Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Mkuu,inawezekana aliyemvalisha mbwa huyo alikua na nia nzuri tu labda uanzi kwa CCM ulikua umezidi.Kaazi kwa waliomuua.Nadhani akili haikushiriki ktk maamuzi
 
Send this article

Tarime: Ni utata mtupu!

2008-10-03 19:22:43
Na Emmanuel Lengwa, Jijini


Licha ya jitihada za Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kuwa hali ya amani na utulivu inaendelea kuwepo wakati wa Kampeni za kuwanadi wagombea wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa Mbunge katika Jimbo la Tarime, hali bado imeendelea kuwa tata kutokana na kuongezeka kwa matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani ambapo jana, mama mmoja na wanawe wawili wanadaiwa kupigwa na kumwagiwa pilipili kwenye nyuso zao.

Inadaiwa kuwa mama huyo na wanawe wamepata kipigo na kupakwa pilipili baada ya kuhusishwa na dhihaka ya kitendo cha mbwa mmoja kuonekana mtaani akiwa amevishwa nguo zenye bendera ya chama kimoja cha siasa.
Imedaiwa kuwa tukio hilo limetokea jana , mishale ya saa 9:00 mchana.

Ikadaiwa na mmoja wa mashuhuda kuwa baada ya mbwa huyo kuonekana mitaani, watu wanaodhaniwa kuwa ni makomandoo wa chama kinachohasimiana na kile ambacho bendera yake imevishwa mbwa, wakamkamata mama mwenye mbwa huyo na wanawe kabla ya kuwapeleka porini na kuwasulubu kwa kipigo na kisha kuwasiliba nyuso zao kwa pilipili.

``Kabla ya kuwapiga, mama huyo na wanawe walivuliwa nguo na kumwagiwa pilipili ... inasikitisha sana,`` akasema mmoja wa mashuhuda.
Hata hivyo, kiongozi mmoja wa kampeni wa CHADEMA, Bw. Msafiri Mtemelwa, amesema mama huyo na wanawe ni wafuasi wa chama chao na kwamba waliomtendea unyama huo ni watu wanaodhaniwa kuwa ni wa CCM.

Akasema Bw. Mtemelwa kuwa cha kushangaza, baada ya wao kutoa taarifa polisi, mama huyo na wanawe wakafuatwa huko waliko na kushikiliwa polisi badala ya wahusika wa tukio hilo kusakwa.

``Hivi sasa, tupo hapa Polisi tunashughulikia hatma ya mama huyu na wanawe... maana tunashangaa kuwa sisi ndio tuliotoa taarifa zake polisi ili asaidiwe, lakini badala yake yeye na wanae ndio wamekamatwa.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Liberatus Barow amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo la mbwa kuvishwa sare za CCM.

Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi, Kamanda Barow amesema amepata taafa za tukio hilo na kuwa yuko safarini kutoka Musoma mjini kwenda Tarime kulishughulikia.

``Taarifa ya tukio hilo nimezipata, lakini sina maelezo zaidi na hivi sasa niko njiani kwenda huko kulishughulikia,`` akasema Kamanda Barow.

Aidha Kamanda Barow ameiambia Alasiri kuwa tayari Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini,DCI, Robert Manumba, amewasili mkoani Mara ili kusimamia hali ya usalama.

Akasema pamoja na mambo mengine, DIC Manumba anakwenda kusimamia upelelezi wa sakata la usambazi wa waraka wa uchochezi unaodaiwa kusambazwa na Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila.

Katika hatua nyingine, baadhi ya viongozi wamekuwa wakilalamikia vitendo vya vurugu jimboni humo na kueleza kuwa havifai kwani ni vya hatari.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, CCM, Yusufu Makamba amelalamikia vitendo hivyo, vikiwemo vile vya kuzomewa kwa wagombea na pia viongozi wa chama chake wakati wa mikutano ya kampeni.

Amesema Makamba kuwa vitendo vya kuzomewa kwa viongozi vinaashiria vurugu ambazo zinaungwa mkono na wapinzani wao wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia, CHADEMA.

Hata hivyo alipoulizwa kuwa matukio hayo yanaathiri kwa kiasi gani mbio za chama chake za kulinasa jimbo hilo, Makamba alijibu kwa kifupi: ``Sina cha kusema. ``

Aidha, wakati Katibu huyo wa CCM akimwaga chozi dhidi ya hali ya vurugu ambayo amedai kuwa si njema kwani inazorotesha hali ya amani na utulivu, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe ambaye alikuwa pia jimboni humo, anadaiwa kuwa hadi sasa yuko nje ya nchi.

Imedaiwa kuwa Bw. Zitto yuko nchini Rwanda kwa shughuli za kikazi, kwani ana nyadhifa nyingi zinazomfanya awe akihitajika katika maeneo tofautitofauti.

Akizungumzia jambo hilo, Mwanasheria wa Chama hicho ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CHADEMA, Bi. Halima Mdee, amesema safari za Zitto haziwezi kuhusishwa moja kwa moja na yale yanayojiri kwenye kampeni za uchaguzi.

Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Bi. Halima amesema Zitto ni kijana jasiri na kuwa hawezi kukimbia kauli ya Mkuu wa wilaya ambaye anajua wazi kuwa hana ubavu wa kuamuru kukamatwa kwake.

``Binafsi namjua Zitto kuwa ni jasiri, ingekuwa ni kukimbia angekimbia wakati ule aliposimamishwa bungeni, lakini nimjuavyo hawezi kukimbia kauli ya mkuu wa wilaya,``akasema Bi. Mdee.

Akasema kilio cha muda mrefu cha vyama vya upinzani kuwa watendaji wanatumia madaraka yao vibaya kwa manufaa ya vyama vyao au wao binafsi kimedhihirika kupitia agizo la mkuu huyo wa wilaya.

``Kwa muda mrefu tumekuwa na kilio chetu juu ya watendaji wa Serikali, Mkuu wa wilaya pale anamuwakilisha rais, lakini inaonyesha kuwa hawezi kutenganisha majukumu yake na siasa, sasa anatumia rungu lake kutaka kumuonea kila anayeona anahatarisha maslahi ya chama chake,`` akadai Bi. Mdee.

SOURCE: Alasiri

My take: wakuu huu ni unyama uliokithiri,hivi kumfanyia mwanamke unyama wa aina hii utavumilika kweli? Hapana sasa inabidi wananchi wamtetee huyo mama wakamtoe kwa nguvu huko polisi maanke kama polisi walishindwa kumkamata mhalifu insteady wakamkamata victim,basi hata wananchi wakivamia kituo cha polisi jeshi hilo litakua limejitakia.Hizi sheria mwitu dawa yake ni civil disobedience full stop!
 

Mh...Kazi ipo...
 


Kaazi kwelikweli,
 
Watu huwwa wanabandika stika za kampeni kwenye magari, mbao za matangazo, kuta na nguzo za umeme. Wengine huvaa nguio zenye ujumbe wa kampeni, kuna shida gani kumtumia mbwa kutangaza ujumbe wa kampeni?
 
Hivi kweli vurugu zinaongeza kura zozote? Hivi hatuoni dalili zote zinazoonyesha tunaelekea walikofika Kenya?

Mheshimiwa Masha, shusha jeshi lote la polisi huko Tarime ili kuokoa maisha na mali ya watu. Watu maskini hatutakiwi kabisa kujiingiza kwenye vitu vya kijinga hivi. Umaskini mwingine ni wa kujitakia kabisa.

Wakati Tarime mnatiana mapengo na kuharibiana mali, hawa wanasiasa ikifika tarehe 13/10 wanarudi kwao kwenye familia zao huku wamewaachieni machangu kwenu.

Inasikitisha sana!
 
Chondechonde wanatarime acheni kumwaga damu tofauti yenu ya mtizamo iwe chachu ya kuleta mawazo bora yatakayo elekeza viongozi kufikia maamuzi bora.Nawaomea kwa mungu awajalie busara na utengamano.
 

Hao wanaharakati ni wa Mbwa tu ama vipi? mbona sijasikia wanahakati wa mbuzi,ng'ombe,kondoo wanapochinjwa.

Hii inanikumbusha kama sikosei ni mbeya ambapo mbwa alihukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupewa jina la binadamu.
 

Kazi ipo.....
View attachment 2637
Mbwa ambaye alivalishwa fulana ya CCM yenye picha ya mgombea ubunge wa chama hicho akiwa mitaani huko Tarime kabla ya kuawa na mmliki wake kutiwa mbaroni Alhamisi. - Mwananchi



Wafuasi wa CHADEMA na NCCR-Mageuzi wakishangilia huku wakimpitisha mitaani mbwa aliyevishwa fulana yenye nembo za CCM, mjini Tarime juzi. - Majira
 
Kumuua huyu mbwa ni kumwonea, kwani hakuivaa mwenyewe. Kumkamata mmiliki wa mbwa...sijui?
 
Hizo ni kampeni, hakuna mwenye kosa Mbwa wala mmiliki wake..sidhani kama wamemtendea haki kuumua huyo mbwa. Kampeni zina vituko vingi sana, akina Komba kukata mauno mbele ya kadamnasi basi katika kuvuta wapiga kura. Mbwa amefikisha ujumbe kwa akina Makamba et al mwisho wao hauko mbali sana. Hata tukiangalia kwenye kampeni za marekani wapinzani wa Republican wanatafuta mwanadada mwenye sura kama ya mgombea mwenza wa McCain, Sarah Palin acheze picha ya ngono...hii yote ni kuhakikisha replican hawashindi

Soma habari kamili hapa

Porn hunt for Palin double

Published: 03 Oct 2008

AN LA porn studio is hunting for a lookalike of US Republican vice-presidential candidate Sarah Palin. Porn mogul Larry Flynt has started advertising for the part, offering £1,700, according to online adverts.

"Looking for a Sarah Palin look-alike for an adult film to be shot in next ten days," one said. "Please send pix, stats etc."

America's multibillion-dollar pornography industry is centred in Los Angeles' San Fernando Valley region.

Source: The sun
 
Iweje mbwa auawe eti kwa sababu kavalishwa T shirt ya CCM?
Mbwa kakosa nini?
JE ni kosa la jinai kumvalisha mbwa T-shirt?
JE ni kosa la jinai kumvalisha mbwa T-shirt ya CCM?
Vipi je angevalishwa Kofia ya CCM?
Vipi mbwa huyo angepakwa rangi ya kijani na neno CCM ubavuni?
Vipi mbwa huyo angevalishwa kablasha la matangazo ya kampeni za CCM?

Mbwa kauawawa kwa kosa gani, wakati shati hakuvaa mwenyewe?

Mbwa ana kosa gani?

Waliomuua mbwa na mbwa mwenyewe nani katenda kosa la jinai?
 
Mbwa ana kosa gani?

Waliomuua mbwa na mbwa mwenyewe nani katenda kosa la jinai?

Bila shaka Mkuu Madilu, walioua Mbwa wana kosa, si la jinai, bali la mauaji. Mbona tunaona magari yamebandikwa picha za kampeni nayo hayachomwi moto!!!!!
 
Hao wanaharakati ni wa Mbwa tu ama vipi? mbona sijasikia wanahakati wa mbuzi,ng'ombe,kondoo wanapochinjwa.Hii inanikumbusha kama sikosei ni mbeya ambapo mbwa alihukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupewa jina la binadamu.

Shallow arguinment as usual,kwa hiyo CCM mmechinja mbwa?
 
Kama ni hivi 2008 Tarime, je 2010 Tanzania nzima, watapata wapi askari wa kuhakikisha ulinzi? Mimi naona kitendo cha viongozi wote kitaifa kujiingiza kwenye kampeni hii sasa tunaanza kuona madhara yake. Kulikuwa kuna ubaya gani kuwachia wahusika wajinadi peke yao, CCM kumleta Mtikila kuja kupandikiza chuki sasa wanaipeleka wapi nchi?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…