizi wa mifugo nayo yatashughulikiwa kwa umakini ili kuhakikisha wilaya hii inakuwa shwari wakati wote,'' alisema Mwera.

Naye, katibu mwenezi wa Chadema, Erasto Tumbo aliwataka wakazi wa Tarime kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kumpigia kura mgombea wa chama hicho bila hofu na kwamba hakuna ambaye anaiba kura zao kama wanavyodhania.

''Ukimaliza kupiga kura kaa mita 100 mbele ya kituo hadi matangazo ya matokeo yatakapobandikwa na wakimaliza sote twende halmashauri kusubiri kutangaziwa mshindi wetu kwani hakuna kulala siku hiyo hadi kieleweke,'' alisema Tumbo
 
Damu yamwagika Tarime

Watu wawili wafuasi wa CCM na Chadema wamekufa kwa kukatana kwa panga na kisu baada ya kutofautiana kimtazamo kuhusu ushabiki kwa vyama vyao juzi usiku. Kamanda wa Polisi Mkoani Mara, Liberatus Barlow, amewataja waliouana kuwa ni Mwita Marwa (25) na Manga Mesere (22), wote wakazi wa Kijiji cha Mangucha Kata ya Nyanungu.

Barlow alisema kwamba tukio hilo lilitokea juzi saa 12 jioni wakati marehemu hao walipokuwa wakinywa ulevini na kuanza kutoleana matusi yaliyosababisha Mesere kumjeruhi shingo Marwa ambaye kabla hajakata roho alimchoma Mesere kisu tumboni na kusababisha utumbo kumwagika.

Barlow aliongeza kuwa kutokana na vifo hivyo hakuna aliyekamatwa kwa sababu mahasimu hao waliuana baada ya kuchokozana wao wenyewe. Alisema Polisi itafanya uchunguzi na kuweka jalada hilo katika kumbukumbu. Hata hivyo, amewaonya wanasiasa waache siasa za mabishano na kumwaga damu ikiwa ni pamoja na kufikia hatua ya kuuana.

Wakati mauaji hayo yakitokea, juzi pia kulitokea kituko mjini hapa kwa mbwa kuvalishwa fulana ya CCM ya rangi ya kijani ambayo ilikuwa na picha ya mgombea ubunge wake Ryoba Kangoye. Tukio hilo lilitokea saa moja kasorobo usiku kwa mbwa huyo kufika eneo la Stendi bila kuhofu kelele za watu na kwenda kwa mmiliki wake, Robi Ikwabe, aliyekuwa akiuza vyombo vya ndani karibu na Kituo Kidogo cha Polisi.

Akizungumzia tukio hilo,Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba alikielezea kitendo hicho kuwa ni cha kihuni na kinaonyesha baadhi ya vyama vya siasa vinavyojimaliza. Alieleza kuwa CCM ina nguo, bendera na kadi nyingi za vyama vingine lakini haiwezi kuthubutu kuwavalisha mbwa au kuzichoma moto kadi hizo.

Kutokana na tukio hilo polisi wamewatia mbaroni, mama mmiliki wa mbwa na vijana wawili ambao wametajwa na Kamanda wa Polisi, Barlow kuwa ni Chacha Ikwabe,na Chacha Kitumbo ambao wanadaiwa kuhusika kumvalisha mbwa huyo fulana ya CCM. Baada ya kukamatwa kwa watu hao, mgombea ubunge kupitia Chadema, Charles Mwera na wa udiwani wa Tarime Mjini wa Chama hicho, John Heche, wametaka Polisi wawaachie mara moja.
 
Ohh noo...........maskini mbwa, kiumbe hiki kinahusishwa na tabia chafu za kisiasa.....na hatimaye kuuawa!!!!........too bad kwa kweli
 
Huyo aliyemuua mbwa anatakiwa kushitakiwa kwa kudhulumu haki ya mnyama kuishi. Miaka ya nyuma alitokea mtu mmoja akampa mbwa wake jina "Immigration". Mmiliki huyo aliposhitakiwa mahakama ya mwanzo hakimu akatoa amri kuwa mbwa auawe. Nakumbuka hilo jambo wanaharakati wa haki za wanyama walilipigia kelele sana, sijui liliishia wapi. Hili la mbwa huyu aliyeuawa ati kwa "kosa la kuvalishwa tisheti ya CCM" hebu wanaharakati tusaidiane jamani, ni ukatili wa ajabu! Mbwa huyu hakuwa na utashi wa kuamua avae tisheti hiyo au la, kwa nini anauawa?
 
ONLY in Tanzania!...
Yaani Makamba ktk yote hayo alichokiona kitendo kibaya sana ni huyo mbwa kuvishwa jezi ya CCM...Hivi kuna mtu anaweza kunambia tusi kubwa la mbwa huyo kuvishwa jezi ya CCM kiasi kwamba hukumu yake iwe kifo?..na Makamba wala asizungumzie kitendo hicho kuwa ni cha kinyama badala yake wanatafutwa vijana waliokisiwa kufanya hivyo... What if...ni mtu wa CCM aliyemvisha mbwa huyo hiyo jezi kuonyesha ushabiki wa chama hata kwa mbwa wake!... mbona nchi za Ulaya na Marekani ambazo tunaiga kila wanalolifanya huvishwa mbwa bendera za nchi yao, hulala nao kitandani, hula nao sahani moja na kadhalika iweje leo ktk mfumo wa kampeni za kuiga imported demokrasia tunaweka mbele mila ambazo zinapingana na kile tunachoiga!..
Ikiwa kweli CCM wana machungu kuona mbwa kavishwa jezi lao kutokana na mila zetu kuhusiana na Mbwa basi turudi ktk basics... Wabunge wetu warudi kuwa wale Machief wetu!...hapo tamaduni na mila zetu zitaweza kutumika kirahisi na nadhani itapunguza sana hizi siasa za kuiga wakati hutafahamu kabisa nini maana ya vyama vingi isipokuwa Uadui.
Ni aibu kubwa sana kwa kiongozi kama Makamba kuendesha Udikteta ambao wazi unaonyesha kwamba Ukichoma bendera ya CCM hukumu yako inaweza kuwa kifo.....Uchungu wake hauwezi kufikiria nje ya kuwa amepoteza roho ya mtanzania mmoja kwa sababu ya bendera isiyokuwa na Uhai wala ufunuo..
 
Damu yamwagika Tarime
Makubo Haruni, Tarime
Daily News; Saturday,October 04, 2008 @00:01

Watu wawili wafuasi wa CCM na Chadema wamekufa kwa kukatana kwa panga na kisu baada ya kutofautiana kimtazamo kuhusu ushabiki kwa vyama vyao juzi usiku. Kamanda wa Polisi Mkoani Mara, Liberatus Barlow, amewataja waliouana kuwa ni Mwita Marwa (25) na Manga Mesere (22), wote wakazi wa Kijiji cha Mangucha Kata ya Nyanungu.

Barlow alisema kwamba tukio hilo lilitokea juzi saa 12 jioni wakati marehemu hao walipokuwa wakinywa ulevini na kuanza kutoleana matusi yaliyosababisha Mesere kumjeruhi shingo Marwa ambaye kabla hajakata roho alimchoma Mesere kisu tumboni na kusababisha utumbo kumwagika.

Barlow aliongeza kuwa kutokana na vifo hivyo hakuna aliyekamatwa kwa sababu mahasimu hao waliuana baada ya kuchokozana wao wenyewe. Alisema Polisi itafanya uchunguzi na kuweka jalada hilo katika kumbukumbu. Hata hivyo, amewaonya wanasiasa waache siasa za mabishano na kumwaga damu ikiwa ni pamoja na kufikia hatua ya kuuana.

Wakati mauaji hayo yakitokea, juzi pia kulitokea kituko mjini hapa kwa mbwa kuvalishwa fulana ya CCM ya rangi ya kijani ambayo ilikuwa na picha ya mgombea ubunge wake Ryoba Kangoye. Tukio hilo lilitokea saa moja kasorobo usiku kwa mbwa huyo kufika eneo la Stendi bila kuhofu kelele za watu na kwenda kwa mmiliki wake, Robi Ikwabe, aliyekuwa akiuza vyombo vya ndani karibu na Kituo Kidogo cha Polisi.

Akizungumzia tukio hilo,Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba alikielezea kitendo hicho kuwa ni cha kihuni na kinaonyesha baadhi ya vyama vya siasa vinavyojimaliza. Alieleza kuwa CCM ina nguo, bendera na kadi nyingi za vyama vingine lakini haiwezi kuthubutu kuwavalisha mbwa au kuzichoma moto kadi hizo.

Kutokana na tukio hilo polisi wamewatia mbaroni, mama mmiliki wa mbwa na vijana wawili ambao wametajwa na Kamanda wa Polisi, Barlow kuwa ni Chacha Ikwabe,na Chacha Kitumbo ambao wanadaiwa kuhusika kumvalisha mbwa huyo fulana ya CCM. Baada ya kukamatwa kwa watu hao, mgombea ubunge kupitia Chadema, Charles Mwera na wa udiwani wa Tarime Mjini wa Chama hicho, John Heche, wametaka Polisi wawaachie mara moja.

Hii kali ya mwaka...

Kwanza walevi hao waligeuka kuwa wafuasi wa chadema na ccm na baadae wakawa wanasiasa kwa mujibu wa mwandishi na Kamanda Rwambow.

Pia nimeshangazwa sana na hatua ya Katibu mkuu wa ccm Bw Makamba kuwadharau mbwa kiasi hicho.

Hawa wazee wapumzike sasa....Hawajui kuna haki za wanyama nowadays?

Haki za watoto na wanawake zenyewe bado wanasuasua..Ama kweli wako waaay behind.

Habari hii bado pia imenichanganya kiana na ni muhimu kwa wananchi wa Tarime kuelewa kuwa watalishwa kila kitu this time around...
 
Jamani kwa hili la mbwa inabidi nitoe dukuduku langu,huyo mama alikuwa stend akiuza vyombo sasa inakuwaje hao polis bilakufikilia wamkamate mama wawatu ambaye kwanza hajui nn kinaendelea na hao polis waache unafiki mbona walivyo muona huyo mbwa walikuwa wanacheka,nn maana yakucheka ni kwamba walikuwa wamefurai sasa kwann wamchukue mama wawa watu wakati yeye hausiki.mbwa mwenye mpole utadhani mbwa mbuzi hata mtu yeyote anaweza kumwita ukaenda nae.
 
Mbwa/Mwenye Mbwa kukamatwa kwasababu eti ana nguo zenye rangi yenye kufanana na bendera ya chama cha Mavituz ni UNAZI.
Huku sasa ni kutapatapa...Yani badala ya sera ni ushabiki kama michezo?
Hivi mbona ni vituko?
Hii kwanza ni zaidi ya michezo na sasa ni kama Baath Party tu..No different..Hawa viongozi wa sasa wa ccm waachie madaraka mara moja na wawapishe vijana..
Yani kama ukiwafanyia wananchi yale wanayostahili kufanyiwa kuna hata haja ya polisi kuwakamata?
Si wananchi wenyewe watawafukuzia mbali?
Ama kweli Siku ya kufa nyani...
 
Hii kali ya mwaka...

Kwanza walevi hao waligeuka kuwa wafuasi wa chadema na ccm na baadae wakawa wanasiasa kwa mujibu wa mwandishi na Kamanda Rwambow.

Pia nimeshangazwa sana na hatua ya Katibu mkuu wa ccm Bw Makamba kuwadharau mbwa kiasi hicho.

Hawa wazee wapumzike sasa....Hawajui kuna haki za wanyama nowadays?

Haki za watoto na wanawake zenyewe bado wanasuasua..Ama kweli wako waaay behind.

Habari hii bado pia imenichanganya kiana na ni muhimu kwa wananchi wa Tarime kuelewa kuwa watalishwa kila kitu this time around...

Mkuu soma vizuri ni kamanda BARLOW na si RWAMBOW kamanda RWAMBOW ni RPC Mwanza na si Mara
 
Nashukuru...Barlow...Unajuwa haya majina utafikiri sijui ni wazungu ama?
Marlow,Barlow...Halafu kuna Chico...Kama Spanish vile...

Anyways...Ujumbe umefika...Kuwa walevi hao wafuasi wanasiasa waliouwana huko ulevini...Ukiongezea na kisa cha mbwa bado utaona ccm wana shida kubwa sana.
 
Mbwa/Mwenye Mbwa kukamatwa kwasababu eti ana nguo zenye rangi yenye kufanana na bendera ya chama cha Mavituz ni UNAZI.
Huku sasa ni kutapatapa...Yani badala ya sera ni ushabiki kama michezo?
Hivi mbona ni vituko?
Hii kwanza ni zaidi ya michezo na sasa ni kama Baath Party tu..No different..Hawa viongozi wa sasa wa ccm waachie madaraka mara moja na wawapishe vijana..
Yani kama ukiwafanyia wananchi yale wanayostahili kufanyiwa kuna hata haja ya polisi kuwakamata?
Si wananchi wenyewe watawafukuzia mbali?
Ama kweli Siku ya kufa nyani...

Mkuu kwa mujibu wa habari ni kwamba Mbwa huyo alivalishwa fulana yenye rangi ya CCM na pia fulana hiyo ilikuwa na picha ya mgombea wa CCM...Kimsingi zinahitajika siasa na kampeni za kistaarabu na si za aina hii za kuwatumia wanyama wasio na ufahamu na kuwaua pasipo kuwa na hatia yoyote(wako wapi watetezi wa haki za wanyama????).....kwa kweli waliomtumia Mbwa huyu na waliomuua nina uhakika Mungu atawaadhibu kwa kitendo hiki cha kukatisha maisha ya kiumbe hiki kisicho na hatia.....Mbona USA kampeni zinafanyika lakini hakuna matukio ya magari kuvunjwa vioo,,viongozi kupigwa mawe,,mbwa kuvalishwa fulana nk..sababu ni nini hasa????,ni ujinga ama ni umasikini wetu??????????mhhhhhhhh....kaaaaazi kwelikweli...safari bado ni ndefu sana kufikia ukomavu wa kisiasa...kama nia Dar-Mbeya saa hizi ndo kwanza gari lipo maeneo ya Mbezi Luguruni
 
Kila unaposoma mambo ya Tarime unagundua jinsi nchi yetu na watu wake walivyo wajinga wa kutupwa.

Hivi kweli ingelikuwa kama huku West, Tambwe angepata wapi hata nguvu ya kusimama jukwaani na kusema hayo anayoyasema sasa? Waandishi wangemtolea hotuba zake za huko nyuma alipokuwa upinzani na hapo ndio ungelikuwa mwisho wake.

Hivi mtu unaweza kuzua jambo kubwa kama hili la kusema viongozi wa CHADEMA watakamatwa, bila ushahidi wowote na vyombo vya habari vikaandika?

Kumbe mambo yanayotokea hapa JF ni refection sahihi ya Tanzania na wananchi wake walipofikia.

Kwa Tanzania tunahitaji mabadiliko makubwa sana katika fikra za watu. Looh! jitihada zote za Nyerere inaelekea tumerudi hatua kumi nyuma, inasikitisha sana!

Kama hizi ndizo siasa, kweli tuna safari ndefu sana.

Mkuu,

Sasa umeongea maneno mazito,lakini please and please achana na matusi dhidio ya watanzania mkuu.Una tatizo gani? Unajua unaweza kujenga hoja bila kuweka hilo neno "Wajinga"?

Anyway,bravo kwa mchango wako
 
wakuu,

Hivi aliyeua mbwani nani? Ni polisi au wafuasi wa chama fulani? Liwe liwalo,wanaharakati wa haki za wanyama inabidi kulaani vikali kitendo hicho cha kikatili.

Ina maana mnyama alikua kosa gani mpaka watu wakurupuke kumuua? Kwa hiyo mnyama kauawa kisiasa? It is very disgusting kuona watu waliopewa akili wanakurupuka na kumuua mnyama aliyetumika kisiasa as if huyo mnyama alijivika hayo magwanda peke yake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom